Barrick Waingilia Michezo?! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Barrick Waingilia Michezo?!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Steve Dii, Oct 13, 2007.

 1. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #1
  Oct 13, 2007
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Sina data nzuri na kuhusiana na wadhamini wa michezo hapa Tanzania, ila najua wimbi la udhamini limeongezeka kwa kasi katika nyanja mbalimbali za michezo hapa nchini. Kama habari ifuatayo inavyosema:

  Source link: ThisDay.

  Maswali ninayojiuliza sasa hivi ni kuwa:
  --Je, Barrick walikuwa wanadhamini michezo siku kitambo zilizopita?!

  --Kama walishawahi, je ni michezo ipi au timu zipi hizo?
  --Kama walishawahi, je walijitangaza kama hivi sasa?
  --Kama hawajawahi, je ni kipi kimewapelekea kuanza kudhamini timu nyakati hizi?
  --Kama hawajawahi/walishawahi, je hili ni jambo la maana wao kufanya kwenye nyakati kama hizi ambapo wanasakamwa kutokana na utata wa Buzwagi?
  --Je, wadhaminiwa wanajisikiaje kuhusu kukumbatiwa na washutumiwa?

  WanaJF, naomba msaada wenu kwenye maswali haya. Ahsanteni.

  SteveD.
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Oct 13, 2007
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,542
  Likes Received: 81,975
  Trophy Points: 280
  SteveD,

  Hawa jamaa wanakwepa kulipa mabilioni wanayostahili kulipa kama kodi kwa Watanzania. Si ajabu wameshaambiwa wakimwaga vijisenti hivyo kwenye michezo basi wananchi wanaweza kupunguza hasira zao dhidi ya mikataba feki waliyosaini ambayo haina maslahi kwa Watanzania. Lakini wanasahau kwamba Watanzania hawawezi kununuliwa kwa vijisenti vichache vitakavyoelekezwa kwenye michezo. Tunachotaka ni kusaini mkataba mpya utaowekwa bayana ili Watanzania wote tuweze kuusoma na kisha kuukubali kwa kuwa una maslahi kwa nchi yetu.

  Tunajua ni lazima wapate faida, lakini Watanzania pia tunataka kuona faida kutoka kwenye rasilimali zetu, sio ziwanufaishe wageni tu.
   
 3. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #3
  Oct 13, 2007
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Barrick kudhamini michezo si mara ya kwanza. Iwewahi kuihost kambi ya Taifa stars mara mbili kule Bulyanhulu na kuwalipia gharama zooote na dola 60,000 juu. Pia imewahi kudhamini michezo ya timu za mgodi na wanavijiji wanaoizunguka migodi yake yoote (Tulawaka, North Mara na Bulyanhulu) kwa kutoa jezi na zawadi kwa washindi.

  Kwa hili la michezo nadhani Barrick isidhaniwe kwamaba inajitangaza au kujisafisha. Ni utamaduni wao
   
 4. Dua

  Dua JF-Expert Member

  #4
  Oct 13, 2007
  Joined: Nov 14, 2006
  Messages: 2,481
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Halali mtu hapa hizo peremende hazina faida yoyote, mali wanayoiba ambayo ni haki ya WTZ ni lazima irudi tena sasa hawawezi kuchukua rasilimali yetu bure na kutupatia peremende ili tusahau. Sisi sio watoto wadogo wa chekechea.
   
 5. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #5
  Jun 14, 2017
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,300
  Likes Received: 22,089
  Trophy Points: 280
  Makenikia
   
 6. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #6
  Jun 14, 2017
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,447
  Likes Received: 7,187
  Trophy Points: 280
  Good.
   
 7. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #7
  Jun 14, 2017
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,447
  Likes Received: 7,187
  Trophy Points: 280
  Ten yrs later, Barrick na wao wanapata jambajamba.
   
Loading...