Basi La Abood Lapata Ajali Mbaya

MaxShimba

Platinum Member
Joined
Apr 11, 2008
Posts
36,008
Reaction score
4,093
[h=3]TUKIO KAMILI: BASI LA ABOOD NAMBA T 545 AZE LA KUTOKEA DAR KWENDA TUNDUMA LAPATA AJALI MAENEO YA SAE(MBILINYI) BAADA YA KUGONGANA NA KENTA LILILO SABABISHA AJALI HIYO, MMOJA AFARIKI HAPO HAPO![/h]
​
Hivi ndivyo basi La Abood lilivyo pata ajali baada ya kugongana na Kenta​
​
Basi la Abood ​
​
Hivi ndivyo Basi Lilivyo Haribika ​
​
Haya ni mambaki ya Vioo vilivyo vunjika​
​

​
​

​
​
Baadhi ya vitu vikiwa vimemwagika chini​
​

​
​
Hili ni Scania ambalo lilikuwa likitokea Zambia ​
​

​
​

​
​
Dirisha likiwa limevunjika ​
​

​
​
Baadhi ya Abiria wakiwa wanapata maelekezo kutoka kwa polisi ​
​
Hapa ndipo basi la Abbod lilipo gonga ​

​
*********************​
BASI LA ABOOD LENYE USAJILI WA NAMBA T 545 AZE LIMEPATA AJALI MAENEO YA SAE SEHEMU MAARUFU KWA JINA LA KWA MBILINYI LIKITOKEA DAR ES SALAAM KUELEKEA TUNDUMA. AJALI HIYO IMETOKEA BAADA YA LORI LA MIZIGO AINA YA SCANIA LIKIWA LIMETOKEA ZAMBIA KUELEKEA DAR WAKATI WA KUTAKA KUPISHANA NA BASI HILO, NA NDIPO GARI AINA YA KENTA IKAJITOKEZA NA KUJICHOMEKA BARABARANI NA KUSABABISHA AJALI HIYO.​

​
KATIKA AJALI HIYO MTU MMOJA AMBAYE ANAITWA CHALE KITELEKE AMBAYE PIA ALIKUWA NDIYE KONDA WA BASI HILO AMEFARIKI PAPO HAPO, PAMOJA NA MAJERUHI NANE AMBAO WAMEKIMBIZWA HOSPITALINI .​

​
MPAKA TONE MEDIA LIVE GROUP AMBAO NI WAMILIKI WA MTANDAO HUU TUNATOKA ENEO LATUKIO HIZO NDIZO TAARIFA TUMEFANIKIWA KUZIPATA.​

​
HABARI KAMILI ITAWAJIA KESHO BAADA YA KUPATA TAARIFA KUTOKA POLISI.​

​
PICHA ZOTE NA: MBEYA YETU BLOG
​
 
Hivi bado mabasi yanaendeshwa usiku..?
 
Jina la Kituo cha Mbilinyi ni kwa heshima ya baba yake Joseph aka SUGU Mbunge wa Mbeya Mjini
 
SUMATRA na wadau wa usafiri waangalie hili swala la mabasi ya safari ndefu wawe na madereva wa kupokezana, najua huku ni kuongezeana gharama ila manufaa yake ni zaidi ya gharama husika. Dereva wa basi akikalia kiti chake kuanzia saa 1 asubuhi mpaka saa 4 usiku, uchovu, kelele za engine zinapunguza sana ufanisi wa maamuzi ya papo kwa hapo.
 
Hivi bado mabasi yanaendeshwa usiku..?
Madame tunduma ni kama kilometa 1000 toka dar hivyo kama itatoka saa 12.30 asubuhi na ikienda wa spidi ya wastani wa 80 kph pamoja na saa 1.30 muda unopotea njiani kwenye mizani, police check points, kula na kuchimba dawa safari huchukua karibu saa 14 na ushee hivi.
 
Nahic mungu anajibu kwa yale makanisa yalio chomwa dar
 
Yaani mabasi ya Abood huwa ni kawaida kupata ajali, bila shaka wanatoa kafara hawa wamiliki.

Subiri muda si mrefu ABOOD itanunua mabasi mapya.

Kuna wakati yalikuwa yanaitwa (CHINJA CHINJA)

Tumewazoea ......... wanakera sana.

RIP MAREHEMU.




MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Kwa hiyo waliochoma makanisa ndo walikuwa kwenye bus ama mmiliki ndo aliechoma? Na hii comment umeisema kwa sababu una uchungu wa kuchomewa kanisa lako?
Nahic mungu anajibu kwa yale makanisa yalio chomwa dar
 
..... Hii ndiyo miezi ya ajali............. ndo kwanza zimeanza.... nahisi wanachukua stock taking ya kufunga mwaka..... tumuombe Mungu na majanga haya ya mwisho wa mwaka....................MUNGU AIPEUSHILIE MBALI
 
Kwa hiyo waliochoma makanisa ndo walikuwa kwenye bus ama mmiliki ndo aliechoma? Na hii comment umeisema kwa sababu una uchungu wa kuchomewa kanisa lako?

kwenu nyinyi linawauma mimi sio ulivyofikiria ila kuzama kwa meli z'bar mlisema sababu ya kuchomwa makanisa je yanayotokea huko vipi inawezekana sababu ni hiyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…