Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Salamu kwa vijana na watanzania wote wapenda amani katika nchi yetu.
Tuna shukuru Mungu kwakuwa zoezi letu la kuendelea na uratibu wa kwenda Dodoma kuzuia mkutano haramu wa CCM inaendelea vizuri sana.
Jana tulikuwa Tanga na jioni kikao cha mwisho cha uratibu tulikifanya Singida na hari ya vijana kwenda Dodoma kulisaidia jeshi la Polisi ipo juu sana,na mpaka sasa katika Center ya kupokea majina tayari tuna vijana zaidi ya elfu5 walio tayari kufika Dodoma.
Utakumbuka malengo yetu ni kufikisha vijana elfu mbili na mpaka sasa tumeweza kuvuka lengo tulilojiwekea kwa muda mfupi sana,Jambo la jema kwetu ni kwamba wapo mpaka wana CCM walijitolea kutufadhili kuwafikisha vijana Dodoma kwa lengo la kuona hii double standard inakomeshwa mapema ili nchi yetu ibaki kuwa na umoja,amani na ushirikiano kama awali,
BAVICHA tunatoa wito vijana wetu kuendelea kujiandaa kufika Dodoma, na kuacha kusikiliza maneno ya upotoshaji kutoka kwa wapinzani wetu kuwa tunaenda kufanya fujo.
Ieleweke kwamba BAVICHA tunaenda kusimamia agizo la Rais na jeshi la Polisi la kukataza mikusanyiko yote ya kisiasa mpaka mwaka 2020, hicho ndicho kinafanya twende Dodoma kama raia wema kutoa msaada kwa jeshi la Polisi na si vinginevyo.
Intelijensia ya BAVICHA inatuonesha kwamba Polisi ni wachache mno na hawatakuwa na uwezo wa kuzuia mkutano huo haramu wa CCM, ama kwa uchache wao au kwa kutishiwa na watawala kwakuwa mmoja ya mjumbe wa mkutano huo ni raisi wa jamuhuri ya muungano.
BAVICHA tunataka kuona kama kweli rais anaweza kusimamia maamuzi yake au ataingiza uchama katika hili, jambo ambalo litamshushia heshima zaidi kwa watanzania.
Imetolewa July 05
Edward Simbeye
Idara ya uhamasishaji
BAVICHA Taifa