BAVICHA: Salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu Philemon Ndesamburo

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
BARAZA LA VIJANA WA CHADEMA TAIFA (BAVICHA)​

Salamu za rambirambi kwa Familia ya Marehemu PHILEMON NDESAMBURO na wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro na Kanda ya Kaskazini kwa ujumla.

BAVICHA tumepokea kwa mshtuko mkubwa sana,kifo cha Mheshimiwa Ndesamburo Kama muasisi wa siasa za mageuzi katika taifa letu, na muasisi wa CHADEMA tegemeo na nguzo imara kwa chama chetu na taifa, aliejitoa kwa hali na mali kuipigania haki na usawa kwa wananchi kupitia chadema.

Mzee Ndesamburo amekuwa Mbunge wa Moshi mjini kwa kipindi cha miaka 15 mfululizo, M/kiti wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro na mjumbe wa baraza kuu la chama mpaka umauti unapomkuta jana tarehe 31/05/2017

Mzee Ndesamburo amekuwa muhimili mkubwa sana,kwa siasa za Mkoa wa Kilimanjaro na kanda ya Kaskazini,kwa kuwa mfanya biashara pekee alionesha njia kwa wafanya biashara wengine kuwaunga mkono wapinzani jambo ambalo halikwepo awali kwakuwa wafanyabiashara wengi walikuwa waliogopa kulinga na vitisho vilivyokuwa vikitolewa na watawala.

Baba umeondoka katika kipindi unachohitajika sana, ulikuwa ni ngao na jeuri ya wagombea wetu wa ubunge katika majimbo ya mkoa wako na kanda yako, magari na fedha zako zilitumika kipindi chote cha uhai wako kuipigania Demokrasia na ukombozi wa nchi yetu.

Sisi vijana tumekuwa tukijifunza mengi kwako, umekuwa mshauri mzuri kwetu ninani ataichukua nafasi hii ya ushauri wako kwetu?? umewavutia vijana wengi kuingia katika siasa za mageuzi kupitia Chadema wakitamani kuwa kama wewe baba, taa imezimika wamebaki kwenye kiza kinene tafadhali Baba kama unaweza amka japo utuambie neno la mwisho umeondoka ghafla baba hatukujiandaa bila uwepo wako Mzee wetu.

Tunakulilia Baba, kwa maumivu na uchungu mkali ndani ya mioyo yetu pamoja na maswali mengi tuliyo nayo kwanini umeondoka kipenzi cha watu lakini mwisho wa siku kazi ya Mungu haina makosa pumzika Baba ,tutakuenzi kwa vitendo.

Watumishi wa Mungu wanakulilia, wachungaji kwa mashehe kwakuwa ulikuwa kiungo na msaada mkubwa baina yao kwa ushauri na michango ya ujenzi wa nyumba za ibada kwakuwa uliamini hakuna jambo jema kama kumtegemea Mungu.

Baba nakumbuka mwezi wa nne ulishiriki kuimba kwaya, moja wapo hapo Moshi mjini na ukashoot video ambayo wewe ulisema huo ni ukumbusho kwako na wajukuu zako wajue kuwa babu alikuwa mcha mungu,kumbe kweli ulikuwa unatuaga?? Ndesamburo Mzee wetu ni majuzi tu umepokea tuzo ya uongozi bora kwa mkoa wa Kilimanjaro nani atafuata nyayo zako,? Simba wa mlima Kilimanjaro umeondoka ile hali una nguvu ya kufanya mawindo kutulisha wanao.

Nenda Mwamba,nenda nguli wa siasa za mageuzi, mkweli, jasiri usiyeyumbishwa "Ndesa Pesa" Tangulia baba .

Imetolewa leo 01/06/2017

M/kiti wa BAVICHA Taifa
PATROBAS KATAMBI
 
Back
Top Bottom