Barua ya wazi kwa Mh. DC na Mstahiki Meya wa Arusha Mjini

Edward Sambai

JF-Expert Member
Nov 16, 2013
2,823
3,831
Awali ya yote nawasalimu na kuwapongeza kwa kufanikisha sherehe za Christmas wananchi wa Mkoa wa Arusha kusheherekea kwa amani pasipo hofu japo maisha ni magumu (Pesa Mitaani hakuna)

Mh. Mkuu wa mkoa Ndugu yetu Mrisho Gambo na Mh. Meya wa Jiji la Arusha sasa ni wazi kuwa tunakwenda kuingia mwaka 2017 huku mkiwa na deni kubwa la kutokutana ata siku moja na hili kundi muhimu au pengine niwaite askari wa miamvuli (wenyeviti wa serikali za mitaa) ili kupanga na kung'amua changamoto zinazowakabili.
Sijajuua ni nini hasa kimesababisha msikutane na hawa viongo japo hisia zangu zinapelekea niamini kuwa 2016 mlikuwa na mambo mengi na kufanya nafasi kuwa finyu ila 2017 ninamatumaini mtakutana nao.

Mh.Mkuu wa Mkoa na Meya wa Jiji la Arusha ningependa kuwakumbusha kuwa askari wenu wa miamvuli (wenyeviti wa serikali za mitaa) wanalipwa 50,000 tu kwa mwezi na hawana posho yoyote ile. Pia majukumu yao ni makubwa sana kimtaa na familia zao zinawategee.

Mh. Mkuu wa Mkoa mwaka huu 2016 Umethubutu, umeweza kwa vijana wa bodaboda kwa kuwatafutia pikipiki 200. Nakuomba mwaka ujao 2017 uthubutu kwa Hawa wenyeviti wa serikali za mitaa, wakopeshe ata pikipiki. Kwa kuwa unakauli mbiu isemayo "UONGOZI WENYE KUACHA ALAMA" nakuomba uache alama yako kwenye hili kundu la wenyeviti wa Serikali ya mtaa.

Mh. Mkuu wa mkoa na Mstahiki Meya sipendi kuwachosha kwa maneno mengi, nini imani Ujumbe wangu umewafikia na kwa kuwa Jamiiforums ni baba yao nasubiria kurudisha mrejesho na shukurani zangu siku zijazo.

Ninawatakia maandalizi mema ya mwaka mpya 2017
 
Gambo hawezi kukusikiliza maendeleo kwake ni kupambana na upinzani na kumuweka ndani lema. Hayo ndio maendeleo kwa tafsiri yake na icho ndicho kipimo cha utendaji kazi ambacho maboss zake nao wanaona jamaa anafaa kwa nafasi ya arusha.
 
Back
Top Bottom