BAVICHA Mnafanya nini?

Freeland

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2012
Posts
14,481
Reaction score
10,233
“Vijana msilale, lale lale. Vijana msilale, bado mapambano! Mapambano, mapambano!

"Na sisi hatulali,lali lali.Na sisi hatulaliii,bado mapambano!


Huu ni wimbo Maarufu ambao ulitamba nchini Kenya katika liberation movements RIP Otieno Kajwang

Baraza la Vijana la CHADEMA ,BAVICHA linabeba dhamana kubwa sana ya kuitikia chorus katika wimbo huo wa Otieno Kajwang.Mapambano bado yanaendelea ,tena ndio yamepamba moto.Lakini kwa nini BAVICHA imelala?

BAVICHA inabeba matumaini makubwa kwa taifa hili ambalo kwa takwimu za sensa ya mwaka 2012 ni taifa la vijana.

Sensa ya mwaka 2012 ilionesha taarifa zifuatazo

[TABLE="width: 500"]
[TR]
[TD]Umri
[/TD]
[TD]Idadi ya watu
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Miaka 0-4
[/TD]
[TD]7,273,832
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Miaka 4 hadi 14
[/TD]
[TD]12,451,624
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Muaka 14 hadi 17
[/TD]
[TD]2,779,070
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Miaka 17 hadi 60
[/TD]
[TD]18,179,978
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Miaka 60 hadi 65
[/TD]
[TD][TABLE="width: 145"]
[TR]
[TD] 2,507,568
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Miaka 65 na kuendelea
[/TD]
[TD]1,736,851
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Jumla
[/TD]
[TD]44,928,923
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Ukisoma Takwimu hizo za baraza la taifa la Takwimu (National Bureau of Statistics | Statistics for Development) ni kwamba zaidi ya watanzania milioni 30 ni Vijana.Hawa ndio BAVICHA inabeba matumaini yao yote.

Kati yao Milioni 22 ni vijana na watoto chini ya miaka 17.BAVICHA ianabeba matumaini yao.

BAVICHA Inatakiwa itambue kwamba serikali iliyopo imeshindwa kulisaidia taifa hili hasa katika hali ya maisha ,elimu,afya ,ajira,kuondokana na subsistence economy n.k

BAVICHA walifanya Uchaguzi mwishoni mwa mwaka jana na kupata viongozi wapya

Cha kushangaza sana baraza hili limekuwa kimya kupita kiasi....hakuna kazi zozote zinazoonekana kufanywa na baraza hili....Tulitarajia katika wakati huu vijana hawa wangekua field kuhamasisha wananchi katika mazoezi anuwai ya kitaifa....hasa ukiwa ni mwaka wa uchaguzi mkuu...hatujasikia comment zozote za BAVICHA katika maswala mazito yaliyolikumba taifa....Naomba kukumbusha...Taifa letu ni taifa la Vijana...YOUTH agenda sio ya kukwepa...Wameshindwa kujua kuwa wanabeba matumaini ya idadi kubwa ya Vijana.?

Nauleta huu uzi kwenu ili tuweze kuchambua na kuliweka wazi tatizo la BAVICHA ili waweze kulisaidia taifa kuvuka katika mkwamo huu.


[h=1][/h]
 
Hoja hii ni ya msingi sana. Hatuoni kazi ya uongozi wa Bavicha hadi sasa. Kweli amkeni unganisheni vijana, hamasisheni watu kujiandikisha, ingieni vijijini, changisheni fedha za kampeni. Fanyeni kazi banaaaa!!
 
Kwa statistics hizi vijana hawatakuja kuisha nchi hii, sababu naona tayari watoto ni wengi kuliko vijana.
 
Hoja hii ni ya msingi sana. Hatuoni kazi ya uongozi wa Bavicha hadi sasa. Kweli amkeni unganisheni vijana, hamasisheni watu kujiandikisha, ingieni vijijini, changisheni fedha za kampeni. Fanyeni kazi banaaaa!!

Operesheni Delete CCM ambayo iliwaonesha CCM 'rangi zote' kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ilisimamiwa na BAVICHA waliokwenda kwa staili ya infantry (wakati Mwenyekiti wa Taifa na Katibu Mkuu Dk. Slaa wakipiga angani), mikoa ya Dodoma, Morogoro, Singida, Tabora, Katavi, Kigoma.

