Baraza la mawaziri linalochimbia nchi kaburi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baraza la mawaziri linalochimbia nchi kaburi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by hittler, Aug 25, 2011.

 1. h

  hittler Member

  #1
  Aug 25, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni muda mrefu sasa nimekuwa nikitizama mfumo mzima wa uongozi katika baraza la mawaziri Tanzania. Mawaziri wamesahau kabisa wajibu wao, wamejikita zaidi katika siasa mbovu za makundi na kufikiria zaidi uchaguzi mkuu ujao. Huo ni ufinyu wa mawazo unao lichimbia Taifa kaburi. Mawaziri watambue kuwa wananchi wanaangalia utendaji wao na kupima uwezo wao. Malumbano ya majukwaa si muhimu kwa huu muda, muhimu wakae washauriane nini cha kufanya ili kuweza kulinusuru taifa. Umbea na Mipasho majukwaani si sifa ya kiongozi bora, kama kuna jambo wakae walitatue wenyewe, sisi tunataka utendaji. Watambue kuwa 2015 bado ni mbali na kila binadamu ana mipango yake ila Mungu ndiye muamuzi, wengi wanapanga lakini wanakufa kabla ya kufikia malengo vivyo hivyo serikali inaweza kuanguka pia kabla ya 2015 na kufuta ndoto za hao wote wanaosahau wajibu wao na kukimbilia Ikulu
  Mbaya zaidi anguko la serikali si la Kikwete peke yake bali ni lao wote, na ata kama ni kushtakiwa atoshtakiwa Kikwete mwenyewe bali na wafuasi wake ambao ni watendaji wakuu wa serikali, Kina Samweli Sitta na wenzako hayo maneno mnayoyasema majukwaani huwa mnamwambia Kikwete pia au mnataka tuwaone bora ili hali mpo katika serikali legelege? Naogopa sana hili lisije kuwa ni baraza la mawaziri linalochimbia nchi kaburi
   
 2. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #2
  Aug 25, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,100
  Likes Received: 1,424
  Trophy Points: 280
  Mh, sijajua unalaumu baraza zima la mawaziri au Samuel Sitta na kambi yake?
  Tangaza interest yako kwanza, nitarudi kuchangia...
   
Loading...