Mdude_Nyagali
Member
- Dec 11, 2022
- 84
- 1,494
Juzi akiwa katika jukwaa la mjasiliamali na mfanyabiasha wa neno la Mungu Mwamposa huko Arusha Bashite alisikika akiwakemea viongozi wa dini wanaotoa matamko ya kupinga utekaji na mauaji katika taifa letu. Bashite alienda mbali kidogo na kusema kwamba hata Yakobo alivyokatwa kichwa na Petro kufungwa gerezani kanisa halikutoa tamko kama makanisa haya yanavyotoa matamko.
Kwa lugha nyingine ni kwamba Bashite anaunga mkono watu kutekwa, kupotezwa na kuuawa na matamko ya makanisa yanamkera. Naona niwaombe viongozi wangu wa dini maaskofu, mapadri, wachungaji na wazee wa makanisa mnipe kibali nimpe elimu kidogo ya Theology huyu kibaka na bumunda anayefanya utani na neno la Mungu.
Kwanza bwana Bashite unapaswa kujua kwamba wakati Yakobo anakatwa kichwa ulikuwa wakati wa utawala wa Roma Empire ambao ulipiga marufuku ukristo karne ya kwanza baada ya Yesu. Kwamba ukristo ulikuwa haramu na haukusajiliwa na dini pekee zilizopitishwa na serikali ya Roma Empire ni dini za kipagani pamoja na dini ya kiyahudi. Kuhubiri ukristo ilikuwa sawa na kuuza bangi ni haramu hilo jukwaa la kutoa matamko wanalitoa wapi wakati tu kusajiliwa kwenyewe hawajasajiliwa? Ama na nyie katika serikali yenu na Samia ukristo ni haramu hivyo ni marufuku kutoa matamko?
Pili bwana Bashite nakupa elimu kwamba matamko ya kanisa yalianza kutolewa karne ya 3 baada ya maridhiano ya wakristo na serikali ya Roma Empire chini ya kaisari Konstantino Mkuu. Kwamba wakati huo ukristo ukasajiliwa na kutambuliwa rasmi kuwa ni miongoni mwa dini zinazotambulika na utawala wa Roma. Kuanzia wakati huo kanisa lilianza kukemea maovu na wafalme waliheshimu sana matamko ya kanisa tofauti na nyie na Samia mnaoleta dharau na kubeza.
Tatu bwana Bashite kabla ya ukristo kulikuwepo manabii na mitume. Ninaposema manabii na mitume simaanishi huyo mfanyabiasha wa neno la Mungu aliyekualika na kukupa share za mauzo ya udogo na mafuta. Namaanisha manabii na mitume kama akina Eliya, Elisha, Yeremia, Isaya, Daniel na wengine.
Sasa nakupa machache kuhusu manabii na matamko dhidi ya watawala. Mnamo karne ya sita kabla ya kuzaliwa Yesu masihi, nabii Isaya alitoa tamko dhidi ya utawala wa mfalme Uzia dhidi ya haki kwa kuwadhulumu wananchi, yatima na wajane. Katika tamko hilo Isaya alisisitiza utawala wa Uzia kukomesha dhuluma - Soma Isaya 1:17. Hata hivyo mfalme Uzia alimpuuza nabii Isaya na Mungu akampiga ugonjwa wa ukoma akafa kama kuku wa kideli.
Nabii Yeremia alitoa tamko kuhusu haki na dhuluma kupotea katika taifa. Yeremia aliishia kukamatwa na akina Bashite na Mafwele wa wakati huo kisha kupewa kesi za uchochezi.
Kwa hiyo bwana Bashite kanisa kutoa tamko la kukemea maovu yakiwemo utekaji na mauaji katika taifa ni msingi wa imani ulioanzishwa na Mungu mwenyewe kupitia manabii na mitume wake tangu zamani mpaka sasa. Ukitaka kufuta matamko ya makanisa dhidi ya serikali maana yake mshauri Samia afute makanisa. Tofauti na hapo makanisa yanaendelea kutoa matamko.
Mdude Nyagali 7 x 70 Sumu ya Nyigu.