Majuzi wamefanya ziara ya mkoa mzima wa Kagera ambako walizindua operesheni kubwa itakayosambaa nchi nzima kuhusu kujiandikisha na kupiga kura, na sehemu ya Geita. Infantry kaka ndiyo inayoongoza vita.

Wakati unasubiri kuwaona 'wakipiga makelele', vijana wanakwenda chini kwa chini na athari yao kote wanakopita majibu wanayo CCM.

 
Miaka 20-30 ijayo mifuko ya jamii itafirisika. CCM idhbitiwe haraka kutumia hela za hizi mifuko.
 
Nani kamziba mdomo mwenyekiti mpya wa BAVICHA Patrobas Katambi? Ukimya wake si wa kawaida.
 

Thanks 4 the +ve info mkuu
 

Asante sana Tumaini Makene

Kazi inayopigwa na vijana wa Bavicha kila mtu anaona na kuithamini.

Kwa kuongezea tu ulipoishia Makamu Mkiti Ole Sosopi amekuwa na operesheni ya muda mrefu katika mikoa ya nyanda za juu kusini.

Na ni jana tu Vijana wa Bavicha wakiongozwa na Philipo Mwakibinga wamemaliza operesheni ya mwezi mmoja huko Mufindi Kaskazini.

Matokeo mazuri ya uchaguzi wa mitaa mwaka jana huwezi kutenganisha na Bavicha.

Bavicha siyo kama vijana wa CCM wanaoropoka tu kwa kila jambo wanalofanya.
 
Last edited by a moderator:
Viatu vya John Heche vimempwaya P.Katambi nakama sio hivyo basi huenda Bavicha imebadili mbinu
 

Mkuu Tumaini Makene, hii ya kufukuza mwizi kimyakimya ndiyo mbinu pekee niliyokuwa naiogopa. Hii imefanywa sana na ccm Wakati huo sisi tukiwa mabarabalani tukihamasisha watu kwa maandamano na hamasa za hapa na pale.

Sasa kama hili ndilo linalofanyika, hakika napongeza kwa nguvu zang zote, Oparesheni ya mlango kwa mlango, kijiji kwa kijiji ni nzuri na hatari kwa uwepo wa ccm. Kama kuna haja ya kuongeza nguvu kwenye hili iongezwe tafadhari ili twende na kasi ya huu mwaka. Hii inatakiwa iwe ni non stop tukitoka wilaya hii twende hii mkoa huu twende ule.... Naam kimyakimya kana kwamba hatupo.!!

Ila pamoja na hayo, makelele ya hapa na pale majukwaani hayatakiwi kusimama, Tunamakamanda wengi wahamasishaji wazuri tujigawe ktk makundi mawili, Team,Kimyakimya na. Team Majukwaani. Hii iwe ni mpaka mwezi wa kumi kama ni wakati wa kupuuza kazi zetu binafsi kwaajili ya chama ni huu, Tusilale!!

Pamoja na yote Kamanda Patrobas Mkiti Chadema taifa atoke hadharani apige kelele wengi wanataka kusikia na kuona nguvu yake bila kutumia viongozi wakuu wa chama. Nimeona Naibu Mkiti akijitahidi kidogo tena nisiseme kidogo sanaaa.... anapiga kazi kwelikweli..!! Patrobas ashtuliwe afanye kitu na roho za vijana Chadema zisuuzike naamini anaweza.

Kila lakheri.

BACK TANGANYIKA
 
Last edited by a moderator:
 
Asante sana Kamanda wangu wa habari ukweli utatuweka huku na sita vumilia mtu yoyote anaye kwenda kinyume na chama Changu
 
Sio kila anayetifautiana na wewe kimtazamo nankifikra basi unampa jina la ACT au msaliti, hizo sio siasa mkuu.

Sita Tetereka na watu kama nyie sanasana tutawa delete kwenye operation delete ccm
 

Asante sana pacha kazi ya Bavicha inaonekana ndani na nje ya Tanzania
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…