KERO Responded Baraza la Wauguzi (TNMC) lijitathmini, linakandamiza wauguzi

KERO Responded Baraza la Wauguzi (TNMC) lijitathmini, linakandamiza wauguzi

  • Thread starter Thread starter Anonymous (62c3)
  • Start date Start date
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Habari.

Baraza la wauguzi Tanzania (TNMC) ni Baraza lenye watumishi wengi sana nchini kaaribia asilimia 60 Kwa watumishi wote wa AFYA katika private sector na serikalini.

Ila hili Baraza limekuwa na changamoto sana na halisikii dawa kiasi kwamba linafanya wauguzi Sasa tukimbilie fani nyingine Kwa upande wa degree na kuachana na Baraza lao linaloendesha kimabavu.

Changamoto zifuatazo.

1. Uhuishaji wa leseni ulikuwa ni wa kidigitali mtu anatafuta CPD points 60 Kwa mfumo na kuihuisha leseni lakini Kwa sasa wanataka wauguzi wote nchini watafute point nyingine nje na online kitu ambacho ni kigumu Kwa watu wasio na ajira na hata walio makazini maana muongozo Wao unasema point utapata kwenye mafunzo na semina na kitu ambacho Kwa watumishi wengi semina wanapeana viongozi tu Tena wauguzi wa vijijini hata hawajui Wala kusikia kitu Cha semina maana zinaishia wilayani.

2. Baraza limekuwa likishindwa kutatua changamoto za wauguzi Kwa muda mrefu tofauti wanavyofa wenzao MCT Kwa kigezo Cha kusema Wao kazi yao kusimamia maadili ya muuguzi tu wakati muuguzi wa Tanzania amekuwa akikosa stahiki zake za msingi mpaka Leo na amekuwa mtumwa wa hospitali muuguzi halipwi House allowance, Risk allowance ila Daktari analipwa Baraza limekaa kimya.

3. Baraza mpaka Leo limeshindwa kutatua changamoto ya muundo wa mshahara Kwa wauguzi wa degree ambapo Kwa sasa wanalipwa TGHS C ilhali kisheria walitakiwa waanze TGHS D sawa na mfamasia au biomedical maana wote wamesoma miaka minne kitu ambacho kimekuwa siasa.

4. TNMC wamekuwa Kila siku wakilalamika kwanini wauguzi wanakimbia hii fani kiukweli yaliyonje ni mengi kuliko yaliyo ndani hivyo hili Baraza limekaa kimaslahi na Wala halina msaada wowote Kwa muuguzi zaidi ya kumkandamiza na kusubiri amefanya majanga wakae kikao wamfukuze.

Tutaukimbia tuu uuguzi kwa ukiritimba wa TNMC.

===== ================================

Majibu ya Baraza yapo hapa ~ Baraza la Wauguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) yatoa ufafanuzi kuhusu hoja za Mdau aliyehoji utendaji wao

Pia soma:
~
Baraza la Uuguzi na Ukunga (TNMC): Wahitimu wanaosubiri Leseni wawe watulivu, tupo kwenye mchakato
~ Baraza la Uuguzi na Ukunga (TNMC) mtusaidie tupate Leseni mapema, fursa zinatupita Mtaani
 
Hapo kwenye CPD point nje ya online courses naona wamedhamiria watu wakose hizo leseni, Mimi sijaajiriwa Niko mtaani hivi hizo seminar nazipataje
 
Back
Top Bottom