Barua ya wazi kwa Rais na wasaidizi wake

SHANGWEH2011

New Member
Jan 20, 2018
2
6
BARUA YA WAZI KWA MH. RAISI KUTOKA KIGOMA

Nianze kwa kukupongeza mh.Rais kwa kuendelea kuliongoza taifa kwa UZALENDO na UADILIFU MKUBWA. Kazi yako huko ni nzuri isiyo na kifani kiukweli kila mwenye akili timamu anatamani uendelee kuliongoza taifa kwa mfumo huu maana huenda tukapiga hatua kubwa.

Mh Raisi pamoja na kazi nzuri unayoifanya athari ya kazi yako haiko sawa katika hii mikoa ya pembezoni sawa na mikoa ya karibu yako yaani unayoelekeza huko hayafanyiiwi kazi ipasavyo mfano

UPUNGUFU WA MADAWATI mh raisi huku kwetu hali si shwari huenda unapewa taarifa kuwa kila shule ina madawati ya kutosha na hakuna wanafunzi wanaokaa chini lakini hili si kweli. Ni baadhi ya halmashauri tu kv.manispaa ya kigoma ujiji na kasulu wametekeleza lakini kwa halmashauri zingine hali si yenyewe mfano halmashauri ya kigoma tuma watu wako waende shule ya MSINGI KIYENGA, MGOGO, KIZENGA na RUSIMBI bado watoto wanakaa chini na kibaya zaidi darasa la TATU NA LA NNE wanasomea CHUMBA KIMOJA kibovu kilichojengwa na wananchi na kwa sasa kimetobolewa sana na mbuzi na kondoo. Tunaomba mh uendelee kuhamasisha na kuagiza watendaji chini yako hata huku pembezoni ili tupate elimu bora sawa na watanzania wengine.

UTENDAJI MBOVU WA HALMASHAURI, mh raisi huku kwetu watendaji wako wako zaidi kimigogoro zaidi si kikazi hali ambayo imepelekea wao kutofanya kazi. Watu wako uliowateua wanatishiana nafasi zao na kuona hakuna aliye mkubwa zaidi ya mwenzake kwa sababu wote wameteuliwa na mtu mmoja. Mfano MKURUGENZI WA KIGOMADC NA MKUU WA WILAYA hawana maelewano hata kidogo hadi mkurugenzi kushindwa kutekeleza maagizo ya mkuu wa wilaya, mkurugenzi na madiwani na wakuu wa idara kigomA dc imepeleka kuathiri kupanga mipango ya kimaendeleo kwa sababu mvutano ni mkubwa sana .mh raisi sisi tunaoishi hapa hatuelewi tunafanyaje kwa sababu hata wanafunzi wetu waliofaulu kwa kiasi hawana maeneo ya kusomea ni zaidi ya wanafunzi 1000 hawajui hatima yao kwenye halimashauri ya kigoma na buhigwe mf kata ya muhinda buhigwe na kigoma dc wanafunzi waliobakia ni wengi sana. Ombi langu mh raisi itoe kauli yako tutoke hapa tulipo kwa kutoa maelekezo au kwa wateule wako kuwabadiishia vituo au uonavyo inafaa.

KUTOTEKELEZWA KWA SERA YA ELIMU BURE, mh raisi huku kwetu sera ya elimu bure ni kama haiwezekani kwa sababu michAngo ni lazima iwe mingi kwa sababu ya upungufu wa walimu na vyumba vya madarasa, watumishi wengi wakija mikoa hii ya pembeni wanaita ni mikoa a kuanzia kazi na muda kidogo hutafuta uhamisho na kuondoka na wengine hawafiki kabisa. Mh raisi shule zako nyingi za msingi zinawalimu wawili hadi wanne kwa wanafunzi 700 hadi 800. Hali hii imepelekea walimu waliopo kuomba msaada kwa wazazi maana halmashauri haziwasaidii kwa kuajiri walimu wa kujitolea mfano S/M KITERAMA,MGOGO ,AMANI RUSIMBI na KIGALYE kigoma dc hakuna shule yenye zaidi ya walimu 4 ila wanafunzi wake ni kuanzia 700 hadi 800 ila kuna shule mh zina walimu zaidi ya 20 zile zilizoko pembezoni mwa mji na mrundikno huu unatokana na TOA KITU PATA KITUO KIZURI kwa baadhi ya wakuu wa idara.

