Barua kwako Mzee Joseph Sinde Warioba

Barua kwako Mzee Joseph Sinde Warioba

KAMBOTA

Senior Member
Joined
Mar 21, 2011
Posts
176
Reaction score
104
warioba+px.jpg

Na Nova Kambota, Jumatatu Novemba 3, 2014

Shikamoo mzee wangu Warioba na pole sana kwa masaibu yaliyokukuta jana .

Mimi mjukuu wako pasi na shaka ukiangalia kwenye diary yako utanikumbuka kwani niliwahi "kukutupia" swali moja pale chuo kikuu Mzumbe siku ya tarehe 16 mwezi Novemba 2011.

Tangu hapo hatujapata kuonana tena ingawaje nimekuwa nikifatilia harakati zako zote tangu hapo. Kwanini nimekuwa nikifatilia? Jibu ni moja tu, kwa namna ulivyonijibu siku ile sikutia shaka uelewa wako mkubwa sambamba na uzalendo wako usio na doa kwa taifa hili.

Ulizidi kunifurahisha zaidi kwa namna ulivyoratibu mchakato wa kukusanya maoni ya katiba mpya na uandaaji wa rasimu. Najua wapo baadhi ya "wakubwa" hawafurahishwi na namna unavyotetea kile unachoamini ni chema kwa vizazi vijavyo vya Tanzania, Mungu akubariki sana.

Vitimbi ulivyofanyiwa na maneno ya kejeli uliyojibiwa yanaonyesha kuwa hayajakuvunja moyo hata kidogo, kwani jana nilikuona ukiongea kwa uso uliojaa bashasha huku ukidhihirisha kuwa ungali na ari ileile ya kupigania katiba ya wananchi.

Sitaki kukuchosha kwa maneno mengi mzee wangu lakini nina uhakika Mungu yuko upande wako katika hili, tuliotega sikio na kukusikiliza tunajua unaongea ukweli mtupu na MSEMA KWELI NI MPENZI WA MUNGU.

Hata manabii walipingwa na kudhihakiwa hivyohivyo lakini leo tunawasoma na kuwaheshimu kama mashujaa wa imani, ni ukweli kuwa katiba lazima iwe mwafaka wa kitaifa na siyo mpasuko wa kitaifa, wanaokupinga wanalijua hili?

Wasalam,
Ni mimi Mjukuu wako mtiifu,
Nova Kambota
0712-544237
novakambota@gmail.com
 
Wananchi tunamuunga mkono Jaji Warioba, mtetezi wetu dhidi ya dhuluma za vikundi fulani vya watawala na watwana wao
 
kama una akili, mleta uzi ungemshauri warioba akatulie nyumbani kwake asubiri siku ya kupiga kura apige kura ya HAPANA. warioba kuendelea kuikosoa katiba pendekezwa, kimaadili ukizingatia yeye ni jaji, anakosea.

mnajua kwa nini hakimu au jaji huwa anajitoa kusimamia kesi iwapo mtoto wake au mjukuu au mkwe yumo ktk kesi ile?

tafakari!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
wananchi au maharamia!!! baada ya kura za maoni ndio utajua wewe na wenzako hamko miongoni mwa wananchi bali ni kundi la maharamia wa kisiasa.
TUNAWADHARAAAAAAAUUUUUUU
 
kama una akili, mleta uzi ungemshauri warioba akatulie nyumbani kwake asubiri siku ya kupiga kura apige kura ya HAPANA. warioba kuendelea kuikosoa katiba pendekezwa, kimaadilii ukizingatia yeye ni jaji, anakosea.

mnajua kwa nini hakimu au jaji huwa anajitoa kusimamia kesi iwapo mtoto wake au mjukuu au mkwe yumo ktk kesi ile?

tafakari!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!![/QUOTE

Sitaki kuamini unataka watz tusiwe tunahoji kitu kikiletwa na watawala, tabia hii ya kutokuhojiwa mambo yenu kwa kisingizio cha kuharibu amani ndio kimewalemaza uwezo wenu wa kujenga hoja, mmebaki kulazimisha hoja kwa kutumia dola. Mmejisahau mkatumia udhaifu wa watz kuhoji mambo muhimu, leo mna mikataba mingi mibovu ikilindwa na tabia ya usiri. Mchezo huu ndio utawafanya mpelekee nchi hii kwenye machafuko ya kulazimisha kubaki madarakani. Ila nikuhakikishie mda kidogo umebaki kila kitu kitafahamika.
 
Akili za kipuuzi tu ndizo zitakazompinga Mzee Warioba, au vichaa au waliokosa Malezi ya Wazazi na kukulia mtaani. Lakini mwenye akili timamu na aliyeelimika hawezi kwame kumpinga Mzee Warioba.
 
kama una akili, mleta uzi ungemshauri warioba akatulie nyumbani kwake asubiri siku ya kupiga kura apige kura ya HAPANA. warioba kuendelea kuikosoa katiba pendekezwa, kimaadili ukizingatia yeye ni jaji, anakosea.

mnajua kwa nini hakimu au jaji huwa anajitoa kusimamia kesi iwapo mtoto wake au mjukuu au mkwe yumo ktk kesi ile?

tafakari!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
unapenda mtawala mwananchi kutomwajibisha mbunge wake,unapenda mtawala kuwa na akaunti nje ya nchi?unapenda mbunge kuwa na vyeo lukuki kama uwaziri,uDC?Unapenda mtawala akipewa zawadi kama ya mama Tibaijuka aiweke nyumbani kwake?Jibu haya kwanza kabla ya kukuuliza juu ya zanzibar
 
tuache ushabiki tusimamie ukweli sasa vijana wenzangu ficheni uovu na kufumbafumba maneno kwa badae tutajuta. mzee waryoba anaemdhihaki atazamwe akili.
 
