Mbao za Mawe
JF-Expert Member
- May 11, 2015
- 23,372
- 54,931
Naomba Mods Msichanganye uzi huu na wowote ule kuisadia BASATA na WASANII.
Wasalaam ndugu wana Jamii Forum nashukuru sana uwepo wa jarida hili la kupashana habari ambazo hata kwingineko hazisisiki ila humu utazipata.
Nianze moja kwa moja lengo la huu uzi, Kwa miaka nenda rudi kuna mtu amezuka na kutumia jina la BASATA na cheo ambacho sijui wasanii gani anawaongoza akijiita MWENYEKITI WA WASANII HAPA NCHINI na kudhulumu watu ambao hawajui chochote kumhusu huyo dada tapeli.
Huyu si mwingine ni Jackie Akinyi ni Binti Anaetokea katika wilaya ya Rorya (Mjaluo) ambae anafanya kazi za sanaa mara nyingi Nchini Kenya ila hii tabia yake ya kuonea na kuvaa vazi la MWENYEKITI WA WASANII HAPA NCHINI ni aibu na ni kejeli kwa wasanii pia ni Aibu kwa baraza la sanaa hapa Nchini kutumiwa vibaya na huyu dada ambaye naamini hajulikani hata kwenye ofisi za BASATA na wala anaweza kutojua zilipo.
Huyu dada akienda huko Kenya huwa anarudi na kuchukua maaskari na kuzunguka nao katika maeneo mbalimbali ndani ya mkoa wa Mara na baadhi ya maeneo katika jiji la Mwanza (Vijijini) akichukua hao askari huenda kibanda kwa kibanda na hujitambulisha kama Mwenyekiti wa wasanii na pia kama moja ya viongozi wa BASATA na huchukua vifaa katika vibanda vya wale wote wanaouza kazi za wasanii kwa kuzingatia sheria na taratibu zote, Vifaa hivyo ni pamoja na Computer baada ya kuchukua huelekea na wewe hadi kituo cha polisi na kuanza kukudai pesa ili uwr huru (Haya nayazungumza yashanipata ila yamejirudia kwa watu wangu wa karibu naumia sana).
Kwangu mimi lilinitokea 2013 nikiwa sehemu fulani ndani ya mkoa wa Mara alikuja na askari akabeba Computer pasi ukaguzi wowote na kusema kuwa kosa ni kuuza kazi za wasanii bila ya kibali ila kweli kwa kipindi kile tulikuwa tunachoma nyimbo za wasanii bila ya kuwa na kibali cha kazi ile, aliponikamata alibeba Computer na tukaendelea kukusanywa wengine hadi tukajaa kwa idadi aliyoona n sawa kwake hadi kituo cha polisi UTEGI.
Wakati anakamata alikuwa na Dada mmoja hivi ameshiriki kwenye Filamu ya CHOZI LANGU (jina limenitoka) tulipofika pale kituoni ulikuwa unaitwa mmoja mmoja na kuanza kuulizwa una shilingi ngapi ili uachiliwe huru baada ya kutoa pesa ulikuwa ukikabidhiwa Computer na Askari na unarudi katika eneo lako.
Mazingira yale yalikuwa si mazingira ya kunufaisha wasanii wala kwa ajili ya BASATA bali ni sehemu ya kula ya mjanja mmoja na wenzake, kwa kujiita Mwenyekiti wa wasanii Nchini (sijui wasanii gani hao).
Sasa leo katembelea tena maeneo yake na kivuli kile kile cha UBASATA NA UWENYEKITI WAKE na kuanza kutishia wenye vibanda kwa kuwaambia kuwa kama Jumatatu hawatakuwa na vibali vya kazi basi atawakamata kitu ambacho naona ni uonevu sana hasa kuna wengine wana leseni ya biashara hizo ila anawaambia kufikia Jumatatu wawe na vibali vya kazi za sanaa na kama huna unaandaa laki mbili na nusu kwa ajili ya kupewa kibali na yeye ndiye mtoaji.
Najua kazi hizi jamii nyingi hazijui utaratibu wa kuzifanya ila BASATA na Wasanii naombeni mgutuke kuna mtu anakula ile hali mmelala kwa kivuli chenu hizi pesa anazokusanya huko vijijini kuna msanii aliwahi kupewa kama sehemu ya faini kwa wale wanaofanya biashara hii ya uuzaji wa kazi za wasanii? Mbaya zaidi akiona tu Computer anajua ni biashara ya uuzaji wa kazi za wasanii zinafanyika.
Naombeni BASATA hasa kwenye mikoa hii ambayo haijajua utaratibu wa kufanya shughuli hizi mtoe elimu na namna ya kuweza kuhakikisha kuwa wanajisajili chini yenu na si chini ya mtu mmoja mwenye masilahi yake na familia yake (Aliwahi kuchukua pikipiki Mwanza na kuondoka nayo kama Faini na ikawa yake)
Pia wasanii mjur kuna wasanii wanaokula jasho lenu bila nyie wenyewe kujua yaani (Meno yenu wenyewe yanaumana).
Asante sana wote watakaoshiriki kwenye uzi huu.