Pia sera ya elimu bure inashindikana kutkana na ukosefu wa vyumba vya madarasa. Wazazi wanachangia sana ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa lazima kwa sababu hakuna fedha inayokuja kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika maeneo yetu hali inayosababisha tujenge wenyewe, sasa usipochangia michango hii utachukuliwa hatua kali na watendaji ikiwa ni pamoja na kukufunga na kukuondoa kwa dhamana ya fedha taslimu.

Ombi mh raisi naomba ulione suala la walimu, madarasa na maabara kwenye mikoa a pembezoni kama suala maalumu ili usumbufu huu umalizike kukataza kwako tu bila kuchukua hatua za kumaliza tatizo hakutatusaidia sisi wanyonge sisi huku wnafunzi wanasomea hadi MSIKITINI nenda kata ya ZIWANI kigoma dc utayaona haya.
USIMAMIZI WA MIRADI NI MBOVU SANA KIASI CHA MIRADI MINGI YA SERIKALI KUWA CHINI YA KIWANGO mfano miradi ya maji KIGOMA MJINI, NYARUBANDA, NKUNGWE, MUBANGA HAITOI MAJI IPASAVYO LICHA YA PESA NYINGI ZA SERIKALI KUTOLEWA NA KUTUMIKA

RUSHWA BARABARANI ni kubwa sana si sawa na kauli yako, yaani polisi wa barabarani ni bonge la dili wananchi wanatozwa rushwa sana kwa sababu ya kutojua haki zao. Kwa sababu barabarani kuna maslahi kila polisi anatamani kuhamia barabarani ukianzia mwandiga hadi manyovu km56 kuna maeneo ya vizuizi vya polisi 8 mh raisi huenda ukawa unaambiwa ati wanaimarisha usalama ila wanatafuta pesa tu

UMEME VIJIJINI mh raisi sera yako ya umeme ni nzuri lakini huku kwetu malalamiko ni makubwa sana hii inatokana na shirika na umeme kuandaa mazingira ya kutapeli wananchi. Katika maeneo mengi watu wametapeliwa na wakandarasi wa umeme (SYBA ) ambao walikuwa na ubia na shirika la umeme(maana kiongozi wao ni mfanyakazi wa tanesco BENJAMINI GASOMI) ambao walikuja mapema wakati rea inaanza kisha wakaanza kutambua watu wanaohitaji umeme baada ya kuwapata walikuwa wanafanya tathmini ya gharama ya vifaa vinavyohitajika na kukuagiza ulipe baadae ilionekana kwamba watu hawa si watu wa tanesco. Shida inayokuja hadi tunaamini kuwa wana uhusiano ni kwamba pale kampuni ilipoweka alama hata tanesco ndipo walipoweka nguzo zao. Mfano KITUO CHA KULEA WATOTO YATIMA MATYAZO KIMETAPELIWA ZAIDI YA MILIONI THELATHINI NA NANE , wananchi ni zaidi ya 4000 wameibiwa Na wametapeliwa tanesko ukiwauliza wanakwambia aliyetapeli wao walishamfukuza kazi

Pia mh raisi waliopata umeme ni watu wachahche sana yaani umeme umepita barabara kuu na mtaa mmoja nyuma ya barabara kuu kama hauko barabarani sahau kupata umeme. Mh raisi sote hatuwezi kuwa barabarani tunaomba hata sisi tulio katka mitaa tupate huduma maana ukienda mikoa ya wenzetu miradi ya rea ina tofauti sana kiusaMBAZAJI sijui kwetu kulitokea nn hadi ikawa hivi. Mwisho kwenye suala hili la umeme mh raisi ni UKATAJI OVYO wa umeme sisi huku WANAKATA WATAKAVYO hakuna cha taarifa wala tangazo pindi wanapotaka kukata umeme na umeme unakatika kila siku mh raisi naomba usichoke kuendelea kutoa maelekezo ya walioko chini yako.

Mh RAISI nina imani nimeandika sana na nimekuchosha sana huenda nimekosea pia niombe unisamehe bure lakini nimeelezea kile ninachokiona. Nakutakia kazi njema

Raia mwema

kigoma
 
Zito kabwe ni mbunge wa kigoma kutwa anapiga porojo zisizohusu jimbo lake wakati kuna changamoto kibao.Halmashari kigoma iko chini ya ACT wazalendo lakini watoto wanakaa chini Zitto kabwe anazurura dar es salaam haongelei matatizo ya jimbo lake unakuta kakalia kuongelea vitu visivyo na kichwa wala miguu.Zitto kabwe nahalmashauri yako katutueni hizo kero pesa mwakusanya zingine mwapewa na serikali huwa mnazipeleka wapi?
 
Kwa taarifa yako tu ni kuwa nafasi za uteuzi zishajaa!

Kilaaa kitu lazima mlete siasa,
Hivi wewe huwezi hata siku moja ukaamua kujibu jambo kisomi na kuwa muungwana ???
Hata kama huu ni uhuru wa maoni lakini wewe mwenzangu unakera. Uzandiki, Uzandiki tu, kwanini ???
Mtu anasema kwa kadiri aonavyo, wewe kama msomi unajukumu la kukosa na kurekebisha bila kuleta hizi kashfa.
Grow up bwana..............
 
Zito kabwe ni mbunge wa kigoma kutwa anapiga porojo zisizohusu jimbo lake wakati kuna changamoto kibao.Halmashari kigoma iko chini ya ACT wazalendo lakini watoto wanakaa chini Zitto kabwe anazurura dar es salaam haongelei matatizo ya jimbo lake unakuta kakalia kuongelea vitu visivyo na kichwa wala miguu.Zitto kabwe nahalmashauri yako katutueni hizo kero pesa mwakusanya zingine mwapewa na serikali huwa mnazipeleka wapi?

Hivi ile Katiba ya Warioba ingepita leo hii hawa wabunge wa Tanzania ni lazima wangekuwa na adabu.
 
Common Sense is no longer common,
Its a highest form of thinking to some Individuals!
NB: Nadhani darasa la lugha lilikushinda maana unawaza na kuongea kwa sequence kama kasuku wa muhindi.
Narudia tena Warioba hana na hajawahi kuwa na katiba fullstop!
 
Wewe RAIA mwema wa kigoma. Ni kwa vile hujui ila hayo matatizo yapo kila mahali. Usipumbazwe na zile hotuba kwamba mambo yanaenda sawa.

Hivi unajua huko Mwanza kila mwanafunzi lazima aende na dawati..!! Unafikiri upungufu ni hapo kigoma vijijini tu.. Looh

Hujui huko Butiama wanachangishwa elfu 70, 70 ili kujenga madarasa. Unafikiri ni hapo kigoma tu.

Hivi hujui hapo Dar kuna mabango ya matangazo yule bw. Paul makonda anaomba michango kujenga nyumba za walimu.

Hivi hujui kule Nchemba Dodoma kwa Jumaa Nkamia zahanati kama 20 hazina manesi wala daktari ..yani ni sawa na magodauni.

Hivi hujui huko Njombe mwanafunzi wa shule ya msingi anaandikishwa kwa elfu 20.

Hivi hujui huko Simiyu hawana maji safi ya kunywa.

Hivi hujui kule Lindi na Mtwara Umeme unawaka kwa uhakika kukiwa na ziara za waziri mkuu au rais ..

Hivi hujui hapa Dar na sisi leo tuna natengenezo na hivyo mbezi, nk hakuna Umeme.

Hivi hujui kuna hospital hapa Dar kubwa tu ya Mlonganzila , ni mpya ila haina madaktari na manesi ktk idara kibao..

Unasema aiangalie mikoa ya pembezoni.

Huoni hayo machache niliyotaja kwani unafikiri ni nyie tu..

Hahaa zile hotuba huwa ni kuonesha tu kuwa mambo yapo sawa ila si hivyo.

"Watakwambia tufanye kazi tuache kulia lia".. Hahaa

"Wengine watasema huko kwenu shida ni msaliti zito , kumbe hana usaliti huo"..

Hahaa..

Ni hayo tu
 
Uchochezi huu. Nafikiri hadi muda huu utakuwa umeshikiliwa kituoni kwa uchochezi. Msamiati mpya wa kuwasulubia watanzania.
 
Ni baadhi ya halmashauri tu kv.manispaa ya kigoma ujiji na kasulu wametotekeleza lakini kwa halmashauri zingine hali si yenyewe mfano halmashauri ya kigoma tuma watu wako waende shule ya MSINGI KIYENGA, MGOGO, KIZENGA na RUSIMBI bado watoto wanakaa chini na kibaya zaidi darasa la TATU NA LA NNE wanasomea CHUMBA KIMOJA kibovu kilichojengwa na wananchi na kwa sasa kimetobolewa sana na mbuzi na kondoo. Tunaomba mh uendelee kuhamasisha na kuagiza watendaji chini yako hata huku pembezoni ili tupate elimu bora sawa na watanzania wengine.


Kuna dalili kuwa shule hiyo haina choo, watoto wanakojoa ukutani na ndiyo chanzo cha mbuzi kuchakaza ukuta
 
Back
Top Bottom