- Tunachokijua
- Madai
Katika mitandao mbalimbali ya kijamii imesambaa barua inayodaiwa kutolewa na shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika (CAF) kuwa mchezo wa fainali ya pili ya kombe la shirikisho barani Afrika itachezwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa.
Uhalisia wa madai hayo
Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa barua hiyo si ya kweli. Ufuatiliaji kwa njia ya mtandao umebainisha nakala hiyo ya barua haijachapishwa na chanzo chochote cha kuaminika ama CAF wenyewe.
Aidha klabu ya Simba ambayo ndiyo inayoonekana kuandikiwa barua hiyo haijaandika chochote wala kuchapisha barua hiyo katika kurasa zao rasmi za mitandao ya kijamii. Aidha kurasa za mitandao ya mashindano ya Total energies shirikisho na klabu bingwa barani Afrika imekanusha kuhusika na barua hiyo.