Barua kwa Waziri Mkuu:Anza na wahalifu waliokuzunguka kwanza,DECI ni kushindwa kwenu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Barua kwa Waziri Mkuu:Anza na wahalifu waliokuzunguka kwanza,DECI ni kushindwa kwenu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gembe, Apr 15, 2009.

 1. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #1
  Apr 15, 2009
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Mheshimiwa Waziri mkuu,

  Awali ya yote naomba kukupongeza kwa hatua yako ya kuzungumzia suala la DECI,na kuonehsa jinsi suala hilolilivyo la kihalifu,Umefanya vyema sana kwa kuwa kwa baadaye litakuwa tatizo la serikali pindi wannachi watakapoanza kudai pesa zao.Pia ningependa kukopongeza kwa juhudi zako za kuokoa pesa za wananchi zinazopotea katika stendi ya ubungo
  ambao ni uhalifu mwingine ambao unamhusu kada wa chama chako ambaye hana uwezo wa kuona mandishi madogo mpaka ulipoweka miwani yako

  Mhe waziri mkuu kwa tafsiri ya karibu kabisa uhalifu ni uvunjaji wa sheria kwa kuiba kwa njia mbalimbali,aidha kwa mtandao,au uvamizi na mara zote hatua kali huchukuliwa kwa watu wanaotenda uhalifu.

  Baada ya kusema hayo naomba nianze na maelezo yangu ya awali.Ni jambo lililozooleka sana kwa watu kupanga njama na kufanikisha wizi wa mabilioni ya pesa kwa njia zisizo kihalali,chukulia mfano wa suala la wizi wa Pesa Za EPA,KAGODA,IMPORT SUPPORT,RDC na wizi wa mabilioni ya pesa unaotekea katika wizara na ofisi nyingi za serikali.Kwa tafsiri yako huu wote ni uhalifu tena wa wa muda mrefu na inawezekana unaujua vyema sana kutokana na wewekufanya kazi katika wizara ya tawala za mikoa na serikali za Mitaa

  Mhe. Pinda kwa maoni yangu kabla ya kuanza na DECI ,ama hatua ambazo umepanga kuzichukua kwa watu wa DECI ningeomba uanze na wahalifu hawa ambo wako karibu yako na unafanya nao kazi kila siku.Hawa ndiyo wanochochoea uhalifu mwingine sababu watu wanaona maovu yanatokea na wanatafuta mbinu za kujitafutia Pesa.Na kwa kuwa wanacci wana maisha magumu,wamekata tamaa na umasikini wa muda mrefu wanatumbikia katika shimo hili la waharamia wnaofanya biashara haramu

  CHIMBUKO LA DECI
  Mhe waziri mkuu utakumbuka moja ya kauli mbinu iliyotumiwa kumnadi Rais kikwete ni kuwapa watanzania maisha bora kwa kutumia chachandu ya Tanzania yenye neema inawezekana.Kauli mbinu hii ilichochoea wananchi kumpa mwenyekiti wetu wa CCM kura nyingina kusema kweli wakati huo kwa kweli 'zilitosha'.

  Wananchi 430,276 kwa mujibu wa takwimu za DECI ndiyo wnachama wa DECI,hawa ndiyo wale watu waliokata tamaa ya kukosa maisha bora na wnaona ni bora na DECI kuliko serikali,DECI imewapatia maisha bora walimu,mapolisi,wanajeshi na waumini wa madhehebu mbali mbali!maisha bora wakliyoyakosa kwa muda mrefu na hawa ndiyo hawakufaidika na yale 'mabilioni'

  Mhe waziri mkuu,ukiangalia historia ya mabenki yetu ya ndani na vyombo ambavyo hukopesha pesa kama Bayport,FINCA na PRIDE ni kuwa ,yanatoza riba za juu sana ambazo hata kam mwananchi akikopa pesa na kuzifanyia biahsara hawezi kufaidika na hiyo pesa sababu pesa yote itaishia katika matumizi ya kawaida tu na kulipa deni.

