Barua ndefu ya wazi kwa Rais John Pombe

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,866
5,742
Kwenye gazeti la Raia Tanzania la leo 22/01/2016 imeandikwa makala nzuri sana yenye kichwa cha habari "BARUA NDEFU YA WAZI KWA RAIS JOHN POMBE". Makala hii imeandikwa na mtu aliyejitambulisha kwa barua pepenassirmshanga@yahoo.com.
Lengo la mwandishi lilikuwa ni kumfikishia ujumbe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli umuhimu wa serikali yake kutoa kipaumbele katika tafiti za SAYANSI TUMIZI(APPLIED SCIENCES) badala ya Tafiti za siasa. Mwandishi ameelezea namna ambvyo mataifa tajiri yanavyojikita katika kufadhili tafiti za sayansi ya siasa katika mataifa maskini, Tanzania ikiwemo na siyo kufadhili tafiti za Sayansi tumizi. Mwandishi amefafanua vizuri sana sababu za mataifa hayo kufanya hivyo. Kwa ujumla wake ukisoma sababu hizo unagundua kuwa tafiti za sayansi ya siasa zinatufarakanisha wakati huo huo zinawaneemesha wao. Kufadhili tafiti za sayansi tumizi, tungeweza kuendelea na kuachana kuwa tegemezi, jambo ambalo kwao lingekuwa na athari kubwa.

Ni mfano ambao mwandishi ameutumia wa mataifa yaliyoendelea kama Marekani, China na Japani kutokana na kutumia pesa nyingi kuwekeza katika tafiti za Sayansi tumizi ndiyo ulinivutia sana kwenye makala hii.

Ukisoma mwanzoni mwa makala hii, utaona mwandishi alivyo na imani na serikali ya JPM hasa pale aliposema zamani kumfikia Waziri, Mkurugensi na maafisa wengine wa Serikali ilikuwa ni kama kumsubiri Mwana wa Adam arudi. Huu ni ujumbe mkubwa sana kwa Serikai ya awamu ya tano kwamba "WARUHUSU WATANZANIA WENYE TAALUMA YA KUFANYA TAFITI MBALIMBALI ZA SAYANSI TUMISI WABISHE HODI MAOFISINI WAO KWA USHAURI ILI TANZANIA YA VIWANDA ALIOINADI JPM WAKATI WA KAMPENI IWEZE KUFIKIWA".

Makala hii ni nsuri sana, rais yangu kwa washauri wa rais watakaoisoma makala hii wamfikishie ujumbe wa huyu mwandishi.
 
Hayo ndiyo maneno ya kuyaunga mkono siyo haya ya eti waziri wa mambo ya nchi za nje anatakiwa kuwa nje muda mwingi kuliko anaokaa nyumbani "Bernard Membe"
 
Back
Top Bottom