basi gani zuri liendalo mwanza?

kama vipi njoo kwangu nitakupeleka usiku by air ungo
 
hivi uzuri wa basi nini? nauli mwendo wa dereva au bodi ya gari hiyo kwa nje? au huduma azipatazo mtu ndani ya gari? nisaidieni kuelewa hili kabla sijajibu.

Rangi mama, rangi ya basi ndo kila kitu
 


Hayo mabasi ni mazuri kwa mwendo lakini seat zake zinaumiza mgongo hazina tofauti na za kosta.
 
rangi ????????????????????? ya basi ndio kila kitu? dereva wake akiwa mlevi na anaendesha kwa mwendo wa ajbu kwako itakuwa sawa mkuu?

Kumbe majibu unayo unauliza nn sasa.
Ushawahi kuona mtu anabisha kwa asilolijua?
Unajua kabisa sifa za bus zuri hapa unaleta longolongo tu
 
Hayo mabasi ni mazuri kwa mwendo lakini seat zake zinaumiza mgongo hazina tofauti na za kosta.

kweli, ni basi aina ya YUTONG made for chinese people ni wafupi ndo maana zinatupa shida cc watanzania. hazina space ya kutosha btn one seat and another... but ziko adjustable nway
 
Shukrani bus services 45000/ mwanza sa tatu usiku unaingia full luxury mwendo ni reasonable ofisi ubungo oil com
 
Kama bado hujasafiri panda HAPPYNATION mkuu nilisafiri nao juzi wako vizuri
 
Panda Nshashi bus service. ( kesheni mkiomba. Dreva baba madebe.
 
Msaada tutani..
Ni basi gani zuri luxury liendalo mwanza lenye huduma nzuri pamoja na mwendo mzuri (usiokuwa wa mbio)

Nakushauri utumie FastJet.
Fast and lowcost.
 
Basi zuri ni Fast Jet nauli buku 32 tu.. Sema dereva anakimbiza sana masaa mawili tu upo mwanza..

Sema jiandae hakuna pipi wala maji ya bure humo, kila kitu unanunua
Hili basi limenivutia ha ha haa!!Lakini hii bei inanipa utata mbona cheap sana ulipata ofa nini au wajuana na wauza tiketi counter??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…