  Benki nyingi na vyombo vya kifedha hukopesha kwa riba ya asilimia 19 hadi 22 kwa watu wa maisha ya chini,hivyo kuwa wia vigumu wanachi wengine kurudisha pesa hizo,suala hili linachangia watu wengi kutafuta pesa za haraka na ikitokea kitu kama DECI wanachi wanakuwa wa kwanza kuchangamkia.Wanachi wamezwe kutambua kuwa "hauwezi kula kwanza mpaka uliwe"na ndiyo mana wako DECI.

  Kimsingi DECI ni utapeli na naungana nwa ewe katika hilo,sababu biahsara yoyote ambayo inaingiza faida zaidi ya asilimia 40 ni kamali,hivyo unaweza kuliwa ama kula kwa faida itakayoaanishwa na wamiliki wa hiyo kamali.

  HATUA ZA KUCHUKUA KUHUSIANA NA DECI

  1.Hatua ya kwanza ni serikali kukaa na watu wa DECI na kuzungumza nao kujua pesa za wanachama ziko wapi na nia yenu kama serikali kuhusiana na mchezo huo.

  2.Nyie kama Serikali muangalie uwezekna wa kuiweka pesa hiyo katika mizunguko ya kibenki na kuona ni faida gani halisi inaweza kupatikana kama pesa hiyo ya wanchi ikiwekwa kwa mfumo wa FIxed deposit inaweza kupatika.Faida hiyo ndiyo mwashauri DECI waitoe kwa wanachi,inawezekan kama ukiwekza benki Billioni 13 unapata 10% kwa mwaka basi igawiwe kwa wananchi kama faida kwa pesa zao.

  3.Kama ni vigumu kwa hilo basi Serikali iwashauri wananchi kuwa pesa yao itaingizwa katika benki mojawapo inayomilikiwa
  na serikali na wawe kama wamenunu a HISA.

  4.Kama ikishindikana kabisa,Funga DECI na wananchi warudishiwe Pesa zao kama walivyopanda!

  HITIMISHO
  Mhe waziri mkuu,naamini sasa umetambua ni kwa kiasi gani watanzania wengi walivyo na masiah duni ukiangalia kwa undani zaidi ya asilimia 30% ya watanzania hawajui kesho watakula nini na pia hawajui nchi inakwenda wapi na hili ni Tatizo.Mie nina uhakika leo ukiuliza swali kwa waziri mmojawapo ni nini mipango ya wizara yake kwa mwak 2011 hatakuwa hajui.

  Tatizo hili ni la muda mrefu na ni bomu ambalo tunalitengeneza wenywe,embu kwa kuanzia hapa naomba muandae Program ya muda mrefu ya kuondoa umasikini na tuachane na Mkurabita,Mkumbita na TASAF sababu zimeshindwa kubadili chochote.Tujifunze mbinu kutoka nchi zingine kama Gambia na Noth Korea na hata nchi nyingine zenye misingi mizuri ya kimaendeleo.

  Mie nina imani kubwa kama tukitumia watalaam Wazalendo,wenye uchungu na nchi hii basi mpango mkakati wa kiuchumi utalisaidia taifa hili kuondokana na umasikini wa muda mrefu.Tuachane na wataala wa Serikali wa muda mrefu waliozoea "copy and Paste".Tuangaze vijana wasomi waliopo katika sekta mbalimbali na kuwatumia katika kuimarisha uchumi wa nchi hii kwa mipango mizuri.

  Mheshimiwa Waziri mkuu,naomba sasa kuhitimisha kwa kukuomba uanze kushghulikia wahalifu wakubwa waliokuzunguka na nikipata nafasi nitakuletea barua ofisini kwako.

  Mhe. Pinda tuache kulalamika kila siku,wananchi wanalamika na nyie pia?tuwasaidie watanzania wenzetu sasa na tuache kupiga porojo kwa kuunda tume kila siku zisizo na tija wala mafanikio.

