Kijukuu03
Member
- Aug 24, 2018
- 19
- 32
Hii nimeikua sehemu ikabidi niilete hapa;
“Habari yako bwana HASSAN
Natumaini hatufahamiani, mimi naitwa Mr JOHN au Baba Hellen, mke wangu ni ANITA ambaye kwa sasa ndio baby wako kipenziiii kwa maelezo niliyoyakuta kwenye simu yake.
Leo nakutumia SMS hii sio kwa ubaya bali kwa kukupongeza kwa kumbadilisha sana mke wangu, kitu ambacho hata Mapadri na wazazi wake walikishindwa. Kiukweli Anita wangu sasa hivi kabadilika sana, hanywi tena pombe kupitiliza kama hapo mwanzo, hafokei hovyo watoto na kuwapiga kama mwanzo, harudi nyumbani usiku tena, sasa hivi Anita ananipikia na kunifulia. Nimeshangaa sana, haya mambo niliyasahau muda kutoka kwa mke wangu mpendwa.
Tatizo lilikuwa ni mimi mwenyewe baada tu ya kunifumania na mwanamke mwengine ndipo mke wangu alibadilika sana mpaka nilijuta, kila jitihada zilishindikana za kumrudisha awe kama zamani, ikawa inapotokea nashindwa kutimiza haja zake za kimwili kama zamani basi ni ugomvi, inaonekana kama nimemalizia nguvu huko nje.
Mabadiliko ya hivi karibuni ndio kitu ambacho kimenishangaza, mke wangu amekuwa na furaha kama mwanzo, amekuwa mcheshi kwa watoto, anapika na kufua.
Lakini nimegundua sababu kubwa ya mabadiliko haya ni wewe HASSAN, tokea akupate uwe mchepuko wake amekuwa akikuheshimu sana, amekuwa akikusikiliza sana, nimekuta SMS zako nyingi ukimuuliza mke wangu
Anita umepikia watoto?
Anita umemuandalia chakula mumeo?
Anita uko wapi saa hizi muda wa kurudi mumeo, rudi kwako haraka.
Nimefurahi sana kwani naye amekuwa akitii maagizo yako kuliko yangu.
KWELI MCHEPUKO MPYA UNA NGUVU KULIKO MUME.
Nimefurahi zaidi kwakuwa hunywi pombe kulingana na imani yako, na hivyo hata yeye umemkataza kunywa pombe na ameacha kabisa, hata nilizonunua mimi ili anywe ziko tu kwenye friji, hataki kabisa kwakuwa anakuogopa.
Wewe ni miongoni mwa wanaume wachache sana ambao hutembea na mke wa mtu na bado akahitaji asiharibu ndoa yake. Yaani wewe kutembea na mke wangu kumeimarisha sana ndoa yangu.
Hata unapomuudhi wewe huwa najua, maana atashinda hana raha kabisa.
Ahsante sana HASSAN, ila ninachokuomba mwambie na mie asinisahau sana kwenye tendo la ndoa
maana mkiahidiana kukutana wiki ijayo ujue wiki nzima sipewi anakutunziaa 🤣🤣

Naomba umwambie hilo, mimi ni mtu mzima nahitaji kulea wanangu kwa amani zaidi. Pengine nguvu zangu za sasa siwezi mtimizia mahitaji yake ya kimwili.
Bora adui mmoja ninayekujua kuliko akiwa anahangaika ovyo kutafuta kukidhi haja ya mwili wake.
SIKU NJEMA MR HASSAN.
usimwambie Anita kama nimekujua maana atachukia sana na anaweza kununa mwezi mzima.
TUMPENDE MKE WETU.
WAKO MR JOHN.”
Sent using Jamii Forums mobile app