Barua kwa mh. Mbowe

Barua kwa mh. Mbowe

mantegi

Member
Joined
Oct 16, 2012
Posts
27
Reaction score
20
Mwenyekiti wangu, wanachadema hatuko tayari tena kuona maccm yakijichagua bila kuchaguliwa halafu viongozi wa dini wanakufuata eti wanakushauri uwe na subira. Chaguzi zijazo liwalo na liwe lazima wananchi waruhusiwe kuchagua viongozi na sio kuchaguliwa na tume ya uchaguzi kwa maelezo ya haya mapanya yanayomaliza mazao yetu. Kiongozi yeyote atayeshindwa kusimamia na kutetea maamuzi ya wananchi lazima kuadabishwa.
Mwenyekiti wangu naomba tujipange mapema na chaguzi zijazo japo mapanya nayo yanajiandaa kwa kuiba kura. Napendekeza 2015 tuwe na mfumo wa kukusanya na kujumlisha kura nchi nzima mapema kabla hawajatangaza matokeo ya NEC, kuanzia kijiji/mtaa, kata, jimbo na taifa ili kujua ukweli kabla hawajachakachua. Kura zihesabiwe na kutumwa kwenye kata, kata zijumlishwe na kutumwa jimboni, jimboni zijumlishwe na kutumwa taifani. Hii njia iliwasaidia wabunge wetu wengi akiwemo Kamanda Wenje. Tuwatumie viongozi wa chama na pale ambapo hatuna viongozi basi tuwatumie makamanda wenye uchungu na nchi yao. Kuhusu ulinzi wa vituo vya kupigia kura usihofu wananchi watalinda na tuliona 2010. Mawakala wetu waandaliwe na kuelekezwa kusain karatasi ya matokeo na kukabidhi kwa uongozi wa chama ili zitumike kuonesha uwizi pale utakapo bainika.
Wambie viongozi wa dini wawashauri mapanya ili kuacha ubakaji wa democracy na sio kutuomba tumwache mmbakaji anaendelee kubaka ( haikubaliki). Haya mawazo ukiongeza na ya wadau wengine, nadhani chaguzi zitakuwa huru na haki ili kama ni kushinda tushinde halali na kama ni kushindwa tushindwe halali. Watanzania watulalamikia kwamba wanatupigia kura lakini tunashindwa kulinda kura zao. Hadi wanafikia hatua ya kutuhoji kama tunahongwa au la!. Watanzania wamechoka, wanahitaji mabadiliko hivyo tusimamie mabadiliko hayo hata kama yatatoa roho zetu ndo maana nitafurahi kama ''masalia'' wote watapukutishwa mwishoni mwa wiki hii kwani wanahujumu mabadiliko. Naomba kuwasilisha barua hii. Ahsante na kazi njema.
 
Ushauri murua kabisa. Kupiga kura bila kuilinda kwa mazingira ya Tanzania ni zero.
 
Back
Top Bottom