Barua ya wazi kwa John Pombe Magufuli, Rais wa awamu ya tano Tanzania

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,276
23,227
Nianze kwa kusema wewe, Rais Magufuli ni binadamu na hakuna binadamu mkamilifu asiye na mapungufu, hiyo ni sifa ambayo Muumba wetu pekee anayo na anastahili kuwa nayo.

Mimi Mag3, nina hakika 100% kwamba nakusaidia Magufuli kuliko wanafiki wanaoshinda mitandaoni wakikusifia hata pale inapotakiwa uambiwe, hapana Mkuu, hapa umejikwaa.

Naamini Rais unasukumwa na nia ya dhati ya kuwasaidia ndugu zako Watanzania waondokane na matatizo yaliyoliandama taifa letu kama kupe kwa nusu karne toka tupate uhuru.

Katika misingi hiyo nina hakika kwamba Rais unafuatilia ukosoaji wetu ukijua unakusaidia katika kujua kwa nini wengine wetu tulikunyima kura na tulifanya hivyo kwa kusukumwa na nini.

Kila mtu anajua fika kwamba kuitoa CCM madarakani kwa Katiba tuliyo nayo ni ndoto, hata hivyo bila kujali maslahi binafsi, tuliwapigia kura wapinzani kwa kuzingatia maslahi ya taifa.

Tulifanya hivyo tukijua juhudi zitakazotumiwa na chama tawala kuhakikisha ndoto zetu zitabaki ndoto kwani uhuru na haki ni vitu viwili adimu sana katika msamiati wa CCM.

Wapo waliatanguliza maslahi binafsi na kwa tamaa ya ajira serikalini, mafanikio kibiashara na kitaaluma, walikupigia kura wakitegemea upendeleo kiitikadi katika teuzi mbali mbali.

Watu kama hao kamwe hawawezi kupata ujasiri wa kukuambia ukweli na kwa kuwa wengi ni wa chama chako, watakusifu mchana huku usiku wakilalama walivyo na wasiwasi nawe.

Wengine hatuko hivyo, hakuna tunachotaka kwako bali utawala bora unaotoa uhuru na haki kwa wananchi wote bila kujali kabila, jinsia, rangi, itikadi...yote kama yalivyooanishwa ndani ya Katiba.

Hivyo hatutasita kuita koleo kwa jina lake kama tutahisi hatutendewi haki kwa kufuata sheria na kwa bahati wote tunakubaliana kwa jambo moja la msingi...kutanguliza maslahi ya kwa taifa.

Tunajua kwamba watendaji wote wakuu waliotufikisha hapa tulipo ama walikuwa ni viongozi wa CCM na serikali yako kwani ndio wamekuwa waamuzi wa hatma ya nchi miaka yote.

Hivyo inajulikana wazi kuwa kama majipu yapo, ama yapo tele ndani ya chama chako au ndani ya serikali yako na yaendelee kutumbuliwa tu hata kama mengine yapo sehemu nyeti.

Tatizo linakuja pale majipu yanapokushangilia ukitumbua majipu, ni jukumu ketu kukushtua uwe mwanagalifu na huo ushangiliaji kwani hakuna namna unaweza kuwa kwa nia njema.

Tukikosoa tunaitwa maadui lakini kwa ukweli sisi tunafanya hivyo kwa nia njema tu na hapa tunasisitiza nia ni kukusaidia kiutekelezaji kuliko inavyopotoshwa na wanafiki waliokuzunguka.

Huna haja ya kutuogopa kama nia yako na yetu tunaokukosoa ni moja...kuliona taifa linanusurika kutoka lindi la umasikini...achana kabisa na wanafiki, ungana na wananchi wa Tanzania. Mungu ibariki Tanzania.
 
Unafiki ni pale mtu anaposema, Rais Magufuli hafai kuwa Rais wa Tanzania kwa sababu ni mwizi kama wezi wengine ndani ya CCM, halafu baadae anakuja tena na kusema Rais tunakusaidia kutumbua majipu hata yale yako sehemu nyeti.

Mtu asiyemnafiki ni yule anayesema Rais Magufuli hafai kuwa Rais wa Tanzania halafu baadaye anagundua kama fikra zake zilikuwa siyo sahihi baada ya kuona utendaji wa Rais lakini pia anaenda mbele zaidi na kumwambia Rais kuwa alikosea kudhani kama hafai.

