monjozee
Senior Member
- Sep 19, 2016
- 115
- 297
BARUA YA WAZI KWENDA KWA MH.JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI,RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Imeandikwa na; Joseph Monia Politician
Rais Magufuli salaam!!
Leo nimelikumbuka zoezi uliloasisi na kuliendesha kwa usaidizi wa watumishi wa serikali waliopo chini yako. Zoezi hilo uliliita "KUWAONDOA WATUMISHI HEWA".
Nakumbuka kwa maelezo yako mwenyewe, uliwagawa watumishi hewa katika makundi mawili;
1. Watumishi wote waliokuwa wamefoji vyeti na kutumia majina yasiyo halali kwao serikalini.
2. Watumishi wote wanaopokea mishahara ilihali wakiwa wamestaafu ama kuacha kazi na wengine wakiwa wameshafariki,lakini bado wanahesabika kwenye payroll ya serikali.
Zoezi hili lilipelekea watumishi takribani 1855 (kwa mujibu wa tovuti ya TAMISEMI) kupoteza kazi.
Binafsi napenda kusimamia kwenye category namba moja ya aina ya watumishi hewa kwa maana ya "wafoji vyeti".
Falsafa yako Mh.Rais ni "MSEMA KWELI NI MPENZI WA MUNGU" kwa lugha nyepesi ni kuwa hutaki kuficha maovu.
Mteule wako yaani RC Dar es Salaam, anasemekana kufoji vyeti katika safari yake ya Elimu. Huyu PAUL MAKONDA, inasemekana kuwa hilo siyo jina lake halisi, bali jina halali ni DAUDI ALBERT BASHITE.
Mh.Rais huyu akiwa kama mteule wako, mbona umeamua kulinyamazia hili??
Hii ndiyo falsafa yako uliyokuwa ukiimba kila siku?.
Makonda kama hili ni la kweli atakuwa hana utofauti wowote na wale watumishi uliowaita "HEWA" wakiwa1855.
Makonda kama hili ni la kweli atakuwa anazo sifa zote za kuungana na wanafunzi wale wa Dodoma 7805 uliowafukuza pale chuoni na kuwaita "VILAZA".
Rais Magufuli, fanya maamuzi juu ya hili kabla Watanzania hawajakuhusiha nalo, kwa maana ya kufunika kombe mwanaharamu apite.
Kwenye suala hili kuna njia mbili pekee;
1. Kumuagiza Makonda athibitishe ama akanushe taarifa hizi (kwa documents,yaani vyeti),kama alivyofanya Waziri wako wa Mambo ya ndani wa sasa Mh.Mwigulu Nchemba, pale Elimu yake ilivyoleta utata kama ilivyo kwa Makonda hivi sasa.
2. Kumuondoa kutoka katika nafasi aliyopo kwa vigezo vilevile vya watumishi weha wengine.
Na kwa kufanya hivyo Mh.Rais utatufanya sisi kama Wananchi kuiishi na kuifuata falsafa yako.
MWISHO; Naamini ujumbe wangu umekufikia na utaufanyia kazi.
Kulikalia kimya suala hili suluhisho la kisomi.
#Makonda_hakiki_Elimu_yako
#Ndalichako_hakiki_Elimu_ya_Makonda