BARUA YA WAZI KWA RAISI

BARUA YA WAZI KWA RAISI

ANDREW JOSEPH

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2017
Posts
422
Reaction score
405
Mheshimiwa raisi pole na majukumu yako ya kuongoza nchi ila acha niongee haya madogo niliyoyaona.

Jana tarehe 24-02-2018 kuna mkutano wa hadhara ulifanywa na waziri wa ardhi mheshimiwa Lukuvi ktk harmashauli ya Kahama nilichokiona hapo ndio kinanifanya kuandika hapa

Kwanza nampongeza Lukuvi alivyojitoa kuhudumia wananchi hao wanyonge kuanzia asubuhi mpaka usiku japo tanesco walijatahidi kumhujumu lakini aliwasha tochi na kuendelea kutoa huduma

Mheshimiwa raisi kwa mazingira niliyoona jana wakurugenzi pamoja na wataalamu wa ardhi ni tatizo kubwa kwenye hii nchi ukiona waziri anafanya kazi mpaka usiku ujue kuna jambo

Adhma ya serikali ya kuhudumia wananchi itaendelea kukwama kama tutaendelea kuwafumbia macho wakulugenzi wahuni kama huyu wa halmashauri ya mji Kahama

Jana waziri kapokea malalamiko yasiyopungua 700 nayote ni matokeo ya uhuni unaofanywa na mkurugenzi pamoja na wataalamu wake wa ardhi

Mheshimiwa raisi mengi waziri ameyaona lakini hatujatibu ugonjwa kwa sababu waliosababisha wapo kwenye nafasi zao na kesho waziri anaondoka na hatujui kama maelekezo yake yatafanyiwa kazi

Mheshimiwa raisi kuna haja kupitia upya utendaji wawatumishi wako unaowateuwa maana hao ndio wanachangi kukugombanisha wewe na wananchi wako

Mwisho pongezi kwake waziri wa ardhi maana anaonekana kuwa dira ya wanyonge waliodhulumiwa haki zao kwa muda mrefu na kwa haki hii tunaanza kuona mwisho wa migogolo ya muda mrefu ambayo wakati mwingine ilighalimu maisha ya watu ..

WAKO MWANANCHI WAKAWAIDA
 
Hakuna mkamilifu, kikubwa ni kujirekebisha tuu ndo dawa labda Kama mkurugenzi ni malaika hapo sawa atamridhisha kila mtu
 
Back
Top Bottom