Barnaba alidanganya kwenye wimbo wa "nikutunze"

Chagga King

JF-Expert Member
Jul 6, 2011
1,850
1,065
Msanii Barnaba akiimba kiitikio (chorus) kwenye wimbo wa "Nikutunze" ambao ameshirikiana na José Chameleon alidanganya maana ya kile alichoimba Na kutafsiri nanukuu "wachaga tunasema aika mbe, yaani baby njoo nikutunze".
Akimaanisha maana ya "aika mbe" Ni sawa Na kusema "nikutunze" kwa kiswahili, maana ya aika mbe ambayo ni Maneno mawili ya kichaga yakiwa Na maana ya "aika/eeka" = Asante Na "mbe" ikimaanisha mtoto yoyote kwanza (kwakibosho) ingawa hii "mbee" Ina utofauti kidogo Sana kimatumizi kwenye variety nyingine za wachagga.

Sina uhakika Kama Barnaba Ni mchagga au lah, lakini kuimba kitu usichokijua Ni vyema kwa msanii au mtu yoyote kufanya utafiti wa maana ya hicho kitu kabla hujakitumia katika jamii,

Kiufupi alitakiwa kusema "ocho ngikutunse" /kikibosho/ simple tu.

So nyie wasanii kuweni makini mnapotumia lugha msizozifahamu, maana Kuna siku mtajikuta mnaongea matusi.

Huu wimbo Ni mzuri ila umekuwa ukinikera hasa kwenye kipengele hicho maana hakileti maana iliyokusudiwa na kinawapotosha wasiojua
 
Hapo ndio kuna umuhim wa msanii kujua lugha au maana halis ya maneno ya lugha fulani ambayo msanii anahitaji kuitumia kwenye wimbo wake!!!Big up Linex Linenga Sunday Mjeda wa VOA.
 
Msanii Barnaba akiimba kiitikio (chorus) kwenye wimbo wa "Nikutunze" ambao ameshirikiana na José Chameleon alidanganya maana ya kile alichoimba Na kutafsiri nanukuu "wachaga tunasema aika mbe, yaani baby njoo nikutunze".
Akimaanisha maana ya "aika mbe" Ni sawa Na kusema "nikutunze" kwa kiswahili, maana ya aika mbe ambayo ni Maneno mawili ya kichaga yakiwa Na maana ya "aika/eeka" = Asante Na "mbe" ikimaanisha mtoto yoyote kwanza (kwakibosho) ingawa hii "mbee" Ina utofauti kidogo Sana kimatumizi kwenye variety nyingine za wachagga.

Sina uhakika Kama Barnaba Ni mchagga au lah, lakini kuimba kitu usichokijua Ni vyema kwa msanii au mtu yoyote kufanya utafiti wa maana ya hicho kitu kabla hujakitumia katika jamii,

Kiufupi alitakiwa kusema "ocho ngikutunse" /kikibosho/ simple tu.

So nyie wasanii kuweni makini mnapotumia lugha msizozifahamu, maana Kuna siku mtajikuta mnaongea matusi.

Huu wimbo Ni mzuri ila umekuwa ukinikera hasa kwenye kipengele hicho maana hakileti maana iliyokusudiwa na kinawapotosha wasiojua
Kasema alitafsiri maana ya neno hilo au wewe ndo unembandikia maneno..?!
 
Inawezekana wewe hujamuelewa Barnaba, na maneno hayo yote pamoja huenda siyo tafsiri ya kingine bali ni mwendelezo wa sentesi. Wachaga wanasema aikambe, likawaneno tofauti na mtoto njoo nikutunze kama unavyodai.

Naona kama wewe ndo huelewi hivi lugha za muziki.
 
Basi kazi ipo, ubishi utakuwa Ni hulka yako, Na hili Ni tatizo la wengi katika kusikiliza miziki, hamsikilizi ujumbe uliokusudiwa. Anyway we elewa ulivyoelewa
 
Hata wewe ulieleta huu uzi umepotosha.

Tafsiri sahihi ya Aika Mbe ni Asante baba.
...haha, we unakijua kichagga?, eti Asante baba, aliyekuambia "baba" kwa kichagga Ni inaitwa mbe, kakudanganya vibaya, mi kichagga nimezaliwa nacho kule mtudu, Na nimekuwa nacho, so mi sikibahatishi, ninakijua vizuri.

Aliyekudanganya kamuulize tena
 
Back
Top Bottom