BAVICHA taifa kuna tatizo?

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,096
2,000
Wacha tu niseme ya kwangu moyoni kwani msema kweli ni mpenzi wa Mungu, kuuficha ukweli ni unafki, kama kuna kitu hakiko sawa ni lazima lisemwe tu provided kuna upande mmoja utachekelea na mwingine utalalamika.

Haiwezekani tukawa tunajivuta vuta hivi juu ya suala la kupotea kwa Mwenzetu Ben Saanane, Ben alikua mpiganaji mkubwa sana hasa kukitetea chama na vijana kwa ujumla. Mengi aliyafanya bila kuogopa mtu wala kikundi cha watu akidhani kua Mungu Pekee ndiye mtetezi wake, Pia aliamini pia sisi vijana tutaweza kusimama nyuma yake.

Mtu anapotea tunaonesha reaction ndogo sana as if hatumjui, As if kazi yake hatuitambui!! Yalitokea ya Mazwazo ikaonekana tumeguswa kiasi flani japo tulibaki kulalamika tu pasipo kuonesha nia thabiti ya kupinga vitendo hivi.

Tumemwachia Malissa na kundi lake wakilalamika na kuhenya tu unafikiri hakuna taasisi kubwa inayoweza kusimama kuhakikisha kuwa kwa namna yeyote ile Ben anapatika, mimi sikubaluani kabisa kupwaya huko! hapana there is something wrong with BAVICHA.

Hivi tunategemea Mwenyekiti Mbowe atuambie ni hatua ipi inapaswa kuchukuliwa? Inawezekana kabisa Mbowe anaitizama activeness ya BAVICHA na ndio maana yeye kama kiongozi mkuu wa Chama hajazungza lolote.Nilitegemea BAVICHA wangetoa hata muda kwa mamlaka husika kusema kama Ben yupo au hayupo lijulikane moja na sio Ukimya huu.

Hili suala lingetokea kwa akina Julius Malema wa Afrika Kusini pasingekalika kule, this is a very traumatizing issue!! Sio kwa Mwendo huu!! Mimi nakataa kabisa.
 

Mwasita Moja

JF-Expert Member
Dec 31, 2015
2,906
2,000
Bavicha wako bize kushangilia na kudeki barabara ili mafisadi wapite.

Chezea mrungula wewe
 

Alen K

JF-Expert Member
Dec 8, 2016
221
225
Ni kweli lipo tatizo maana siwaoni hata kwenye ziara za kujenga chama!
 

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
15,552
2,000
Tumemwachia Malissa na kundi lake wakilalamika na kuhenya tu unafikiri hakuna taasisi kubwa inayoweza kusimama kuhakikisha kua kwa namna yeyote ile Ben anapatika, mimi sikubaluani kabisa kupwaya huko! hapana there is something wrong with BAVICHA
Kuna tatizo la 'power struggle' kati ya Malisa na kundi lake, Ben Saanane dhidi ya BAVICHA ni suala la wakati tu. Malisa anatengeneza mazingira ili aonekane yeye ni bora kuliko BAVICHA alafu kuna ile tabia ya kwanini BAVICHA iongozwe na watu wasiotoka kaskazini?
 

Alexism

JF-Expert Member
Aug 14, 2011
3,430
2,000
Mleta mada ongeza na ili...kwanini polisi na upelelezi wa serikali ya CHADEMA hawafanyi haki katika kumtafuta Ben kama wanavyo angaika na Faru John..PolisiCDM Mungu anawaona.
 

KAPURO

JF-Expert Member
Feb 12, 2016
235
250
Mtoa mada mbona na wewe unalalamika tu bila kutoa ufumbuzi acha unafiki na wewe.
Unafiki gani MTU kusema ukweli?
Ndani ya BAVICHA kuna tatizo kubwa haiwezekani MTU anapotea ktk mazingira tatanishi tena alikuwa kiongozi ndani ya chama then hakuna kiongozi yeyote aliyejitokeza kuhoji, au kutuambia Ben yuko wapi????? Huu ndio unafiki wenyewe. Bavicha tunapaswa kulinda na kutetea maslahi ya wanachama wote.
Hapo lazima tupige pelele.
Mwenyekiti wetu Bavicha Patrobas utuambia kuna tatizo gani??? Ukumbuke wewe ni kiongozi tu umepewa dhamana tu
 

swissme

JF-Expert Member
Aug 15, 2013
13,660
2,000
Kwako wewe Kutumbuliwa Magembe ni bora zaidi kuliko kuonekana Saanane.

Ndio maana mimi naamini Chadema mnajua aliko Saanane.!
CHADEMA&co tunajua aliko na hapo ccm na serikali yake lazima tuwabane tu.


swissme
 

Kigodoro

JF-Expert Member
Apr 25, 2014
1,645
2,000
Mkuu mleta mada nchi imefika hapa ilipo kwasabb ya uoga. unashangaa la ben saanane? mangapi yametokea nchi hii lkn watu wako kimya wanabaki kulalamikia chinichini.. hii ndiyo tabia ya watz na bavicha ni watz.

umeongelea akina julius malema. ndg yangu usifananishe watu hai na wafu. waafrika kusini ni watu hai, hawajaanza leo kulianzisha. angalia movie ya sarafina utajua nasema nn.

unawalaumu bure bavicha, watanz ndivyo tulivyo ukiwemo na ww. ww mbona hujatoka hadharani kama kweli unaumizwa na kupotea kwa mtanz mwenzako?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom