Gamba la Nyoka
JF-Expert Member
- May 1, 2007
- 7,022
- 9,292
Kwako mheshimiwa Rais
Shikamoo mheshimiwa Rais, Nianze kwa kukupongeza na kukushukuru kwa kazi nzito sana ya kuipa uongozi nchi yetu. Ninatambua kuwa kazi yako ni ngumu sana na ina lawama nyingi, hata hivyo kama Wahenga walivyosema kwamba chuma cha pua hakiwi chuma cha pua mpaka kipitie katika tanuri la moto basi na mimi ninatambua pasi na chembe ya shaka kwamba juhudi zako na hatua unazochokua ni tanuri ambalo ni kwa nia njema kabisa ya kunyoosha mambo ili baadae tuvune matunda ya Taifa lililonyooka, siyo Taifa la kuishi kiujanja ujanja tu.
Mheshimiwa, Wahenga pia walisema kuwa Kabla ya Pasaka hutanguliwa na Ijumaa kuu, kwa hiyo basi naamini hatua unazochukua leo za kutaka mambo yaliyonyooka zitalisaidia Taifa kwa miaka mingi ijayo.
Mheshimiwa Rais, Nakupongeza kwa dhati kabisa Operesheni ya kutafuta vyeti feki, Mheshimiwa operesheni hii imetuma meseji kali sana kwa watu wote waliofanya udanganyifu wa kitaaluma au waliokuwa wakifikiri kufanya udanganyifu wa kitaaluma, hili Zoezi japo ni chungu na linaumiza lakini LINALIPONYA TAIFA DHIDI YA UDANGANYIFU WA KIELIMU.
Hili ni jambo zuri sana.
Mheshimiwa Rais, tukiacha udanganyifu wa kielimu ambalo ni kosa la Jinai lakini pia tukija katika sheria za Utumishi ni kosa kwa mwajiriwa kupeleka taarifa za Uongo juu yake kwa Mwajiri, Kiufupi Kama wenye vyeti feki watashitakiwa mahakamani wanaweza kupata kifungo cha miaka mingi jela na pia pengine kutakiwa kuilipa serikali pesa nyingi sana kwa kuwa waliingia katika mkataba wa utumishi kwa taarifa za uongo.
Hata hivyo nikushukuru wewe mheshimiwa Raisi kwa huruma uliyowaonesha watumishi hawa, kwa kutoamua kuwashitaki na badala yake ukawataka wajiondoe wenyewe tu, kusema kweli mtu ambaye anajiongeza na alifoji vyeti basi bila shaka ataitikia wito wako mara moja.
Mheshimiwa Rais mimi nilikuwa nina ombi moja tu kwako kuhusu Watumishi hawa waliogundulika kuwa ni wenye vyeti feki na kama utaliona linafaa basi nitakuwa ni mwenye kushukuru kweli kama utalichukua. MHESHIMIWA NAOMBA HAWA WENYE VYETI FEKI WAPEWE MUDA WARISITI AU WARUDI DARASANI WASOME QT ILI WAPATE VYETI HALALI VYA KIDATO CHA NNE AU CHA SITA, wakifanikiwa kupata credit basi vyeti vyao vitambulike kuwa ni halali, Na hapo sasa Mafao yao walipwe, na Wale waliokuwa Kazini warudi.
Lakini pia baada ya kusafisha vyeti vyao vya kidato cha nne au cha sita basi kwa wale waliokwisha kupata digrii vyeti vyao vya elimu ya juu viwe ni halali!. Kwa wale watakaokaidi kurudi darasani kusoma basi rungu lilelile la kuachishwa kazi liwaangukie!!
Mheshimiwa Naomba hili kwa Watumishi walioguswa na Zoezi hili tu la Uhakiki, na si watumishi Watakaoingia katika Utumishi wa Umma baadae!.
Mheshimiwa Raisi nimeomba hivi nikitambua hali ya maisha ya watakaostaafu huenda ikawa ngumu, na pia nikitambua miongoni mwao huenda walikupigia kura.
Mheshimiwa naomba Ulifikirie ombi langu.
Wako katika Ujenzi wa Taifa.
Raia wa Tanzania.
YAH : OMBI LA NAMNA YA KUWASHUGHULIKIA WENYE VYETI FEKI