Nassib Sanga
Senior Member
- Aug 11, 2012
- 169
- 110
Kwa simple observation yangu nimeona hiki chombo hakina nguvu kama Nay Wa Mitego alivowaimba. Kwa maana tumekuwa tukisikia wakitoa maonyo kwa wasanii kadhaa na wengine kuwafungia kabisa.
Msanii Diamond Platnumz alipotoa video ya "nasema nawe" aliyomshirikisha Khadija Kopa nilidhani watatoa onyo kwa sababu ya maudhui ya ile video. Tumeona wadada wakicheza isivyo kawaida na wengine mpaka wakilala chini wakikatika. Ikumbukwe video kama hiyo iliyotolewa na Offside Trick ya wimbo wao wa "Samaki" ilifungiwa kuchezwa kwenye vituo vya redio kwa sababu iko nje ya maadili. Video ya Diamond iliendelea kuchezwa kwenye vituo vyetu.
Juzi hapa msanii aliyeko chini ya Diamond katoa wimbo wa "Bado" akimshirikisha Diamond na katika video ile Diamond ameonekana akionyesha vitendo ambavyo havifai kuonyeshwa kwenye vituo vya TV (alipokuwa anamkiss yule mdada shingoni kwa maudhui ya kingono) lakini sijasikia BASATA wakisema kitu.
Kwa maelezo hayo naweza kusema BASATA wanamuogopa Diamond??