Joseph Tunu
Member
- Apr 8, 2016
- 55
- 14
1 Mheshimiwa Rais,
Ninakupongeza sana Mhe Rais kwa kazi nzuri sana unayofanya kuhakikisha kwamba wananchi wote wa Tanzania wanafaidi rasilimali za nchi yao kwa kupambana na ufisadi serikalini. Ninakuombea kwa Mwenyezi Mungu akupe afya njema na nguvu ya kuendelea kupambana na mafisadi na wanaotumia madaraka yao vibaya na hivyo kulitia Taifa hasara.
2 Mheshimiwa Rais,
Inaweza kuwa kazi ngumu kupambana na rushwa, ubadhirifu wa mali za umma, ufisadi nchini kama wananchi hawatashirikiana na serikali kutoa taarifa sahihi kuhusu mambo mbalimbali ya hovyo yanayofanywa na watendaji wasio waaminifu katika maeneo mbalimbali ya nchi. Kama Raia wa kawaida tunao wajibu wa kutoa taarifa sahihi za kila jambo lisilo la kizalendo lenye nia ya kuharibu ustawi wa jamii na Taifa. Kwa mujibu wa Ibara ya 27 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ni wajibu wa kila mtu kulinda mali asilia ya Jamhuri ya Muungano, mali ya Mamlaka ya Nchi na mali yote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi.
3 Mheshimiwa Rais,
Chuo cha Ufundi Arusha ni mali ya Mamlaka ya Nchi. Chuo cha Ufundi Arusha kina dhamana ya kutoa mafunzo ya Elimu bora kwa wananchi wote wa Tanzania. Katika kutekeleza majukumu yake, Chuo kimejikuta kikikumbwa na matatizo mbalimbali. Miongoni mwa matatizo yaliyopo ni upatikanaji wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia, upungufu wa malazi kwa wanafunzi hasa wa jinsia ya kike, Ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka.
4 Mheshimiwa Rais,
Kutokana na upungufu wa malazi wanafunzi wengi wa jinsia ya kike wanakaa nyumba za kupanga mitaani. Matokeo yake wanafunzi wengi wamekuwa wakipata ujauzito na wengine wengi wamekuwa wakishindwa masomo yao kwa kukosa mazingira rafiki ya kujisomea. Wanafunzi wanaoathirika zaidi ni wanafunzi wanaosoma ngazi ya cheti na stashahada. Wengi wa wanafunzi hawa wanatokea kidato cha nne (4) wengi wao wakiwa na umri wa chini ya miaka 18.
5 Mheshimiwa Rais,
Chuo kingeweza kuondokana na tatizo la upungufu wa malazi kwa wanafunzi hawa kama kungekuwa na nia ya kuondoa tatizo hilo kutoka kwa uongozi wa chuo. Sababu za kusema hivyo ni kwamba Chuo kilikuwa na matofali zaidi ya 20,000 lakini matofali hayo yalichukuliwa na uongozi wa chuo kwa ajili ya kufanyia kazi zao binafsi. Chuo kinapata simenti ya msaada kutoka kiwanda cha simenti Tanga lakini haifahamiki huwa inakwenda wapi. Laiti vifaa hivi vya ujenzi vingetumika kwa nia ya kutatua tatizo la malazi kwa wanafunzi ni kiasi kidogo sana cha rasilimali fedha kingeweza kutumika kujenga mabweni na hivyo kuondokana na tatizo la malazi chuoni.
6 Mheshimiwa Rais,
Chuo cha ufundi Arusha kina njia mbalimbali za mapato, lakini kwa sehemu kubwa chuo kinaendeshwa kwa madeni. Upande mmoja wafanyakazi wanadai chuo malipo ya stahili zao mbalimbali na kwa upande mwingine wazabuni/wafanyabiashara nao wanadai chuo mabilioni ya fedha kwa huduma mbalimbali walizotoa kwa chuo. Haifahamiki ni nini kilikuwa msingi wa madeni haya na mbaya ni pale ambapo haijulikani madeni haya yatalipwa lini.
7 Mheshimiwa Rais,
Kutokana na matumizi yasiyoeleweka wanafunzi wa kozi/fani ya Ujenzi na Umwagiliaji wameshindwa kufanya mazoezi yao inavyostahili. Wanafunzi hao wameshindwa kufanya mafunzo yao sawasawa kwa kukosekana shamba darasa kwa ajili ya kufanyia mazoezi (Practical practice). Wanafunzi hawa walitakiwa kuanza kufanya mazoezi hayo kwenye shamba darasa lililopo eneo la Oljoro tangu mwaka 2013 lakini mpaka sasa imeshindikana. Wafadhili mbalimbali wakiwepo DIDF walitoa fedha kwa ajili ya kujenga miundombinu ya shamba hilo. Kiasi cha TZS 300,000,000/= kilitolewa na DIDF kwa ajili hiyo lakini sehemu kubwa ya fedha hizi zilitumika kulipia malipo hewa na mpaka sasa wanafunzi hawajaweza kufanya mazoezi katika shamba hilo na haijulikani ni lini wataanza kufanya mazoezi kwenye shamba hilo. Kwa sasa shamba hilo limegawanywa kwa baadhi ya wafanyakazi wa chuo kwa lengo la kujilimia kwa ajili ya mahitaji yao binafsi.
8 Mheshimiwa Rais,
Katika mazingira yenye utata baadhi ya watumishi wa chuo walijilipa mishahara binafsi kuanzia Juni 2010 na haifahamiki ni mamlaka gani zilizowapa mishahara hiyo. Kwa mtizamo huo, imefikiriwa kwamba pengine mishahara hiyo ilipatikana kwa njia ya kutumia madaraka vibaya. Hali hii imezua manung’uniko na inaonekana kama ari ya kufanya kazi imeshuka kwa baadhi ya watumishi. Kadhalika, katika hali inayoonesha mashaka ya uaminifu, kipindi cha Januari 1999 mpaka Februari 2000 Mkuu wa chuo hakufanya kazi ya utumishi wa umma katika Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) alikokuwa akifanya kazi, lakini alilipwa mshahara na serikali kupitia cheki namba 3781513 na kuchukua mishahara katika kipindi chote bila kufanya kazi ya serikali.
9 Mheshimiwa Rais,
Tangu mwaka wa fedha 2010/11 Mkuu wa chuo amekuwa akilipwa tofauti na cheo chake. Kwa mfano, mwaka 2013/14 Mkuu wa chuo alitakiwa kulipwa kiasi cha Tsh 3,837,000/= kwa mwezi, lakini Mkuu wa chuo alilipwa kiasi cha Tsh 4,823,000/= kwa mwezi ikiwa na tofauti ya Tsh 986,000/= kama malipo ya ziada. Katika mshahara huo, Mkuu wa chuo alilipwa 20% ya mshahara wake kama posho ya kazi za ziada ambapo alilipwa kiasi cha Tsh 964,600/= badala ya Tsh 767,400/= kwa hivyo kulipwa kiasi cha Tsh 197,200/= zaidi ya alivyostahili kulipwa. Hivyo kwa mwezi mmoja katika mwaka wa fedha 2013/14 Mkuu wa chuo alilipwa kiasi cha Tsh 1,183,200/= zaidi ya alivyostahili. Kwa mwaka zililipwa kiasi cha Tsh 14,198,400/= ambazo zinaweza kuchukuliwa kama malipo hewa katika mshahara wa mkuu wa chuo
10 Mheshimiwa Rais,
Chuo cha Ufundi Arusha kimekuwa na bahati ya kupata vibali vingi vya ajira tangu mwaka 2010 hadi sasa. Serikali kwa nia njema imetaka kuboresha utendaji wa chuo kwa kukiongezea nguvukazi/rasilimali watu. Ni dhamira ya Serikali pia kupunguza tatizo la ajira kwa watanzania kwa kutengeneza nafasi nyingi za ajira iwezekanavyo ili watanzania wengi waweze kupata ajira. Ni mategemeo ya serikali kuwa ajira zinazopatikana zitashindanishwa kwa haki ili wale watanzania wenye sifa zaidi waweze kuchukuliwa na kupata ajira. Tofauti yake, kwa nyakati tofauti chuo kimetangaza nafasi za ajira lakini sehemu kubwa ya nafasi hizo huwa tayari zina wenyewe. Pamoja na wingi wa vibali vya ajira kupatikana na chuo kuweza kuajiri wafanyakazi wapya, sehemu kubwa ya wafanyakazi wa chuo waliopo wanaacha kazi kwa sababu mbalimbali kitu kinachoashiria kwambaa kuna tatizo au kuna jambo lisilo la kawaida mahali fulani katika uongozi wa chuo.
11 Mheshimiwa Rais,
Kwa mujibu wa Oda namba 7 (a) ya Tangazo la kuanzisha Chuo cha Ufundi Arusha namba 78 la mwaka 2007, Rais ndiye mwenye mamlaka ya kuteua Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo. Hivi sasa ni mwezi wa 7 tangu kuisha kwa muda wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo Bwana Abrahamu Nyanda (sasa marehemu). Hata hivyo Bodi imekuwa ikiendelea na vikao vyake licha ya kutokuwa na Mwenyekiti jambo linalotia shaka, kwa kuwa Bodi ya Chuo imekuwa ikihusishwa na tuhuma mbalimbali za upotevu na ubadhirifu wa fedha ya Chuo na umma kwa ujumla.
12 Mheshimiwa Rais,
Kwa mujibu wa Oda namba 10 ya Tangazo la kuanzisha Chuo cha Ufundi Arusha namba 78 la 2007, mwenye Mamlaka ya kuteua Mkuu wa Chuo ni Waziri mwenye dhamana ya Elimu. Kadhalika, kwa mujibu wa Oda namba 11, Mkuu wa chuo atatakiwa kuwa ofisini kwa kipindi cha miaka mitano (5) na anaweza kuteuliwa tena kwa kipindi kimoja cha miaka mitano kama utendaji wake wa kipindi cha kwanza ulikuwa mzuri.
13 Mheshimiwa Rais,
Mkuu wa chuo aliteuliwa Mwezi Septemba 2009 kuwa Mkuu wa chuo cha Ufundi Arusha. Mwezi Septemba 2014 Mkuu wa chuo alimaliza kipindi chake cha miaka mitano. Kulingana na taarifa za umri wa Mkuu wa chuo, isingewezekana kuongezewa kipindi kingine cha miaka mitano kwa kuwa kipindi hicho kingemfanya awe na umri wa zaidi ya miaka 60 inayohitajika kustaafu kwa mujibu wa sheria. Inavyoonekana, kuna mtendaji wa Wizara ya Elimu mwenye cheo cha Kaimu Mkurugenzi na baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Chuo wamechukua nafasi (take advantage) au kutumia mwanya wa ugeni wa Watendaji Wakuu wa Wizara ya Elimu kuficha ukweli huu ili Mkuu wa chuo aendelee na kazi kienyeji na haifahamiki lengo lao hasa ni nini.
14 Mheshimiwa Rais,
Yapo mambo mbalimbali ambayo yalifanywa na Uongozi wa chuo na kupitishwa na Bodi na hivyo kuzua maswali na hisia kwamba kuna namna na hivyo maslahi ya Taifa hayazingatiwi katika kufanya kazi kwao. Bodi iliruhusu na kupitisha malipo kwa ajili ya Mkuu wa chuo kuishi Hotelini kwa kipindi cha miezi mitatu (3) kuanzia Mwezi Oktoba, 2010 hadi mwezi Januari 2011 ilihali chuo kilikuwa na nyumba kwa ajili ya Mkuu wa chuo. Upande mwingine, Mkuu wa chuo angeweza kukaa Hotel ya karibu na Chuo ili kupunguza walao gharama za mafuta na kuwa nafuu kwa chuo na Serikali lakini alikaa hoteli ya mbali na hivyo kuongeza gharama kwa ajili ya mafuta ya gari.
15 Mheshimiwa Rais,
Bodi ya Chuo iliridhia Mkuu wa Chuo kuanzisha utaratibu mpya wa Mkuu wa chuo kuishi nje ya Chuo tangu January 2010. Utaratibu huu unasababisha matumizi yasiyo ya lazima kwa chuo na serikali. Chuo cha Ufundi Arusha kilijengwa kwa msaada wa Serikali ya Ujerumani, na wakuu wa kwanza wa chuo walikuwa wajerumani. Wakuu wote wa Chuo waliotangulia wakiwepo Wajerumani walikuwa wakiishi na familia zao kwenye nyumba ya Mkuu wa chuo iliyopo chuoni tangu mwaka 1978. Nyumba hiyo ilikataliwa na Mkuu wa Chuo wa sasa, hivyo kwa sasa nyumba hiyo inakaliwa na watumishi wengine. Kitendo cha Mkuu wa Chuo kukaa nje ya Chuo kimekuwa kikigharimu chuo bila sababu kwasababu kila siku mafuta yanatumika kwa ajili ya gari kwenda kumchukua na kumrudisha Mkuu wa Chuo, kitu ambacho hakikuwepo hapo awali.
16 Mheshimiwa Rais,
Mkuu wa Chuo alitumia zaidi ya Tsh 70,000,000/= kwa ajili ya kukarabati nyumba ya chuo iliyopo eneo la Korido Kijenge jijini Arusha ili ifae kwa matumizi ya kuwa Nyumba kwa ajili ya Mkuu wa chuo. Nyumba hiyo ilikuwa akikaa Mtaalamu wa Korea ambaye alifukuzwa kutoka katika nyumba hiyo ili ikarabatiwe kwa ajili ya Mkuu wa Chuo. PIa Mkuu wa Chuo alitumia zaidi ya Tsh 700,000,000/= kwa ajili ya kukarabati jengo la Utawala la Chuo huku sababu kubwa ikiwa ni kuifanya ofisi ya Mkuu wa chuo kuwa na ukubwa mkubwa pasipo sababu ya msingi. Ofisi ya Mkuu wa Chuo peke yake ilipanuliwa na kuwa sawa na ofisi tatu za kawaida. Wakati ofisi ya Mkuu wa chuo ikipanuliwa kwa gharama kubwa na kuwa kubwa kiasi hicho bila sababu yoyote ya maana, wafanyakazi wengine na hasa waalimu wanabanana wengi kwenye ofisi ndogo huku zikiwa hazina hata samani za ofisi.
