Baraza la mawaziri liundwe kwa kutumia formula ya Rasimu ya katiba ya Warioba

Martin George

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,695
1,470
Ndugu H. Polepole unaweza kutusaidia hapa, kwa changamoto tuliyonayo sasa inahitaji viongozi makini, waadilifu na waaminifu na huenda wakati wa uchaguzi 2015 hatukuzingatia sana sifa Bali tuliweka mbele ukwasi na uvyama, na inawezekana kabisa bunge letu linapungukiwa watu wenyewe ujuzi na weledi. Je, sasa siyo wakati muafaka wa kuitumia formula inayotupa idadi ya mawaziri iliyoandaliwa na tume ya Maji Warioba? Kiukweli kwa sasa yawezekana watu wenyewe sifa stahiki wakawa wamepungua na hii itampa wakati mgumu mh Rais 'anapolazimika' kufanya uteuzi na option pekee inayokuwepo ni kupunguza ukubwa wa baraza la mawaziri. Tumeshuhudia mwandishi mkuu wa Katiba Pendekezwa akiingia ktk kashfa nzito hali inayotuhalalisha kurejea kwenye rasimu ya Warioba. Ningeomba pia tume yetu ya uchaguzi ifanye kama ile ya Kenya MTU fisadi hata kama chama chake kimemteua,jina likifika tume AKATWE!!!
 
CCM ni lazima kife ndiyo utakuwa muarobani. Huwezi kuweka divai mpya kwenye viriba vya zamani.
 
Back
Top Bottom