Thread yako ni kuendeleza tu unafiki baada ya maamuzi ya Lowassa kuwafunua wanafiki wote ambao kwa muda mrefu walituaminisha ni wazalendo kweli kweli.

Yes, Rais Magufuli ni binadamu mwenye mapungufu na kwa mantiki hiyo, binadamu mwenye fikra ambazo siyo za kinafiki atampina Rais kutokana na mzani wa dhamira njema au mbaya katika kulitumikia taifa kwa faida ya wananchi wengi.
 
Naomba ujiulize hapa unamfikishia Rais Magufuli ujumbe gani? Umefanya vizuri kwani bila shaka akisoma barua yangu halafu anakutana na jibu lako, atang'amua mara moja kusudio la ujumbe ulioko katika barua yangu. Asante sana MsemajiUkweli kwa kuupa uzito zaidi barua yangu.
 
Achana na unafiki wa mchana. Bora ufanye unafiki usiku.

Unaikumbuka hii thread yako?
Ulienda mbali zaidi na kusema,
''John Pombe Magufuli kwa sasa ameteuliwa kuwa mgombea wa Uraisi kupitia CCM na moja katika ahadi zake za mwanzo kabisa ni kuendeleza walikofikia waliomtangulia. Sera anazoahidi kuzitekeleza ni zile zile za waliomtangulia lakini cha ajabu ni pale anapotuomba wananchi kumuamini kwa kuwa yeye, tofauti na waliomtangulia, ni mtendaji''

Kinachonishangaza unakuja hapa na thread ukidai unataka kumsaidia Rais Magufuli kutumbua Majipu.

Umesahau kuwa ulisema kutumbua majipu ni sera zile zile za waliomtangulia kulingana na thread yako?

Huu ndiyo unafiki ninaousema.

Acha unafiki ndugu yangu!
 
Mag you are not the right person to write that to JPM!

mnajifunga na issues nyingi sana

hivi huwa hwamuwezagi kabisa mkaishi kama nyie pas kufurahisha watu fulani fulani?
Kuna baadhi ya watu wanashangaza sana.

Mtu anakuja na unafiki wa mchana wakati amekalia bomu lenye hansard za mitazamo yake ya nyuma.

Watu wa aina hii hatutachoka kuwaeleza ukweli na kuwakumbusha unafiki wao.
 
Kwa kweli sijaelewa nini hasa mantiki ya hii barua. Labda mimi ndio sijaelewa.
Tulia, soma taratibu bila kukurupuka na bila shaka utaona mantiki ya barua. Rais Magufuli naye akitimiza wajibu wake bila kukurupuka wala jazba, bila shaka ataweza kupunguza kwa kiasi kikubwa kiwango cha ukosoaji. Kosa si kosa ila kurudia kosa...Wapinzani pia ni watanzania kama yeye.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mag you are not the right person to write that to JPM!

mnajifunga na issues nyingi sana

hivi huwa hwamuwezagi kabisa mkaishi kama nyie pas kufurahisha watu fulani fulani?
Kuna baadhi ya watu wanashangaza sana.

Mtu anakuja na unafiki wa mchana wakati amekalia bomu lenye hansard za mitazamo yake ya nyuma.

Watu wa aina hii hatutachoka kuwaeleza ukweli na kuwakumbusha unafiki wao.
Waberoya na MsemajiUkweli in the same pot? Wonders shall never cease...!
Mag3
Achana na unafiki wa mchana. Bora ufanye unafiki usiku.

Unaikumbuka hii thread yako?

Ulienda mbali zaidi na kusema,
''John Pombe Magufuli kwa sasa ameteuliwa kuwa mgombea wa Uraisi kupitia CCM na moja katika ahadi zake za mwanzo kabisa ni kuendeleza walikofikia waliomtangulia. Sera anazoahidi kuzitekeleza ni zile zile za waliomtangulia lakini cha ajabu ni pale anapotuomba wananchi kumuamini kwa kuwa yeye, tofauti na waliomtangulia, ni mtendaji''

Kinachonishangaza unakuja hapa na thread ukidai unataka kumsaidia Rais Magufuli kutumbua Majipu.

Umesahau kuwa ulisema kutumbua majipu ni sera zile zile za waliomtangulia kulingana na thread yako?

Huu ndiyo unafiki ninaousema.

Acha unafiki ndugu yangu!
Sababu moja tu inayonifanya nikujibu ni kuwa mimi ndiye niliyeanzisha thread la sivyo ningeku-ignore kama ninavyofanya siku zote.

Kama unataka kukumbuka ni hivi...baada ya Magufuli kuapishwa nilimpa siku 60 na hata JF sikuonekana. Katika hizo siku nilikuwa namsoma na nilipoona anajaribu kujitofautisha na waliomtangulia, nilimuomba apate ujasiri ajitenge nao na atuombe radhi Watanzania kwa ushiriki wake ndani ya serikali kwa muda wa miaka zaidi ya ishirini. Hiyo ingeipa nguvu dhana ya utumbuaji majipu.

Na sasa namtonya tena tena kuhusu anaowaita majipu. Bado anao ndani ya chama na serikali, anavyotumbua ni mapele tu huku majipu yenyewe yakimshangilia kinafiki. Ifike mahali akiri kwamba tunaomkosoa kiutendaji tunamsaidia kuliko wanaomshangiloia kama wewe MsemajiUkweli.
 
Ninafahamu huwezi kujibu hoja ambazo chimbuko lake ni fikra zako ndani ya hansard ya Jamiiforums.

Ni lini ulibadilisha mtazamo wako kuhusu Rais Magufuli mpaka umeamua umusaidie kutekeleza yale yaliyokuwa yanatekelezwa na Marais waliomtangulia?

Huu ni unafiki wa kiwango cha PhD!

Tanzania vituko haviishi!
 
Waberoya na MsemajiUkweli in the same pot? Wonders shall never cease...!

Sababu moja tu inayonifanya nikujibu ni kuwa mimi ndiye niliyeanzisha thread la sivyo ningeku-ignore kama ninavyofanya siku zote.

Kama unataka kukumbuka ni hivi...baada ya Magufuli kuapishwa nilimpa siku 60 na hata JF sikuonekana. Katika hizo siku nilikuwa namsoma na nilipoona anajaribu kujitofautisha na waliomtangulia, nilimuomba apate ujasiri ajitenge nao na atuombe radhi Watanzania kwa ushiriki wake ndani ya serikali kwa muda wa miaka zaidi ya ishirini. Hiyo ingeipa nguvu dhana ya utumbuaji majipu.

Na sasa namtonya tena tena kuhusu anaowaita majipu. Bado anao ndani ya chama na serikali, anavyotumbua ni mapele tu huku majipu yenyewe yakimshangilia kinafiki. Ifike mahali akiri kwamba tunaomkosoa kiutendaji tunamsaidia kuliko wanaomshangiloia kama wewe MsemajiUkweli.

Mag 3 rudi kwenye ubora wako

anzisheni maada za kusgikirisha ubongo na kujenga taifa

unayoyaandika ni kama unalialia tu

barua hasomi, na humfanyi lolote, kwanza ANA HAKIKA KABISA HAUKUMPIGIA KURA

bora ungemwomba lowassa afikishe ubunge

hayo majipu unayosema anayo ni pamoja na lowassa

ngau kuwa na shukrani, sidhani kama uliwahi kuota kuwa JPM atafanya haya

aibu!!
 
Mag3 rudi zamani zile kabla lowassa hajaja chadema

utaona mko wawili tofauti kabisa

ulishindwa kusimamia ukweli; mkatafuta sababu zenu ; leo hamna lolote la kuwaamini

I mean hata barua hii kesho unaweza ukairuka kuwa sio wewe umeandika
 
Kama yupo mtu moja ambaye hajabadilisha msimamo humu jamvini ni mimi Mag3. Toka siku ya kwanza najiunga na JF nilitamka wazi kwamba adui wa taifa hili naamini ni CCM na hajawahi kuwa mwingine. Wewe kwa upande wako unaamini adui wa taifa hili ni Lowassa na maadam hayuko huko CCM imekuwa safi na yatubidi tusahau mateso chini ya CCM kwa nusu karne. Huo msimamo haujabadilika hadi leo.

