wana jf;
mwanasheria wa zamani wa serikali ya jmt andrew chenge na takukuru wote kwa nyakati tofauti wamedai kuwa chenge hakuhusika katika kashfa ya rada.
lakini tuhuma na ushahidi uliopo katika barua ya sfo kwenda kwa mwanasheria mkuu wa jmt ya tarehe 21 march 2008 inaonyesha kuwa chenge, bado anao mkono katika tuhuma hizi nzito. Na bado anawajibika kuwajibu wa tanzania alipata wapi usd 1.5 million badala ya kuja na majibu mepesi kwa maswali magumu kuwa "hivyo ni visent vyangu na nina haki ya kikatiba kutokueleza nilikozipata"
ninachoshindwa kuelewa ni wanasiasa wa tanzania na watendaji wao; je wanatufanya watanzania hamnazo au mazezeta sana? Je, kwa barua hii na tuhuma zilizoelekezwa kwake ana majibu gani ya kutupa hata kama anadai sfo wamem- clear. Hizo usd 1.5 million alizitoa wapi? Na huyu ndiye sasa anataka awe spika wa bunge letu.
ole wao wabunge wakimchagua 2015 si mbali, mtakutana na hukumu ya moto!
je pccb na chenge wamedanganya? Ni kweli sfo hawajamhusisha chenge na tuhuma hizi?
naona kizunguzungu bado!
sources:
1. http://hawleyfeinstein.files.wordpress.com/2010/02/sfo-tanzania-request.pdf
2. http://hawleyfeinstein.files.wordpress.com/2010/03/tanzania-bae-allegations1.pdf
3. The guardian tanzania, "moment of shame", 7/2/10
4. bae's secret $12m payout in african deal | world news | the guardian
JF nayo haiishi kunishangaza !!
Mnanishangaza washikaji kutegemea kikwete kumtaka kuchukua hatua wakati mwenyewe ameiba kura kuingia ikulu. Kwa sasa wana jamvi tu brainstorm ni tuwasaidie vipi wananchi hasa wa vijijini wafahamu ubaya wa ccm kuwasababishia umaskini mkubwa kiasi hicho na wafahamu thamani ya kura yao. kwenye uchaguzi uliopita imeonekana kwenye maeneo yenye umaskini mkubwa ndo kikwete kapata kura nyingi now i am very much worried about thisUongozi wa serikali ya Tanzania ni dhaifu sana, sana. Ukimchukua mgonjwa wa akili pale muhimbili, wodi ya vichaa, na kumweka pale IKULU ya Tanzania atafanya mambo makumbwa ya kimaendeleo kuliko hawa watawala waliopo.
Wanasimama na sababu za kijinga, ati kuna watanzania wakitikiswa nchi na usalama wa taifa utatikisika.
Kikwete acha maneno maneno kemea rushwa, chukua hatua.
Kwanini hii isitumwe kwa dg wa takukuru kama kuna mtu ana e mail yao maana si wamesema mwenye kujua wala rushwa awasilishe kwao?
It appears that in breach of Tanzanian law, the Public Leadership Code of Ethics Act 1995 ("Ethics Act"), Chenge has not disclosed assets held in Jersey on the appropriate register. Under the Ethics Acts 1995, Chenge as Attorney General fell within the category of persons obliged to disclosed his worldwide assets annually, on a public register. The SFO has been informed by the PCCB that Chenge has failed to declare any assets on the relevant register
SFO wametafuna haya majinga yanatuambia yamechunguza wakakosa link; anyway basi mtuambie Chenge na Rashidi walifanya biashara gani mwaka 1998 mpaka kulipana kiasi hicho cha pesa!The material obtained fromthe authorities in Jersey also shows that a payment of $600,000 was made from the Franton account controlled by Chenge to an account in the name of Langley Investments Limited ("Langley") in May 1998. That account was controlled by Mr. Idriss Rashidi ("Rashidi")