Barua ya wazi kwa Waziri wa Elimu na wadau kwa ujumla

Munkari

JF-Expert Member
Feb 9, 2013
8,084
4,351
Binafsi nakupa pongezi nyingi sana waziri wa elimu "Prof Joyce Ndalichako"kwa kutumbua hili jipu linaloitwa "GPA"
kwakweli hili lilikuwa jipu lisiloiva kwa Walimu,watoto wetu(kizazi kijacho,)na Taifa kwa ujumla sababu mfumo huu haukuwa na uhalisia wa ufaulu kabisaa kwa wanafunzi ukilinganisha na mfumo wa "DIVISION" japo bado kuna kaupungufu kidogo kwenye upangaji wa alama but atleast umeondoa hizo B+ na E ambazo hazikuwa na mantiki yoyote kwenye level hii ya elimu.It was not fair at all.

Hongera sana kwa hilo Mama!! Hapa sasa ndio Elimu ilipo na siyo GPA ambayo ilikuwa ikibeba wanafunzi mwisho wa siku tunazalisha kizazi kisicho na kiwango!! Hongera kwa hilo.

Lakini pamoja na pongezi hizo,ningependa kuongelea kidogo changamoto chache zinazotokana na hii kitu "ELIMU BURE"

Tunamshukuru Mh Rais kwa kuwa amewaondolea mizigo wazazi juu ya swala zima la Michango mashuleni,Lakini kwa upande wa pili kuna changamoto nyingi sana mashuleni mfano ongezeko la idadi ya wanafunzi linalopelekea ukosefu wa vyumba vya kusomea(madarasa),madawati n.k.Changamoto kubwa kuliko yote niliyoiona ni hii ya KUWAONDOA walimu wakujitolea esp.kwa shule za Sekondari kwa kigezo cha kuwa "serikali haina pesa za kuwalipa" Is that true???!! kwa ELIMU?anyway...

Jamani tukumbuke kuwa kuna shule za vijijini ambazo ndiko kwenye uhaba mkubwa wa waalimu ukilinganisha na shule za mijini.Hawa waalimu wa kujitolea wamekuwa msaada mkubwa sana katika hizi shule pamoja na mishahara midogo waliyokuwa wakipata.Madhara yaliyopo sasa ni shule kukosa walimu pamoja na Ukosefu wa ajira kwa hao waalimu ambao wamerudi mtaani pamoja na uwezo wao mzuri wa kufundisha.Kuwa mujibu wa maagizo ni kwamba "somo kama halina mwalimu liachwe wazi lisifundishwe"hakuna fungu la kuwalipa . Tujiulize kwa mtindo huu Tutafika?na vipi sera ya Ajira?hamuoni kama hamjawatendea haki hao waalimu?okey ..!

Ombi langu :Hakikisheni mnatatua changamoto hizi haraka iwezekanavyo kama kuajiri walimu wa kutosha mashuleni,bila kufanya hivyo basi tutegemee ufaulu mdogo sana mwakani(2017)kwa shule za umma kutokana na wingi wa wanafunzi (Both primary and Secondary )

Mbali na hilo Elimu ya shule ya msingi itazamwe upya mfano mitihani ya darasa la saba esp Hisabati,hivi kweli unaweza kumpima mtoto kuhesabu kwa maswali ya kuchagua??!!Why?Then??! No way!
hii siyo sahihi.

Sambamba na hilo watoto wengi nowdays wanaingia kidato cha kwanza hawajui kuandika wala kusoma,unajiuliza mtoto huyu kapitaje darasa la saba?? and what next for this child??!! mmh!!
Tunapoteza maana nzima ya "elimu msingi "na kuharibu kizazi chetu wenyewe !Lipewe mkazo!!!!

kwakweli i have many things to speak out,let me end here!

it's my hope you(mentioned)will workout with.
Sorry for so long article!!

otherwise ,Next time.....!!!!

Munkari (Junior ed. stakeholder)
 
Kitu bado ni kilekile. Kuboresha zaidi kwa O'level "A" irudi palepale >=81.
Siyo >=75 ya sasa.
 
Kitu bado ni kilekile. Kuboresha zaidi kwa O'level "A" irudi palepale >=81.
Siyo >=75 ya sasa.

yah ni kweli ilitakiwa arudishe mfumo mzima na si robo! but atleast ! hizo B+ sijui E zilibeba sana wanafunzi afu unaambiwa "ufaulu umeongezeka" aisee!!
 
Hivi bado vitabu vya Shigongo vinatumika badala ya vya Shaaban Robert?
na vya yule mbunge wa mara pia?
 
Mtafutie mwanao shule nzuri asome.
Hapa mtaani ninaisha na walimu wengi, asilimia 99 ya walimu hao na mshahara wao mdogo watoto wao wako medium academies schools. JIULIZE WHY? Hawapeleki wanao shule hzo.
Wewe endelea kutuma barua kwa Waziri.
 
mmhhh! baasi sawa!

lakini kuna watanzania wenzio hata hiyo "medium academies "hawajui maana yake unawasaidiaje???!!!
 
Suala la Elimu sio la kupigana kiswahili, midahalo mbali mbali inahitajika kujua jinsi ya kutatua changamoto hizi. Changamoto zilizokuwa zinatatuliwa miaka 10 nyuma kwa njia flani, njia hiyo inaweza ikawa ina mchango mdogo sana wa kutukwamua tulipo kwa maana mazingira na teknolojia vimebadilika na vinasogea kwa kasi sana.
Mfano miaka ya 99 mpaka 2003 kulianza mchepuo wa masomo ya kompyuta katika baadhi ya shule hapa nchini, je mchepuo huo bado upo? Je tumejipanga vipi kuwafundisha watoto msingi wa elimu ya kujisomea, kuwa wagunduzi na wavumbuzi??
Je kuna model za kutosha kumfanya mwanafunzi aelewe somo na si kukariri somo?
Je motisha kwa walimu imekaaje??
Mazingira ya ufundishaji yako vipi?? Utayari wa mwanafunzi kufundishika na kuipenda elimu uko vipi?? Tukizembea hili kila mtu akajiangalia mwenyewe tutakuwa tuna vihiyo wengi nchini na itatuchukua miaka mingi sana kuendelea.
Hii ni nchi yetu na hakuna mtu atakayetoka nje ya hapa kuja kuendeleza elimu yetu pasipo sisi kufunguka na kuweka mifumo yetu sawa.
 
Nitajieni mwanasiasa mmoja tu ambae mwanae anasoma shule ya kata.
 
you are absolutely right!!

there are so many obstacles that must be solved for our education to develop!

mi jicho langu kuu lipo kwa hawa wasio na uwezo wa kupeleka watoto wao shule zinazoitwa "nzuri "au "bora"
serikali inasafari ndefu sana juu ya hili kuikomboa nchi kielimu!

if i were me
ningeanza kuboresha mazingira kwanza ya kusoma like madarasa ya kutosha,distribution of many teachers e.t.c then elimu bure ingekuja badaye!
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom