Barua ya wazi kwa Mh. Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

Apr 20, 2017
76
234
Pole kwa majukumu ya utumishi wa umma.

Mh. Naomba utupie macho yako hapa: panakera sana!

Kuna hii taasisi inaitwa Pharmacy Council of Tanzania. Hatuelewi umakini wa utendaji kazi wake ukoje, ni utata mtupu!

Can you imagine watu walimaliza chuo mwaka 2015 hadi leo hawajapata usajili na hivyo hawajapata ruhusa ya kuajirika wala kujiajiri professionally maana sheria inawata wapate usajili kwenye baraza hilo ndipo waweze kupractise? Kumekuwa na ucheleweshaji na urasimu wa hali ya juu ktk taasisi hii.

Watoto wetu wanaumia, maisha ni magumu. Wamesoma ila ni kama hawakusoma. Ajira zinatangazwa zinawapita kushoto hawawezi kuajiriwa kisa hawajasajiliwa licha ya kuwa wameshafanya na kufaulu mitihani ya baraza hilo.

Walimaliza internship mwezi wa September mwaka jana hadi leo hii hawaruhusiwi kufanya professional job. Watawezaje hata kujiajiri?

Wanadaiwa na bodi ya mikopo wanawezaje kulipa ili hali hawana ruhusa ya kuajirika kwa taaluma walosomea? Vijana wanaambiwa sjui vyeti vyao vya taaluma vinakaguliwa na mamlaka ya ukaguzi (hapa naamini ni NECTA). Inawezekanaje ukaguzi huu ukachukua muda mrefu kiasi hiki?

Urasimu huu na wa aina nyingne utakoma lini kwenye baraza hili la taaluma ya famasia???

Tunaomba wizara iwasaidie vijana hawa.
 
Back
Top Bottom