Kwanza ni kosa kuniita Chadema, mimi niliwaunga mkono Chadema lakini hata siku moja sijawa Chadema wala viongozi wake sijawahi hata kukutana na mojawapo. Hata ukiniamsha usingizini leo msimamo wangu utakuwa pale pale kwamba matatizo yote ya taifa hili yameletwa na CCM. Hivyo hivyo bado naamini kwamba matatizo hayo hayataisha hadi siku CCM itakapoondolewa madarakani.

Kama kwa kuendelea kuamini hivyo nazidi kupotoka naomba unikosoe lakini usinipakazie kwamba nimebadilisha msimamo. Kama tuko tayari kumsamehe Magufuli kwa ushiriki wake na bado yuko CCM, kwa nini tunamkataa ambaye kaamua kuhama na kuachana na CCM? Akili ya kawaida mbona inatakiwa ikiri kwamba aliyehama na kulikana genge hilo naye anafaa kupewa benefit of doubt?
 
Mag3 acha utoto mkuu
Lowassa hakuondoka CCM kwa kuacha lile genge, alikatwa CCM na alikuwa anautaka urais

maneno mengi tu
 
Unafiki ni pale mtu anaposema, Rais Magufuli hafai kuwa Rais wa Tanzania kwa sababu ni mwizi kama wezi wengine ndani ya CCM, halafu baadae anakuja tena na kusema Rais tunakusaidia kutumbua majipu hata yale yako sehemu nyeti.

Mtu asiyemnafiki ni yule anayesema Rais Magufuli hafai kuwa Rais wa Tanzania halafu baadaye anagundua kama fikra zake zilikuwa siyo sahihi baada ya kuona utendaji wa Rais lakini pia anaenda mbele zaidi na kumwambia Rais kuwa alikosea kudhani kama hafai.

Thread yako ni kuendeleza tu unafiki baada ya maamuzi ya Lowassa kuwafunua wanafiki wote ambao kwa muda mrefu walituaminisha ni wazalendo kweli kweli.

Yes, Rais Magufuli ni binadamu mwenye mapungufu na kwa mantiki hiyo, binadamu mwenye fikra ambazo siyo za kinafiki atampina Rais kutokana na mzani wa dhamira njema au mbaya katika kulitumikia taifa kwa faida ya wananchi wengi.
Mnafiki wa kwanza ni wewe
 
Mag3
Achana na unafiki wa mchana. Bora ufanye unafiki usiku.

Unaikumbuka hii thread yako?

Ulienda mbali zaidi na kusema,
''John Pombe Magufuli kwa sasa ameteuliwa kuwa mgombea wa Uraisi kupitia CCM na moja katika ahadi zake za mwanzo kabisa ni kuendeleza walikofikia waliomtangulia. Sera anazoahidi kuzitekeleza ni zile zile za waliomtangulia lakini cha ajabu ni pale anapotuomba wananchi kumuamini kwa kuwa yeye, tofauti na waliomtangulia, ni mtendaji''

Kinachonishangaza unakuja hapa na thread ukidai unataka kumsaidia Rais Magufuli kutumbua Majipu.

Umesahau kuwa ulisema kutumbua majipu ni sera zile zile za waliomtangulia kulingana na thread yako?

Huu ndiyo unafiki ninaousema.

Acha unafiki ndugu yangu!

Mkuu Msemaji Ukweli kuna kitu kinaitwa facts au vigezo katika hoja.

Mimi nipo pamoja na wewe kwa asilimia 100 na nakupa 5/5 kwenye hilo.

Watanzania wana budi kumuunga mkono raisi John Magufuli katika vita hii ya walio nacho ambacho wamedhulumu na wasio nao ambao wamedhulumiwa.

Nchi yetu imefanyiwa "economic sabotage" ya hali ya juu kabisa kuwahi kutokea tangu Uhuru.

Mungu Ibariki Tanzania na Mungu atubariki watanzania wenye nia njema na raisi wetu.

Go, Magufuli Go!
 
Wakati wa utawala wa Kikwete wapo viongozi wa dini waliokosoa serikali kwa ufisadi ,baadhi ya watu akiwemo Pascal Mayalla na Assah Mwambene wakalalamika sana Leo Magufuli ameingia madarakani viongozi wa dini wanamuombea asiuawe lakini akina Assah Mwambene na Pascal Mayalla ndo wa kwanza wanashambulia Ikulu.
Sasa hapo taabuu
 
Back
Top Bottom