Rutorial k
JF-Expert Member
- Jun 8, 2014
- 951
- 843
Ni matumaini yangu kuwa hamjambo nyote na munaendelea na ujenzi wa taifa letu.nami nitumie jukwaa hili kumuandikia waziri wa katiba na sheria mh. Mwakyembe barua ya wazi kuhusiana na mwenendo wa uendeshwaji wa vyesi katika mahakama zetu za T anzania nikiwa na mfano hai wa kesi ya ndoa no 31/2001 kati ya Joyce John dhidi ya Maguzu Masanja.
Mh. Waziri kesi hii ilifunguliwa na Joyce John dhidi ya Maguzu Masanja mnamo mwaka 2001 katika Mahakama ya mwanzo ya Ilemela jijini mwanza. Joyce alikuwa na madai mawili, 1 aliomba mahakama hiyo kuvunja ndoa baina yake na maguzu kwa sababu ya mgogoro mkubwa uliokuwa katika ndoa hiyo, 2 joyce aliomba mahakama hiyo kugawanya mali ambazo walikuwa wamechuma kwa muda waliokuwa pamoja.
Kesi hii ilihukumiwa mwezi juni mwaka 2001 ambapo mahakama ilikubaliana na maombi ya joyce na kwamba ndoa yao ilivunjwa na mgawanyo wa mali ukawa kama ifatavyo; Maguzu alipewa nyumba mbilili kati ya nyumba tatu na vtu vingine, joyce alipewa nyumba 1 kati ya tatu na vitu vingine.
Mh. Waziri, utekelezaji wa hukumu hii ulifanyika trh 10 august 2001 na mali zote zilikabidhiwa kwa joyce kama ilivyokuwa imeamriwa na mahakama ya mwanzo, cha kushangaza ni kuwa trh 3 October 2001 maguzu alipeleka barua kwa afisa mtendaji kutoka katika ofisi ya wilaya iliyomtaka kurejesha mali zote alizomkabidhi joyce kwa maguzu, swala ambalo mtendaji alilitekeleza kwa kurejesha mali zote kwa maguzu kwani maguzu alikuwa amekata rufaa katika mahakama ya wilaya jijini mwanza. Swali la kujiuliza hapa je, ni muda gani ambao mtu anastahili kukata rufaa baada ya hukumu? Kama ni siku 30 je iweje maguzu akubaliwe kukata rufaa wakati muda wa kufanya hivyo ulikua umepita zaidi ya miezi mitatu?
Mh.waziri mahakama ya wilaya ilisikiliza rufaa ile na kutoa maamuzi mwaka 2oo2 ambapo maguzu alishinda kesi ile. Joyce hakupewa kitu chochote hivyo joyce alikata rufaa katika mahakama kuu ya mwanza ambapo mwaka 2003 mahakama kuu aliamuru joyce apewe mali zake kama ilivyoamuliwa na mahakama ya mwanzo.mh. waziri cha kushangaza ni kwamba tangia hukumu hiyo itolewe mwaka 2003 hakuna utekelezaji wowote uliofanyika hadi hivi sasa. Masikitiko yangu ni kwamba kama hukumu haziwezi kutekelezwa kwa nini zinatolewa na mahakama tena mahakama kuu!
Mh. Waziri, kutotekelezwa kwa hukumu hiyo kumechangiwa na watenaji wa serikali ambao kwa nyakati tofauti waliwandikia watendaji wa chini yao kutofanya utekelezaji wa hukumu hiyo. baadhi ya watendaji waliozuia utekelezaji wa swala hili ni pamoja na ; katibu tawala wa wilaya ya ilemela ndg p. Ruhazigwa ambae alimuandikia barua mtendaji wa kata wa nyamanoro kuacha kutekeleza swala hilo, barua hiyo iliandikwa trh 7november 2008. Wa pili ni hakimu mkazi mfawizi wa mkoa a mwanza ndg E.G Rujwahuka ambae alimuandikia barua court broker kusitisha ukamatwaji wa mali alizotakiwa kukabidhiwa joyce .barua hiyo iliandikwa trh 17 September2009. Watatu ni ndg maguzu mwenyewe ambae amekuwa akitumia nguvu kubwa kuzuia utekelezwaji wa hukumu hii tena anatumia siraha kuwadhiti waliojaribu kutekeleza swala hili ukizingatia mtuhumiwa ni mwanajeshi hivyo anatumia nafasi yake vibaya.
Mh.waziri , alichofanyiwa huyu mama, joyce john sio haki kabisa kwani ukiona vielelezo vya kesi hii unaweaza kububujikwa na machozi kwa njisi wanyonge wanavyonyanyasika katikaka vyombo vya kutoa maamuzi katika wizara yako. Niwazi kuwa “ justice delayed is justice denied” kwa mda wote huu mama huyu amepoteza haki yake ya msingi. Kibaya zaidi ilifika wakati ambapo mama huyu aliugua akakosa pesa ya kumpeleka hospitali na mwaka jana mama huyu ALIPOTEZA MAISHA.
Mh, ombi langu kwako ni kuwa pamoja na mama huyu kufariki dunia bado kuna haja ya watu wote waliohusika na ucheleweshwaji wa kutekeleza hukumu hii wachunguzwe ili kubaini uhalali wa kuzuia utekelezwaji wa hukumu hii.hili litasaidia kuboresha utendaji kazi wa vyombo vya kutoa maamuzi na kuwasaidia wanyonge wengine ambao wako hatarini kupoteza haki zao pamoja na mzaisha yao kama ilivyokua kwa joyce john.Niko tayari kutoa ushirikiano kama nitahitajika kufanya hivyo.
Kwa mawasiliano ;0673503558.
kibungi maige
mwanza