EWGM's
JF-Expert Member
- Jul 22, 2013
- 1,521
- 2,112
Mh. Magufuli natambua una nia njema sana na auchumi wa nchi hii na kutimiza ahadi zote za CCM. Viwanda ni moja ya njia sanifu itakayoweza kukuza uchumi wetu na kupunguza idadi ya wasio na ajira nchini. Marighafi tunazo, maeneo tunayo, sera safi tunazo, fedha tunaweza kukopa, tatizo ni rasilimali watu kwenye nchi hii ndiyo tatizo kubwa na usipokuwa makini tutakuangusha.
Tanzania ina watu zaidi ya Miliomi 45 na asilimia 75 kati hao ni vijana ambao ni tegemeo kwa taifa lolote katika kujenga uchumi wa nchi. Pia tuna idadi kubwa ya vyuo vikuu nchini kwa sasa ambayo inatoa vijana wengi waliohitimu masomo ya elimu ya juu. Mh. Magufuli vijana wetu wana vyeti vizuri sana lakini wenye vyeti wenyewe wanamapungufu makubwa sana kwenye vipawa, ujuzi na uwezo wa uwakilishi wa elimu zao.
Wengine wanasema elimu ya bure mliyowapa ni bure kwelikweli sababu wanashindwa kuwakilisha kile walichokisoma kwenye uhalisia wa uchumi wa dunia ya sasa. Kwangu kikubwa nachokiona ni “ignorance” na “attitude” ya kujiona wana vyeti vya elimu ya juu basi inatosha. Hawajui dunia ya sasa inataka vipawa, ujuzi na uwezo vya uwakilishi wa elimu uliyosoma kwenye uhalisia wa uchumi wa kisasa.
Wakishahitimu na kupata vyeti vyao basi wao ndiyo wao na wanajua kila kitu, ukishakuwa hiyo “attitude” kujiendeleza inakuwa ngumu sana. Vijana wetu ni kama sangara akimwekwa kwenye dimbwi basi tayari na yeye anajiona nyangumi. Kingine Mh. Magufuli ni kuwa wakishatoka kule madarasani basi kiburi na dharau “ignorance” kwenda mbele na bahasha zao za kakhi mitaani, hawajishughulishi na chochote wanachokijua wao kinatosha huku hawafahamu dunia haiku hivyo.
Wasomi wa miaka ya nyuma walikuwa wakihitimuu elimu ya juu na wakiwa na kadi ya uanachama wa TANU au CCM wanakuta ajira inawasubiri tayari. Hali ya sasa ni tofauti kidogo sehemu kubwa ya uchumi wa viwanda unaendeshwa na sekta binafsi. Pia teknoloji imefanya dunia imekuwa kama kijiji na nusu ya idadi ya watu duniani iko kwenye harakati za mizunguko ya kikazi. Kazi ikitangazwa leo Tanzania mtu wa mashariki ya mbali ana uwezo wa kuiona na kutuma maombi dakika hiyo.
Hivyo Mh. Magufuli napenda kumnukuu Nelson Mandela aliwahi kusema hakuna taifa litakalo endelea ikiwa raia wake hawajaelimika. Elimu anayoiongelea Comrade Mandela siyo ile ya bure na kuwa na vyeti tu huku uwakilishi kwenye uhalisia hakuna. Pia mwanarakati mmoja wa India aliwahi kusema “kama elimu haijaingia kichwani mwako na moyoni mwako na kubadili uwezo wako wa kutafakari, kufikiri na kutatua mambo kwa madhumuni na malengo mema basi hiyo elimu haina tofauti na joho ulilolivaa na kulivua siku ya mahafali”
Hivyo Mh. Magufuli kama hautaliona hilo basi kazi na nguvu zote unazoelekeza kwenye viwanda zitakuwa za bure sababu vijana wako watakuangusha. Wako tayari kutumia Mb za mabando yao kukesha kwenye magroup ya Whatsapp and Instagram kuongea yasiyo na maana wala maendeleo ya nafsi zao. Wako tayari kupoteza muda wao kujua kama Mama wa Diamond anajua kingereza au la? Wako tayari kupoteza muda wao kujua leo mwanamuziki gani ana ugomzi (beef) na nani?
Wasomi wetu hawa hawasomi vitabu, hawako tayari kujiendeleza, hawako tayari kufanya utafiti wapo wapo tu kutwa kuongelea ngono, umbeya na mambo yaisiyo na manufaa kwao. Na ndiyo hawa hawa unataka kuwapa dhamana ya viwanda, Mh. Magufuli tafadhali fikiria hilo kwanza sababu vijana wako hawa ni mizigo na haya siyo majipu ni matambazi. Pia wamegawanyika kwenye pande mbili; upande huu magwanda na upande ule nambari wani lakini wameshau kuwa wote ni Watanzania na taifa linawatemea wao.
Vijana wetu wanataka kufanya mambo makubwa wakati hataka madogo tu waliyonayo yanawashinda kufanya kwa ustaha na ufasaha mkubwa. Mh. Magufuli tatizo kubwa la nchi yetu ni rasilimali watu na nyinyi wenyewe mnatuonyesha kwa mifano hawa wasomi wetu tatizo. Mkitaka kujenga barabara injinia mnamtoa China, mkitaka kutibiwa lazima muende India kama hamna imani nao kwenye hayo mtawapa vipi dhamana ya viwanda hawa wasomi (vijana) wetu? Ni sawa na kuwa na gari lako la kasi la kifahari ukataka kuliweka mafuta ya dizeli ni lazima litakufa tu.
Hivyo nakushauri Mh. Magufuli sitisha kwanza viwanda na anza kuwekeza kwenye elimu ya juu mpaka pale itakapoweza kutoa vijana watakaoweza kupambana na ulimwengu wa uchumi wa sasa ndiyo tuanza kufikiria viwanda. Taifa hili haliko tayari kwa viwanda bado wana mengi ya kujifunza kwenye ulimwengu wa sasa na mpaka pale tutakapobadili “attitude” na kufuta “ignorance” katika vichwa vyao ndiyo tufikirie viwanda. Na Mwalimu Nyerere alishawahi kusema “it can be done, play your part”. Hii ndiyo nafasi yangu kuanza kukufungua macho kuwa huku kwenye soko la ajira kuna mabomu na watakuangusha hawa wasomi wa sasa.
Wako mtiifu kwenye soko la ajira Tanzania
S.L.P Dar-Es-Salaam