17 Mheshimiwa Rais,
Ilivyo hivi sasa, sehemu kubwa ya matumizi ya fedha za chuo ni kwa ajili ya shughuli za kuendesha chuo (malipo kwa ajili ya posho za wajumbe wa Bodi ya chuo, malipo ya safari za uongozi wa chuo, mafuta na matengenezo ya magari yanayotumiwa na viongozi wa chuo, allowance mbalimbali za uongozi wa chuo). Inafikiriwa na ndivyo inavyotakiwa, kwamba sehemu kubwa ya matumizi ya chuo ingekuwa kwa ajili ya kufanyia mambo ya taaluma (training materials, technical materials, teaching materials nk.), lakini hapa ni tofauti.
18 Mheshimiwa Rais,
Uongozi wa chuo unatuhumiwa kwa kujihusisha na ufisadi kwa njia mbalimbali kupitia malipo hewa. Kati ya mwaka 2011/12 mpaka 2014/15 kiasi cha TZS 320,000,000/= fedha kwa ajili ya mafunzo viwandani zilitumika kama malipo hewa. Mishahara ya wafanyakazi 25 walioajiriwa na Chuo Januari 2014 kiasi cha TZS 30,000,000/=, zilitumika kama malipo hewa. Kati ya mwaka 2011/12 mpaka 2014/15 uongozi wa chuo ulibuni miradi hewa ya ujenzi na kulipwa wastani wa TZS 400,000,000/= kama malipo hewa. Kati ya mwaka 2011/12 hadi 2014/15 kiasi cha TZS 450,000,000/= kililipwa kama malipo hewa ya miradi ya ujenzi kupitia akaunti ya chuo, namba 01J1099202800 inayojulikana kama ATC-PCB.
19 Mheshimiwa Rais,
Orodha ya tuhuma za malipo hewa yaliyofanyika chuoni ni ndefu sana. Ukarabati na upanuzi wa jengo la Utawala, unakadiriwa kulipa malipo hewa kiasi cha TZS 300, 000,000/=. Ujenzi wa jengo la madarasa lijulikanalo kama jengo la Ujenzi na Umwagiliaji linakadiriwa kulipa malipo hewa kiasi cha TZS 1,500,000,000/=. Kadhalika kutoka katika mradi huu, zaidi ya matofali 20,000 yalichukuliwa na Uongozi kwa matumizi binafsi. Fedha ya msaada kiasi cha TZS 300,000,000/= kwa ajili ya kuendeleza shamba la Oljoro kwa kiasi kikubwa fedha hizi zilifanya kazi hewa na kupelekea kuwa malipo hewa.
Kati ya mwaka 2011/12 mpaka 2015/16 chuo kimekusanya kiasi cha wastani wa TZS 300,000,000/= kutoka mishahara ya wafanyakazi kwa ajili ya kodi ya nyumba. Makato ya fedha hizi yalidaiwa kutumika kwa ajili ya ukarabati wa nyumba za watumishi zilizopo chuoni. Sasa ni mwaka wa nne (4) bado nyumba ni chakavu na nyingine zinavuja na fedha yote hiyo haijulikani imefanyia kitu gani.
Kwa wastani, zaidi ya TZS billioni 3.6 zimetumika kama malipo hewa katika kipindi cha kati ya mwaka 2011/12 mpaka 2015/16, Chuo cha Ufundi Arusha
20 Mheshimiwa Rais,
Kuna jitihada kubwa zimekuwa zikifanywa na Uongozi wa chuo kuaminisha umma na serikali kwamba taarifa mbalimbali za kifisadi kuhusu chuo ni uongo na zinapotosha umma na serikali kwa ujumla. Nafahamu taasisi yako Mheshimiwa Rais ni kubwa na ina mkono mrefu kuliko mtu wa kawaida anavyoweza kufikiri. Natumia fursa hii kukuomba kwa heshima na taadhima, utumie utashi wako binafsi na mamlaka yoko uliyopewa kikatiba, kufanya uchunguzi/upelelezi wa chini kwa chini ili upate kujiridhisha kama ukweli uko wapi. Pale utakapobaini ukweli wote kama ulivyo, naomba uchukue hatua kama inavyostahili mheshimiwa Rais.
21 Mheshimiwa Rais,
Mimi na Watanzania wengi wenye mapenzi mema tunakuombea maisha yenye Heri na Baraka wewe na wasaidizi wako wote Serikalini. Mungu ibariki serikali ya Mhe. Rais Magufuli na Mungu ibariki Tanzania. Kwa heshima na Taadhima, naomba kuwasilisha.