  YES I have said "TANZANIA YENYE NEEMA INAWEZEKANA KAMA UKIONDOA WAHALIFU WALIOKUZUNGUKA"  wako Mwenye upeo na mwenye upendo wa Nchi yangu,

  GEMBE
   
  Last edited: Apr 15, 2009
 2. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #2
  Apr 15, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Viongozi wetu bana.
  Saizi mnalia weeee na DECI wkt kuna maswala mengi yamewashinda angalia KAGODA mnaona mpaka aibu kulizungumzia kweli walalahoi hawana chao.
  Mtasikia wanaunda TUME kuichunguza DECI.
   
 3. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #3
  Apr 15, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Viongozi wetu bana.
  Saizi mnalia weeee na DECI wkt kuna maswala mengi yamewashinda angalia KAGODA mnaona mpaka aibu kulizungumzia kweli walalahoi hawana chao.
  Mtasikia wanaunda TUME kuichunguza DECI.
   
 4. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #4
  Apr 15, 2009
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Fidel,

  Tume ilishwaundwa,Mie huwa nashangaa sana tume zinaundwa ili zifanye nini wakati sheria zipo na zinaelekeza nini cha kufanya?Kama sheria ni mbovu kwanini tusizibadili ili kupunguza mambo ya tume?

  We need to have strong team ambazo zinaweza kufanya kazi na kutoa majibu ya matatizo kama haya na siyo kuunda tume

  Kwanini siku zote wanaogopa kufanya maamuzi?tatizo mnalijua sababu za kisiasa tu na hapa ndipo tuliokosea,kuona faida za kisiasa ni bora kuliko maslahi ya nchi..It is on Now Kakobe ndani,Mtikila Ndani who is next after Pinda?
   
  Last edited: Apr 15, 2009
 5. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #5
  Apr 15, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Mkuu Gembe hizi tume mkuu mi iwa nashindwa kuelewa zinafanya nini?Na zikichunguza hatuoni hatua zozote zinazo chukuliwa wkt sheria zipo wazi mpaka uunde tume ya nini?
   
 6. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #6
  Apr 15, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Tatizo sisi waTanzania tunapenda sana kupiga siasa hata pale ambapo hapastahili siasa na chumvi nyingi si tunapiga tu subili utaona na Chilligati nae ataongea maana jamaa hawa wachungaji wanahusisha swala hili la uchaguzi ujao kuwa watawapiga chini.
   
 7. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #7
  Apr 15, 2009
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Hiyo ni another single ya CCM, kama kawaida wanaibua issue na kuambaa nayo kama hawana akili nzuri,wewe watu wamejiunga Deci kwa hiyari yao wenyewe hawajarazimishwa wala hawagombwi wakidhurumiwa ni juu yao wenyewe mbona serekali haingilii mabank yanavyotukopesha hela kwa riba kubwaa 24% + while ukiweka hela yako hata kwa fixed deposit faida haizidi 12%, sasa hapo si wangefuatilia hayo?Kagoda, Mwananchi Gold, Maremeta etc hela kibao imepotea, ya Deci waachie Deci wenyewe sana sana unatafuta ugomvi na wapiga kura 400,000+ watakucost CCM!
   
 8. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #8
  Apr 15, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Sera na programu za nchi hii hazina impact kwa watanzania wanyonge, watekelezaji wenyewe si makini, wanateuliwa kwa kiuswahiba. Yaani tunahitaji mapinduzi Tanzania, yafumue kila kitu tuanza upya. Hatutafika mbali au kuelekea huko wanakosema eti Maisha Bora kwa Kila Mtanzania kwa mtindo huu kama alivyosema Gembe, wa cut and paste (no value added katika cut and paste). Yaani nimechoka taabani, sijue Tz tunaelekea wapi.