Nilisikiliza kwa makini jana Jaji Warioba lakini jinsi alivyopondaponda maana ya TUNU nikajua huyu mzee ana matatizo.
 
Tukishindwa tutafanya kama vile walivyofanya wenzetu wa bukinafaso
hiyo ndiyo silaha ya mwisho kabisa
ccm mujiandae
 
kama una akili, mleta uzi ungemshauri warioba akatulie nyumbani kwake asubiri siku ya kupiga kura apige kura ya HAPANA. warioba kuendelea kuikosoa katiba pendekezwa, kimaadili ukizingatia yeye ni jaji, anakosea.

mnajua kwa nini hakimu au jaji huwa anajitoa kusimamia kesi iwapo mtoto wake au mjukuu au mkwe yumo ktk kesi ile?

tafakari!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Acha unafiki ww ni haki yake kusema kile anachokiamini.. Wewe unaesema akalale asubiri kura.. Lala ww usubiri kuweka kura ya ndio..

Ni watanzania wangapi wameiona katiba pendekezwa, Ni watanzania wangapi wanaoweza kuisoma na kuielewa.. Acha kuongea utumbo ww
 
namuunga mkono mzee Warioba ila sioni mantiki ya huu uzi wako. PUMBA.

View attachment 198698

Na Nova Kambota, Jumatatu Novemba 3, 2014

Shikamoo mzee wangu Warioba na pole sana kwa masaibu yaliyokukuta jana .

Mimi mjukuu wako pasi na shaka ukiangalia kwenye diary yako utanikumbuka kwani niliwahi "kukutupia" swali moja pale chuo kikuu Mzumbe siku ya tarehe 16 mwezi Novemba 2011.

Tangu hapo hatujapata kuonana tena ingawaje nimekuwa nikifatilia harakati zako zote tangu hapo. Kwanini nimekuwa nikifatilia? Jibu ni moja tu, kwa namna ulivyonijibu siku ile sikutia shaka uelewa wako mkubwa sambamba na uzalendo wako usio na doa kwa taifa hili.

Ulizidi kunifurahisha zaidi kwa namna ulivyoratibu mchakato wa kukusanya maoni ya katiba mpya na uandaaji wa rasimu. Najua wapo baadhi ya "wakubwa" hawafurahishwi na namna unavyotetea kile unachoamini ni chema kwa vizazi vijavyo vya Tanzania, Mungu akubariki sana.

Vitimbi ulivyofanyiwa na maneno ya kejeli uliyojibiwa yanaonyesha kuwa hayajakuvunja moyo hata kidogo, kwani jana nilikuona ukiongea kwa uso uliojaa bashasha huku ukidhihirisha kuwa ungali na ari ileile ya kupigania katiba ya wananchi.

Sitaki kukuchosha kwa maneno mengi mzee wangu lakini nina uhakika Mungu yuko upande wako katika hili, tuliotega sikio na kukusikiliza tunajua unaongea ukweli mtupu na MSEMA KWELI NI MPENZI WA MUNGU.

Hata manabii walipingwa na kudhihakiwa hivyohivyo lakini leo tunawasoma na kuwaheshimu kama mashujaa wa imani, ni ukweli kuwa katiba lazima iwe mwafaka wa kitaifa na siyo mpasuko wa kitaifa, wanaokupinga wanalijua hili?

Wasalam,
Ni mimi Mjukuu wako mtiifu,
Nova Kambota
0712-544237
novakambota@gmail.com
 
kama una akili, mleta uzi ungemshauri warioba akatulie nyumbani kwake asubiri siku ya kupiga kura apige kura ya HAPANA. warioba kuendelea kuikosoa katiba pendekezwa, kimaadili ukizingatia yeye ni jaji, anakosea.

mnajua kwa nini hakimu au jaji huwa anajitoa kusimamia kesi iwapo mtoto wake au mjukuu au mkwe yumo ktk kesi ile?

tafakari!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Kama ni kosa angekamatwa acha kuuupotosha umma wewe.
 
Alichofanya Warioba ni hatua ipi kwenye mchakato wa katiba?

kama una akili, mleta uzi ungemshauri warioba akatulie nyumbani kwake asubiri siku ya kupiga kura apige kura ya HAPANA. warioba kuendelea kuikosoa katiba pendekezwa, kimaadili ukizingatia yeye ni jaji, anakosea.

mnajua kwa nini hakimu au jaji huwa anajitoa kusimamia kesi iwapo mtoto wake au mjukuu au mkwe yumo ktk kesi ile?

tafakari!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

wananchi au maharamia!!! baada ya kura za maoni ndio utajua wewe na wenzako hamko miongoni mwa wananchi bali ni kundi la maharamia wa kisiasa.
TUNAWADHARAAAAAAAUUUUUUU

Nilisikiliza kwa makini jana Jaji Warioba lakini jinsi alivyopondaponda maana ya TUNU nikajua huyu mzee ana matatizo.

attachment.php

Paul Makonda amekuwa kijana wa kwanza mpiga wazee.
 
Mungu anawaanika hadharani kwa uovu wao mwenye akili timamu anajua yanayoendelea. Hili bomu ipo sku italipuka vibaya sana ndipo Mungu atakapowafungua macho na itakuwa too late.
 
Back
Top Bottom