Barua ya Waziri January Makamba kwa Askofu mkuu wa KKKT

AbasMzeEgyptian

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
407
312
Askofu Dkt. Frederick Shoo,
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania,
S. L. P 3033
Arusha

YAH: PONGEZI KWA KUCHAGULIWA KUWA ASKOFU MKUU WA KKKT

Baba Askofu, ninaandika kukupongeza kwa kuchaguliwa kuwa Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania katika kikao cha 19 cha Kanisa jijini Arusha. Kuchaguliwa kwako ni kielelezo cha imani na upendo mkubwa walionao waumini wa KKKT juu yako na, zaidi kiashiria kwamba Mwenyezi Mungu amekuteua kati ya wengi, kuwa mlezi wa kiroho atakayeliongoza Taifa lake katika njia impendezayo yeye, kwa ajili ya sifa na utukufu wake.

Binafsi nina imani kubwa na wewe kama kiongozi na kama mchungaji na naungana na waumini wa KKKT na Watanzania wote kukuombea heri na baraka za Mwenyezi Mungu katika kazi yako hii mpya, kubwa na njema. Ninafarijika zaidi kutokana na kwamba, kwa maudhui ya mahubiri yako siku zote, nchi yetu imepata sauti ya ziada ya ulezi wa taifa, hasa katika zama hizi zenye changamoto na majaribu mengi kwa taifa letu. Sisi tulio katika uongozi wa siasa tunategemea busara zako, ushauri wako na sala zako katika kuliongoza taifa hili.

Mimi, mke wangu na familia yetu tunakuombea kwa Mungu kwamba upendo wake ukufunike na kukutunza. Naelewa kwamba kazi ya kuliongoza Kanisa la Mungu ina changamoto zake lakini naamini kabisa kwamba utaiweza kwa nguvu za Mungu kama vile waraka wa Mtakatifu Paulo kwa Wafilipi unavyotuambia “naweza kuyafanya mambo yote katika yeye anitiaye nguvu”. Hatuna shaka kabisa kwamba, chini ya uongozi wako, Kanisa la Mungu litasimama imara.

Ninakuhakikishia ushirikiano wangu binafsi na wa Serikali ambayo mimi ni sehemu yake kwa kuwa Serikali na Kanisa ni wadau katika maendeleo ya binadamu.

Mwanao,


January Makamba (MB),
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)

1.jpg


Mke wa Rais Janeth Magufuli akimjulia hali Sheikh Mkuu wa Tanzania Muhimbili.
 
Imekaa vizuri

Huyu dogo kwenye ku-type yuko poa sana. Nadhani Jk hakukosea kipindi kile kumteua kuwa mwandishi wa hotuba zake. Hapa nimemkubali kwa kuusema ule ukweli.

Kwa hakika safari ya 2025 anaichakata vilivyo

BACK TANGANYIKA
 
Naona mjadala tofauti na content ya barua yake,sioni maneno yanayopaswa kujadiliwa kwa mfumo huu,ama ni hisia tu.
 
Safi mh. January. Hutaacha kuzichota hizo baraka ulizoziomba maana ukimheshim mtumishi wa Mungu nae Mungu anakuheshimu.
 
Kwani January kuwa Rais wa nchi 2025 kunatatizo lipi,nadhani chuki binafsi sana zenu,wewe ni mmoja au wawili watakaopiga kura kumkataa sio wote,haki kuwa na malengo Fulani katika maisha
 
w
Acheni ubaguzi wenu wa kidini, nitawaunga mkono kama mtamchambua kwa uwezo wake wa kuongoza na sio dini yake.

Yaani bado kuna watu karne hii ya 21 wanaongelea udini, ukabila, ubaguzi wa rangi!! Allah awarehemu kwa kweli.
Wajinga hao wanaojadili mambo ya udini
 
Utapongeza sana lkn huyo asahau urais
CCM ina hazina ya vichwa, kumbuka walijitokeza watu zaidi ya 40 na yote yalikuwa majembe ya ukweli. Huwezi kulinganisha ni jinsi ambavyo Chadema inapata taabu hata kumpata mtu sahihi wa kumrithi Dr Slaa.
 
Hatokaa aupate urais huyo
labda urais wa band ya muziki level za kina diamond.
Acheni ubaguzi wenu wa kidini, nitawaunga mkono kama mtamchambua kwa uwezo wake wa kuongoza na sio dini yake.

Yaani bado kuna watu karne hii ya 21 wanaongelea udini, ukabila, ubaguzi wa rangi!! Allah awarehemu kwa kweli.
hyo rais wa ukoo wenu bwana marope ni bure kabisa.
 
Back
Top Bottom