  Kwa wengi ninaowafahamu wamenufaika sana na DECI awali, wamejenga, wamesomesha tena private primary schools. Leo hii watoto hao itabidi warudishwe katika primary zetu ambazo hazina waalimu, hata kama wapo wako busy na shughuli zao za ujasiriamali kwani mshahara haukidhi mahitaji yao. Je muda wa kufundisha kwa ufasaha wataupata wapi?? Kwanza ni hao hao waalimu ambao walikuwa wanaenda DECI (unapoteza more than a day) kufuatilia mbegu zao. Sasa DECI ni kwamba is delcared dead now, as for sure kasi ya kupanda haitakuwepo tena, so mavuno hakuna!!!!

  Maisha ya Mtanzania wa kawaida yataendelea kuwa mabaya, umaskini utaongezeka kwa kuwa serikali yao imeshindwa kuwasaidia. Kila mahali sasa kutakuwa na drop out (mashuleni, biashara ndogondogo, etc) sasa hawa watakuwa wageni wa nani?? Hii ni kuogeza tabaka ka umaskini uliokithiri.
   
 9. Elusive

  Elusive JF-Expert Member

  #9
  Apr 15, 2009
  Joined: Nov 26, 2008
  Messages: 223
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Tulinena zamani katika ukumbi huu kwamba hizi ponzi schemes aina ya DECI itawaliza watu, sasa yametokea Serikali haiwezi kuwasaidia waliopoteza fedha zao bali inazidisha vurugu huu ni kama utapeli wa mchana.
   
 10. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #10
  Apr 15, 2009
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Elusive,
  ndiyo mlinena zitawaliza watu je mliwapa suluhisho la matatizo yao?waachane na DECI na hawana kimbilio?Je mtawasaidiaje?

  YEs,walishindwa kuwasadia sasa wameamua kujitafutia pa kupata Mlo.zile bilini 25 zingetumika Vizuri haya mamabo yasingekuwapo?

  sijui ni kwa kiasi gani mabilioni yale yaliwasaida masikini..kKuna Ripoti?pesa zilitoka wapi?

  Tatizo siyo DECI,kuna tatizo jingine kubwa,hawataki kukubali tu kuwa kuna sehemu wameshindwa na wanhitaji msaada!
   
 11. kisu

  kisu JF-Expert Member

  #11
  Apr 15, 2009
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 803
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  kusema raisi. kutenda ......?? viongozi wote ni kitu kimoja. danganya toto.
   
 12. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #12
  Apr 15, 2009
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Kisu,

  Sie tunanena mkuu na kutenda kuna watendaji,jambo la muhimu ni kujiuliza kama wako tayari kutenda vile tutakavyo

  Mie nina uhakika Mkulu atasikia maombi yangu.Invisible na E-mail ya mkulu nimpenyezee..nitengenezee akaunti ya jamiiforums..ninayo ya jamboforums tu!
   
 13. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #13
  Apr 15, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Mkuu Gembe, nataka pia uwaulize au tuwaulize serikali ilikuwa wapi wakati DECI inaanza ikiwa mche sasa imekuwa mti uliokomaa na mizizi je ilikuwa wapi??? Nataka nielewe usalama wa taifa na raia na mali zao ulikuwa wapi? Hapo ndiyo nasema hatuna serikali na mapinduzi ya kila kitu yanatakiwa haraka sana. Huwezi kuniambia kuwa scheme hii ambayo ni pyramid in nature na ni upatu ambao penal code section zipo ambazo zinakataza mambo kama hayo zipo na hakuna hatua yoyote imechukuliwa hadi leo ambapo wananchi wengi watapoteza fedha zao. Wananchi wengine walikuwa wanakopa taasisi za fedha na kwenda kuwekeza DECI!!!! Sasa hapo ndipo mali na rasilimali za wananchi zitauzwa kufidia mikopo!!! Je hapo ni maisha bora kwa kila Mtanzania!!!???

