Basi la Scorpion la kutokea Shinyanga kwenda Kasulu lilitekwa na majambazi

Watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wameliteka basi la abiria lenye namba za usajili T 116 BHD mali ya kampuni ya Scorpion lililokuwa likitokea mkoani Shinyanga kuelekea Kasulu mkoani Kigoma na kisha kuwapora vitu mbalimbali abiria waliokuwa wakisafiri katika basi hilo.
.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo akiwa katika kituo kidogo cha polisi cha Makere, Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma Kamishna Msaidizi wa polisi James Manyama amesema tukio hilo limetokea katika pori lililopo jirani na kambi ya wakimbizi ya Nduta.
.
Aidha, katika tukio jingine Kamanda Manyama amesema jeshi hilo limeendelea na operesheni maalumu na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa mbalimbali pamoja na magunia 18 ya bangi yaliyokuwa yakitarajiwa kusafirishwa kuelekea nchi jirani ya Burundi.
View attachment 1817570
 
Ukute na wewe umebeba hela za mauzo ukaweka mfukoni daaah Wana wanapita nazo zote ..... Jiwe aliwaambia maaskari ukikamata jambazi piga risasi hakuna kupeleka Mahakamani , na Kabla ya kumuua mnambinya mapumbu mpaka aseme wenzake wako wapi , mnawasaka wote mnawapiga risasi hakuna kulemba.....katika watu waliokuwa wanamuogopa jiwe basi ni majambazi .....!! Kwa maraisi wote kwenye Hilo jamaa ni excellent performer
😂😂😂kwamba abanwe mbupu
 
ITV wanatangaza kutekwa kwa basi la kubeba abiria linalofanya safari zake Kati ya Mwanza na Kigoma.

Basi linalomilikiwa na kampuni ya Scorpion leo limetekwa na abiria kuporwa vitu vyote walivyokuwa navyo na kupokea kipigo.

Mambo Kama haya tulikuwa tumeshayasahau kabisa Sasa ndio wamerudi kwa kasi na wanateka mchana kweupe bila woga.

Miaka ya nyuma basi zilitekwa na watu kuuwawa, kubakwa na hata kuvuliwa nguo kwenye kadamnasi.

My take : rais asipokuwa makini tutaanza kukodi askri wa escorting na kulipa mapesa tena


USSRView attachment 1815483
RPC wa huko bado yuko ofisini? Mama fukuza hao mbona watafanya Kazi seems wanashinda Bar
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom