Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 15,999
Amani iwe kwenu.
Niimuda sasa nimeshuhudia vituko kutoka uongozi wa vyama vya upinzani hususani CUF na Chadema...na wamesababisha kushusha mvuto na kukosa hoja kwa wananchi.Sababu kuu ikiwa ni udhaifu wa vijana ambao umesababishwa na mambo yafuatayo;
1.Bavicha kwa sasa imegeuka "dodoki" na sio muhimili wa chama katika kusimamia misingi na itikadi ya chama asemalo Mbowe twende kazi.
2.Bavicha sio chungu cha kuandaa viongozi wenye itikadi ya chama kwani ifikapo uchaguzi Mbowe huamua nani agombee na hata kama ni mtu anayetoka CCM asiye na itikadi hupewa bendera na kutelekeza vijana ili kuongeza ruzuku mfano.Shibuda,Lembeli,Bulaya,Luwasa,Nangole,Kalanga etc.hawa wote sio Chadema na hawaamini katika Chadema angalia jinsi wanavyofanya siasa...hakika vipaji vingi kufa zaidi kwani vijana wa Luwasa ni lazima watatengeneza mustakabali wao ndani ya chama tusubiri 2019.
3.Bavicha na Cuf mmezidi kutowa matamko na hoja chafu zenye kupinga hata mazuri ya serikali..wananchi watawachoka mfano mlihubiria wananchi taifa linaweza kujitegemea leo mnakuja na hoja kwamba bila wazungu tutakufa,mnajidharaulisha.
4.Bavicha na Cuf hamna tabia ya kukemea viongozi na wanachama wanaotowa kauli za kudharaulisha chama kwa umma mfano Luwasa mara kwa mara anatowa kauli zinazotoa taswira kuwa chadema kinaunga mkono ufisadi..ikumbukwe UVCCM walimdhibiti luwasa na genge lake na kuzima ndoto....Nape,Makonda nk heko kwa uzalendo;hii taswira imefanya wananchi ghafla kuona kumbe Dr.Slaa alikuwa na hoja("siasa ni sayansi")
5.Imedhihirika sasa wabunge wengi;Lijuakali,Haule na viti maalum ambao wengi ni vijana uwezo wao ni mdogo kwanini hawaaminiwi kuongoza kamati hadi chama kimesusa..ikumbukwe kuwa ZZK aliweza kuongoza kamati muhimu kwa umahiri katika awamu yake ya kwanza
tu;..huu ni ushahidi kwamba bavicha ya sasa ni "substandard" imeleta wabunge "substandard".
6.Ikumbukwe Tanu youth league/uvccm, ANC youth league sio" rubber stamp" ,angalia Malema alipokuwa ANCYL alimkemea Zuma hadharani hadi kufukuzwa na sasa kaunda chama tishio EFF....;kazi nzuri ya uvccm imevuwa magamba mazito RA,EL nk na kuleta uelekeo mpya na uongozi mpya.
Shime Bavicha;Saanane,Yeriko,Malisa,Heche ,Mnyika,Kilewo,Wenje nk mmejikita zaidi kutoa propaganda za uongo FB na JF na sio siasa zenye tija..Chama cha siasa kinahitaji viongozi wenye itikadi na sio siasa za kuunga unga,kuazima wagombea kipindi cha uchaguzi.Jukumu la bavicha sio maandamano,matukio na matamko bali hata kukemea uongozi wa chama pale misingi inapokiukwa.