  Ninaweza kusema kuwa hawa DECI ni International matapeli na ni lazima walihakikisha some of the governement machineries wako involved ili wawalinde!!! Inashangaza hata polisi walikuwapo hapo wakilinda makosa ya jinai?? Shame on to this government!!! Yaani haingii akiilini pale mabibo polisi walikuwa wanalinda ofisi zile machana kweupe!!! And Pinda et al... are saying it is a crime/criminal business!!!! Shame.

  Jamani imefika mahali ambapo ni lazima wanasheria wajitokeze kama ilivyo nchi zilizoendelea ambao kazi yao ni kutetea jamii kama ambavyo Rais Obama alifanya na ilimpa umaarufu. Jamani hivyo vitengo vya sheria mara TWLA, NOLA, TAMWA, etc waamke watetee maslahi ya jamii maana wao wana base sana kwa haki za mama na watoto. Serikali ni lazima ishitakiwe hapa, ieleze wanachi ilikuwa imelala wapi au walikuwa busy kuuza rasilimali na mashirika ya umma, yaani kuendelea kutufanya deprived of everything, naona hata pumzi wanataka kuchukua sasa.
   
 14. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #14
  Apr 15, 2009
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Mkuu maane,Kudos!

  Nitaongeza yote hayo,

  Kuhsu UWT,Hawa jamaa inawezekana walikuw awakipanga deal ya kunua X5 wakati suala hili linaanza.si unajua na wenyewe wanataka kuwa na motorcade kama ya Bush Kichaka!

  Mzee Mwanakijiji alishwawahi kuhoji integrity ya hawa jamaa,nadhani kuna haja ya kuammend ile sheria ya kuundwa kwa TISS ya mwaka 1996.Tuwe na mfumo tofauti na uliopo hivi sasa!
   
 15. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #15
  Apr 15, 2009
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  sema baadhi ya watz, sio watz wote wanapenda kupiga siasa kama wewe. wewe sio sisi ujue, labda ungesema"baadhi ya watz" lakini hiyo sweeping generalisation haina maana kabisa, umepoteza point yako.
   
 16. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #16
  Apr 15, 2009
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Deci haiwezi kuwa kama bank. hata wakiibrand iwe new, waibadilishe haiwezekani. cha maana selikali iangalie kama kuna uwezekano wanachama wake wapate chao na walale mbele, mfumo wao umeshaonekana haufai na ni kinyume na sheria. cha maana ni kuwalinda masikini walioweka hela pale. kwasababu wengi wao pale ni waalimu, wastaafu, wanajeshi na mapolisi, na wauza maaandazi kind of people. hao ni watu ambao elimu yao iko chini sana, kipato chao kiko chini sana, ndio maana hata uweke kikao mara mia, hawaelewi mnaposema Deci ni mbaya, hawatakuja wakuelewe kwasababu ndio watu vulnarable hapa nchini, wamesahaulika na mishahara yao ni midogo, wameenda kwenye upatu wameona wanapona kuliko mishahara sasa utawaeleza nini. selikali ichukue tu mzigo hata kulipa ikiwezekana kwasababu Deci ni mtu ambao umeshamea na kuwa mkubwa, kuukata ukadondoka ghafla lazima matawi yake yatabonda mimea mingine na kuharibika. someone will suffer kama selikali itakata bila kuwa makini.

  hakuna ubishi kwamba the thing ni mbaya. na sio endelevu, na haiendeshwi kisomi ni bomb. sasa selikali cha maana ni kulinda maslahi ya members ambao ni innocent, waliweka bila kujua, hawakuwa na malice yoyote ile ya kucheza upatu, hawakuwa na guilty mind kama hiyo. these innocent people ndo wanatakiwa walindwe na selikali. na selikali iwe makini, ila nijuavyo mimi, mwaka huu hauta katisha deci itakuwa historia, kwa nionavyo mimi. sijui. Mungu awasaidie wanaoitegemea kwasababu maangamizi hayo yatawadhuru sana. na kama ni mpango wa Mungu hiki kitu, basi kiendelee, ila kama sio mpango wa Mungu, kidondoshwe lakini kwa uangalifu. ila kudondosha lazima.
   
Loading...