astalavista
Senior Member
- Jul 7, 2014
- 156
- 159
BASATA NALO NI JIPU LINALOHITAJI MTUMBUAJI.
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ni Shirika la umma lililoundwa kwa Sheria ya Bunge Na. 23 ya Mwaka 1984.
Historia inaonyesha kuwa, Sheria ya kuunda upya Baraza hili ilifanywa kwa kuunganishwa Sheria ya Baraza la Sanaa la Taifa ya Mwaka 1974 na Baraza la Muziki la Taifa (BAMUTA) ya Mwaka 1974.
Baraza liliundwa ili lisimamie maendeleo ya sanaa nchini, kinyume na hii kazi waliojipatia sasa ya kufungia wimbo/nyimbo ama wasanii na ambayo inaonyesha wanaiweza zaidi.
Kwa siku za karibuni tumeshuhudia wimbo kama VIVA ulioimbwa na Roma ukifungiwa,pia msanii Shilole akipata adhabu ya kufungiwa kujihusisha na sanaa,kabla ya hivi juzi kufungiwa wimbo wa Ney wa Mitego.
Kabla hatujafika mbali ni vema basi tukizitazama na kuzifahamu kazi za BASATA hili kwa ulewa wetu wa kawaida tuone kama watu hawa wanafanya kile wanachotakiwa kufanya ama la?
Kwa mujibu wa Sheria Na. 23 ya mwaka 1984,ambayo pia Baraza liliundwa,Majukumu ya Baraza ni pamoja na :
Kufufua na kuhimiza maendeleo ya kazi za Sanaa
Kufanya tafiti wa masuala mbalimbali ya sanaa
Kutoa ushauri na misaada ya kitaalamu kwa asasi au watu wanaojihusisha na shughuli za sanaa.
Kuratibu shughuli za sanaa zinazofanywa na watu au taasisi mbalimbali
Kutoa na kuimarisha mipango ya mafunzo kwa wadau wa sanaa
Kuishauri Serikali juu ya mambo yahusuyo maendeleo na uzalishaji wa kazi za
sanaa.
Kuhamasisha maendeleo ya sanaa kwa njia ya maonyesho,mashindano,matamasha, warsha na semina.
Kuanzisha, kukusanya na kuhifadhi ikiwa pamoja na zile zinazohusu watu,asasi, taasisi, vifaa na miundo mbinu inazohusiana na sanaa
Kusajili wasanii na wale wote wanaojihusisha na shughuli za sanaa.
Kwa upana wake hizo ndio kazi hasa za BASATA sasa chukua muda wako kujiuliza watu hawa wanafanya kile wanachotakiwa kufanya kwasasa?
Jiulize tena iko wapi kazi ya BASATA ikiwa Muziki wenye asili ya Kitanzania unapotea kadri wakati unapobadilika.
Ziko wapi ngoma za Asili? hata kama zipo je zina uhai? Wako wapi wasanii wa ngoma za asili waliojitutumua kwa nguvu zao wenyewe kama kina Wanne Star?
Hivi BASATA walishawahi kumpa mwaliko Wanne Star na wengineo japo kuwapa semina elekezi kwa kile wanachokifanya? Maana pia ni sehemu ya majukumu ya kazi zao.
Pata mfano huu,pale nyumbani kijijini kwa Babu yupo Tumpare(mtoto wa mama yangu mdogo) kwasasa Muziki anaosikiliza na kuutazama ni Bongo flava au muziki wa dansi.
Anasikiliza Bongo fleva ambayo wasanii wetu wanaiga kila kitu kutoka mataifa ya nje,Bwana mdogo huyu masikio yake yatapokea nyimbo zenye mahadhi ya Kinigeria na kimarekani zilizo katika lugha ya Kiswahili.
Vilevile Tumpare akipenda kusikiliza Muziki wa Dansi basi itamlazimu kusikia muziki wa dansi wenye sauti za wakongo,ama watanzania wanaotumia lafudhi za kikongo.
Sasa tujaribu kumpa ndoto ya kuwa Msanii mtoto huyu baada ya muda fulani, je tunafikiri ni aina gani ya muziki ataufanya? Kwake itakuwa ngumu kufanya sanaa yenye mahadhi ya kitanzania kwasababu jamii haikumkuza hivyo.
Ipo wapi kazi ya BASATA juu ya kukuza na kuinua sanaa nchini, ziko wapi bendi za muziki zenye wasanii wenye kuutambulisha Utanzania wetu?
BASATA imeshindwa kuibua, kukuza na kuendeleza sanaa nchini na ndiyo sababu msanii kama Ney wa Mitego ambaye mtaa umemkuza sehemu ambayo anawasikia wanamuziki wa Kimarekani wakiimba, au hata wasanii wa nyumbani ambao pia walikopi toka ughaibuni.
Acha watu waige Hiphop,Mziki wa kimarekani na ambao mara nyingi umetawaliwa na matusi kwa sababu BASATA wameshindwa kuukuza na kuulinda mziki wa nyumbani.
Acha tuendelee kumsubiri DAVIDO toka Nigeria kuja kusambaza muziki wetu ng'ambo kwasababu wahusika wa sanaa yetu wameshindwa.
Yako wapi mashindano ya Miss utalii? vipi uhai wa Miss Tanzania kwasasa? na hata ile ya Maria Sarungi haisikiki tena..BASATA imeshindwa kuendeleza au kusadia hata pale wahusika waliponyesha kukwakama.
Yawezekana Ney kakosea sana lakini kwanini tumefika hapa, ni kwasababu kuna sehemu tuljikwaa na kwenye nyimbo za kina Roma na Ney ni kama sehemu ya tulipoangukia baada ya kujikwaa.
Kama Ney katukana ama kazusha sawa,hii watu wa sharia/sheria huuita 'Defamation' hivyo mhusika aliyeguswa atafuata taratibu za kisheria na haki itaonekana.
BASATA rudini kwenye Job descriptions zenu na mjitathimini wenyewe. Ni jipu nasema, na linahitaji upasuaji.
Astalavista!!