Bashite angeng'oka kwa Katiba ya Kenya?

CattleRustler

JF-Expert Member
Oct 26, 2013
1,055
467
Msaada wanao ijua vizuri katiba ya Kenya. Ni sheria gani ya katiba ya kenya ingeweza kumng'oa Bashite kama tungekua na katiba yao?.
 
Katiba ya Kenya ya nini? Sheria za nchi yetu zinatosha kumng'oa. Tatizo la nchi yetu kuna ombwe kubwa la utawala wa sheria. Watu wanajaribu kuongoza nchi kwa ubabe na kufuata hisia zao na siyo katiba na sheria.
  • Tunajua kabisa ni kosa la jinai mtu kufoji vyeti. Anapashwa kufukuzwa kazi na kufungwa. Tingatinga alinza na gia hiyo hiyo ya msako wa vyeti feki. Wengi wamepoteza kazi, wengi wamekimbia kazi. Hiyo sheria mbona haina meno kwa mtu fulani? Double standards in udikteta wa hali ya juu.
  • Kavamie na wewe kituo cha utangazaji ulazimishe wahusika watangaze unachotaka uone nini kitatokea. Tena nenda mchana tu hata bila wembe mkononi. Lakini mtu kafanya kituko ambacho hatujawahi kukishuhudia nchini kabla na baada ya uhuru na anadunda tu. Why? because sheria inakuwa sheria mtu mmoja akijisikia. It is a shame to my country and utter nonsensical governance!
 
Nyetk ndio maana naona ni vizuri kujadili katiba yetu tukilinganishq na ya kenya. Maana maana hatuwezi kulazimisha DPP kufanya lolote na Mwakenyembe kashasema ushaidi uliopo ni wa upande mmoja (maelezo ya clouds na hata ripoti ya Nape )

Kwenye swala la vyeti pia wameuchuna na hata upinzani wanachofanya ni kwenda tume ya maadili ambapo sina moyo nako kabisa.

Nchi kama marekani wanasheria hua wanafunguaga mikesi tena kwa kuwashawishi walalamikaji kama njia ya kutengeneza jina au hata kufaidika na sehemu ya fidia anayopata mlalamikaji

Sasa najiuliza je niwanasheria wa bongo wanatuangusha au nisheria haziwapi motisha kufungua kesi maana Mtikila pekeyake ndie aliekua akifungua kesi alipokua hai.

Kama ni sheria haziwapi motisha wanasheria kufungua kesi. Je Kenya na katiba yao mpya gazeti au mwansheria binafsi anaweza kufungua kesi bila kungojea serekali?

Hii kesi ya Bashite ndio fursa nzuri ya kuonyesha uzaifu wa katiba yetu na jinsi katiba mpya kama ya kenya ilivyo tatua uzaifu wa katiba. Tatizo sina ujuzi wa katiba.
 
Mkuu CattleRustler sijui interest yako ni nini ktk kutaka kufanya comparison kati ya katiba ya Kenya na ya kwetu.
sijui katiba ya kenya ikoje, najua ya kwetu na seria zetu kuhusiana na jambo tunalojadili. Mi nadhani hapa ni uhuru na nguvu ya mihimili ya dola nje ya utawala. Hayati Mchungaji Mtikila aliipeleka serikali (Dola ya utawala) mahakamani mara nyingi na akashinda. Wengi walikuwa wanaona kesi kama hizo za Mtikila hazina tija maana mwisho wa siku hazina masilahi yoyote binafsi. Lakini kwa kweli umuhimu wake ni kuirejesha serikali katika mstari, kuondoa utendaji wa dola kwa kutumia "executive orders" zilizo nje na katiba na sheria na kuweka hansadi kama rejea kwa wakati ujao.

Nchi kama Marekani uliyoitolea mfano bahati nzuri naijua vizuri. Wenzetu "Judiciary" iko huru na ina nguvu kiasi kwamba Mwana sheria mkuu anaweza kupinga executive orders za rais wake na ikiwezekana wanaweza kuipeleka serikali mahakamani na kuzuia utekelezaji wa matamko ya kiutawala. Meno hayo mhimili wetu wa mahakama na sheria hauna maana wote ni wateule wa rais.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
asa si ukawaulize wakenya wenyewe?mbona maswali mengine ya kijinga sana?
 
asa si ukawaulize wakenya wenyewe?mbona maswali mengine ya kijinga sana?

Kenya ndio nchi ya jirani ninayo fahamu iliyoweza kufanya mabadiliko ya Katiba karibuni. Na matunda yake ni vyonbo vya habari vina uhuru mkubwa sana kulinganisha na Tanzania.

