Suala la Elimu sio la kupigana kiswahili, midahalo mbali mbali inahitajika kujua jinsi ya kutatua changamoto hizi. Changamoto zilizokuwa zinatatuliwa miaka 10 nyuma kwa njia flani, njia hiyo inaweza ikawa ina mchango mdogo sana wa kutukwamua tulipo kwa maana mazingira na teknolojia vimebadilika na vinasogea kwa kasi sana.
Mfano miaka ya 99 mpaka 2003 kulianza mchepuo wa masomo ya kompyuta katika baadhi ya shule hapa nchini, je mchepuo huo bado upo? Je tumejipanga vipi kuwafundisha watoto msingi wa elimu ya kujisomea, kuwa wagunduzi na wavumbuzi??
Je kuna model za kutosha kumfanya mwanafunzi aelewe somo na si kukariri somo?
Je motisha kwa walimu imekaaje??
Mazingira ya ufundishaji yako vipi?? Utayari wa mwanafunzi kufundishika na kuipenda elimu uko vipi?? Tukizembea hili kila mtu akajiangalia mwenyewe tutakuwa tuna vihiyo wengi nchini na itatuchukua miaka mingi sana kuendelea.
Hii ni nchi yetu na hakuna mtu atakayetoka nje ya hapa kuja kuendeleza elimu yetu pasipo sisi kufunguka na kuweka mifumo yetu sawa.