Makau Js
Member
- May 25, 2017
- 93
- 233
Ujana wa sasa umejaa ujivuni na starehe na asilimia kubwa ya vijana wa kizazi hiki tumepoteza nidhamu mbele ya jamii na kwa wazazi wetu.
Siku hizi kijana anajitafutia mwanamke kisha anampa uja uzito kisha anaenda kuwajulisha wazazi wake kuwa amepata mchumba ambaye tayari ana mimba .
Mzazi anakubali shingo upande hata kama ameona tatizo kwa binti mwenye uja uzito kwa kuwa tayari ameletewa mwanamke mwenye uja uzito ambaye hamjui wala kumzowea mama mkwe wake :anakubali huku akiwa anaona mapungufu makubwa.
Tunatengeneza ndoa na wanaume/wanawake wasiojua tuliko toka na kushindwa kuwa na future nzuri mbeleni sababu tunatengeneza ndoa pasipo msaada wa kimawazo na kiroho kupitia wazazi wetu ,kiasi ambacho kimetufanya tumezalisha ndoa zilizopoa na kukosa mvuto wa malezi bora na mapenzi bora.
Mama yako mzazi alijinyima kuvaa vizuri ,ili wewe upate elimu bora na malezi bora :Baba yako mzazi alitumia machozi jasho na damu kutafuta pesa ili wewe usome bila matatizo na uishi maisha mazuri ila yeye alikosa mahitaji yake ya muhimu kwa ajili yako ili uwe kijana mwenye maisha mazuri na mafanikio.
Umemaliza chuo na kupata kazi nzuri lakini umewasahau wazazi wako , siku pekee ambayo ulikuwa karibu na wazazi wako ni nyakati ambazo ulipeleke mke wako kwa utambulisho na kuwapa jukumu la taratibu za ndoa huo ndio wakati pekee ambao ulikuwa karibu na wazazi wako pekee.
Mzazi huwa hataki pesa ya mwanae siku zote ,mzazi hujisikia furaha na faraja pale mtoto wake anapomkumbuka kwa njia ya simu,barua hata email .Mzazi husikia faraja kuona wajukuu zake wanamtembelea nyakati za likizo na kupigiwa simu na wajukuu zake .
Vijana tunakosa Baraka za wazazi wetu kwa kuwaweka mbali na sisi ,wakati wazazi walijinyima ili sisi tusome na kuwa na maisha mazuri ,tunafanya kazi zenye mishahara mizuri ila hatustawi sababu tunatawanya pesa badala ya kukusanya ,wazazi wana masikitiko kwa kuwatenga wakiwa bado wangali hai.
Vijana wa kiume tunatumia muda wetu mwingi kuhonga wanawake kwa kuwanunulia vitu vya thamani na kuwapangia nyumba vimada ilhali wazazi wetu wananuka umaskini na matatizo na maradhi yasiokwisha sababu nguvu zao zote walimaliza wakiwa vijana wakitupigania kututafutia maisha mazuri na elimu bora.
Turudishe mila na utamaduni wetu wa kuwa na upendo na mshikamano na wazazi kwa kuwa nao karibu ili tuweze kupata Baraka za ndoa,kazi na kuwa na kizazi bora na kuifanya dunia kuwa sehemu salama …
Kama umeshindwa kumjali mama na baba yako wakiwa hai unaweza kuja tembelea makabuli yao wakiwa wametangulia mbele ya haki?
Kumbuka anayemheshimu Baba yake anajipatia msamaha wa dhambi zake na anayemuheshimu mama yake anajiwekea hazina kubwa
Mtunze na kumpenda Mama na babB yako wakiwa bado hai ili upate baraka zenye tija na wewe ustawi kimaisha kwa kila unachofanya.
️
️
[HASHTAG]#BarakaZaWazazi[/HASHTAG]
Sent using Jamii Forums mobile app