Pili japo nilikua mdogo sana kipindi cha mauaji ya Robert Ouko. Ubabe wa Moi na Biwott uwezilinganisha na Bashite na aliemteua. Ubabe wa Kanu na Moi auwezi kutokea tena Kenya kwasababu katiba yao mpya imepunguza madaraka ya Raisi.

Tatu hata wanao somea sheria za katiba (constitution law) huwa wanazisoma katiba za inchi nyingine. Ndio maana kina Polepole/ Tume ya katiba waliangalia katiba za nchi nyingine kama India walipotengeneza mapemdekezo ya katiba

Kila mtu anajua katiba yetu inampa nguvu nyingi raisi na atuwezi kumshitaki akitoka. Sasa kama katiba ingebadilishwa kama Kenya nakupunguza madaraka ya raisi. Je tungekuwa na njia zipi za kumwajibisha Bashite?
 
Ndugu inshu ya Bashite ya kuforge vyeti in kosa la Jinai kulingana na kifungu namba 333,334,335 na 336 cha Penal Code, kifungu namba 337 cha sheria hiyo hiyo kimetoa adhabu kwa mtu atakae fanya hilo kosa

Hivyo basi kama ni kosa la jinai, jukumu la kuendesha mashtaka ya makosa kama haya wanayo serikali according sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai( Criminal Procedure Act),

Japokuwa sheria hiyo hiyo imeipa madaraka serikali kuendesha makosa ya jinai, sheria hiyo hiyo pia imetoa mwanya kwa mtu binafsi kufungua mashitaka (Private Prosecution).

Ugumu unakuja pale ambapo sheria hiyo hiyo ya mwenendo wa makosa ya jinai kuipa madaraka serikali tena, Director of Public Prosecution(DPP) anauwezo tena wa kuichukua hiyo case kutoka kwa Private Prosecutor na kuamua either kuendesha au kuifutilia mbali bila kutoa sababu za msingi, kwa mantiki hiyo hapo inakuwa ngumu sana kumshitaki hiyo jamaa kwa tuhuma zinazomkabili

Sheria hii inatakiwa ifanyiwe mabadiliko, madaraka ya D.P.P yapunguzwe, kitendo cha kuwa na mandate ya kufuta case atakavyo ni madaraka makubwa sana,
Madaraka ya Private prosecutor yaongezwe ili kutoa mwanya kwa raia kuweza kufungua kesi na kumshurutisha kiongozi yoyote ataekwenda kinyume na sheria.
 
sheria hiyo hiyo pia imetoa mwanya kwa mtu binafsi kufungua mashitaka (Private Prosecution).

Ugumu unakuja pale ambapo sheria hiyo hiyo ya mwenendo wa makosa ya jinai kuipa madaraka serikali tena, Director of Public Prosecution(DPP) anauwezo tena wa kuichukua hiyo case kutoka kwa Private Prosecutor na kuamua either kuendesha au kuifutilia mbali bila kutoa sababu za msingi

Rai Pazzy asante kwa elimu hapo juu ila ndio inakatisha tamaa. Nashidwa kuelewa uamuzi wa meya wa kinondoni kupeleka malamiko tume ya maadili ni bora kuliko kufungua mashitaka binafsi. Maana tume ya maadili sindio kinachenge waligoma kwenda na bado bungeni wananguvu.

Pia sijui kama katiba ya warioba ilisema chochote kuhusu uwezo wa DPP kufuta mashitaka ya mtu binafsi
 
Sina hakika kama katiba ya warioba ila ngoja ntafatilia kwa sababu ninayo halafu ntakupa mrejesho
 
Sasa hii ni kenya hapa au?? ukisikia akili za kitumwa ndio hizi hapa..

Nazani kufahamu kwanini upuuzi alioufanya Bashite clouds auwezi kutokea kwenye media za Kenya unaweza kutadia kujua chakufanya hapa Bongo.
 
Hapa sio Kenya na upuuzi uliopo kenya hapa Tanzania hauna nafasi
Tanzania national examination council ndio wakudhibitisha uhalali wa cheti cha Bashite aka Makonda. TNEC kimya utadhani wamepigwa dozi ya unga.
 
Kwani Kenya wana wakuu wa mikoa

Nazani wana Governor. Naona waliona waondokane kabisa na kuongozwa na wateule wa Rais ambao hata wakifanya ujambazi amuwezi kufanya lolote mpaka Raisi atakapo jisikia kumuondoa. Na uakika wananjia ya kuwawajibisha ma-governor wao.
 
Hapa sio Kenya na upuuzi uliopo kenya hapa Tanzania hauna nafasi

Wewe kenya vyombo vyao vya habari vinauhuru mkubwa sana. Uyo bashite angekua kenya watu wangenfanyia investigative reporting wakamweka uchi. Hapa bongo Gwajima kashawaambia historia ya jamaa lakini media zinaogopa kumchimba zaidi bashite.
 
Back
Top Bottom