Baraza la Mawaziri lijalo

Sungurampole

JF-Expert Member
Nov 17, 2007
984
205
Kwa demo aliyokwisha kuonesha Magufuli na PM nafikiri sasa sifa za mawaziri wake naziona wazi:
1. Mzalendo- kwa vile neno limekwisha kuchafuliwa sana nielezee kuwa huyu ni mtanzania yule akiona kitendo/uamuzi wake umewasaidia watanzania walio wengi moyo wake unaburudika, akiona kitendo/uamuzi wake umewaumiza watanzania walio wengi moyo wake unasononeka hata kama yeye na wachache wamefaidika.
2. Mchapakazi wa ukweli na makini siyo mkurupukaji na mpenda sifa-kabla kuanzisha jambo analitafari kwa umakini, analifanyia kazi kwa umakini na hapati amani mpaka alikamilshe kwa mafanikio
3. Jasiri- nia njema na taifa iliyopo moyoni mwake inamsukuma kukabili mambo magumu ambayo wengine wangesema hayawezkani(hili ndivyo lilivyo)
4. Umri siyo kigezo cha msingi ? ili mradi ni mtu mzima
5. Uzoefu wa uwaziri siyo kigezo cha msingi kwani mara nyingi hiyo ni 'long time wrong experience'
6. Mwenye 'zero tolerance' na ufisadi (kama Magufuli na PM wake wanavyoonesha mpaka sasa)
7. Mbunifu- anayechukia 'Business As Usual'
8. Anayechukia umasikini wa watanzania. Ambaye hili linamnyima usingizi.
9. Mwenye hofu ya Mungu
10. Mwenye uwezo mzuri wa kufanya maamuzi (Proactive-hasubiri kuambiwa) na asiyeogopa kukosea
Tutafakari wote.
 
Ili kuwapata watu hao,itambidi
1.Aunde baraza la watu wasiozidi watano.
2.Akawatafute nje ya system yaani nje ya CCM.
 
Back
Top Bottom