Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Baraza vijana CHADEMA tumesikitishwa na namna ambavyo jeshi la Polisi linatumika kukandamiza Demokrasia ya nchi.
Tumeshangazwa na kitendo cha Polisi kuzuia mkutano wa hadhara uliokuwa ufanyike Kahama june 07, na badale yake waka wapiga mabomu viongozi na wanachama wetu na wakaona haitoshi wakatumia maji ya kuwasha na risasi za moto ilimradi tu kuharibu mkutano
Katika hali ya kushangaza zaidi nipale Jeshi la Polisi lilipopiga marufuku mikutano ya vyama vya siasa kinyume na utaratibu wa katiba ya Jamuhuri ya Muungano.
Katiba ya nchi inatambua uwepo wa vyama vingi na CHADEMA imesajiliwa hivyo kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa na Katiba ya jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inaruhusu kufanya siasa mahali popote katika nchi hii.
Pamoja na hayo katika sheria hiyo hakuna mahala popote inaonyesha kuwa Jeshi la Polisi ndio lenye mamlaka ya kutoa vibali vya mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa.
Kwa sasa Jeshi la polisi limekuwa vibaraka wa watawala na kujipendekeza na jeshi limepoteza weledi wa kiuwajibaki kwa kuwalinda raia na mali zake.
Katika vyama vya siasa jeshi lina kazi mbili kubwa,kwanza kupokea taarifa ya vyama vya siasa kuhusu mikutano yao na , pili ni kulinda mikutano hiyo jambo ambalo ndio kazi haswaa ya jeshi la Polisi
BAVICHA tunaona kila dalili ya machafuko dhidi ya Polisi na raia wema wanaodai haki yao ya kikatiba ya kusikiliza viongozi wao na wawakilishi wao wanasema nini
Tunawaomba viongozi na wanachama wote nchini kusikiliza kauli ya chama juu ya uhuni wa jeshi na safari ya kudai Demokrasia ya kweli itaendelea bila kuchoka,bila na woga wowote
Imetolewa June 08
Imetolewa na BAVICHA Taifa.