Samson Ernest
JF-Expert Member
- Aug 28, 2014
- 1,118
- 1,565
Isa 17:4 SUV
[4] Tena itakuwa katika siku hiyo, utukufu wa Yakobo utapungua-pungua, na kunona kwa mwili wake kutakonda.
Onyo linalotolewa hapa ni kwa sababu ya kupungua kwa utukufu wa Mungu kwa taifa la Israeli, waligeukia mambo mengine yasiyompendeza Mungu wao.
Utukufu wa Israel ilikuwa ni heshima waliyokuwa nayo, nguvu, na ustawi mkubwa waliokuonao wakati wana Mungu wao.
Kupungua kwa utukufu wao, maana yake heshima yao ilishuka chini, na ile hadhi ya Taifa ilikuwa chini, iwe ni kisiasa, kiuchumi, au kiroho, walikuwa wameshuka chini.
Athari hizi zilikuja baada ya kuasi kwao, kuabudu sanamu, na kutegemea msaada wa mataifa mengine badala ya Mungu, yaani waliona wanaweza kupata msaada mkubwa nje na Mungu.
Ndivyo ilivyo na kwa watu leo, wanaweza kuwekeza akili zao na mategemeo yao makubwa kwa watu, na kwa Mungu wanaondoka kabisa.
Biblia inazungumzia hapa kunona kwao, inamaanisha ile neema ya Mungu iliyokuwa juu yao, na kukonda kwao ni ishara mbaya ya kupoteza baraza za Mungu walizokuwa nazo.
Ndipo tunapata jibu kuwa, baraka za Mungu kwa mwana wa Mungu zitadumu kwake ikiwa ataendelea kuwa mwaminifu mbele za Mungu, siku akiacha kuishi katika utaratibu mzuri, na hizo baraka zinaondoka kwake.
Utukufu wa Mungu kuondoka kwa mtu kwa maana nyingine ni ishara ya baraka za Mungu kuondoka, tunapaswa kuwa makini sana katika maisha yetu ya kila siku tusipoteze baraka hizi.
Tunaweza kuzuia kupoteza baraka hizi za Mungu kwa kumrudia haraka tunapogundua mahali tulikosea, tukiwa na shingo ngumu inaweza ikatugharimu katika maisha maisha yetu.
Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia na kutafakari
Mungu akubariki sana