PostGE2025 Baraka Nandonde na Isaya Mwita wapewa nafasi mpya CHADEMA Pwani

PostGE2025 Baraka Nandonde na Isaya Mwita wapewa nafasi mpya CHADEMA Pwani

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
505
Reaction score
887
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Pwani kimewateua Baraka Mussa Nandonde kukaimu nafasi ya aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Kanda hiyo, na Isaya Mwita kushika nafasi ya mweka hazina wa CHADEMA kwa ukanda huo.

‎Taarifa hiyo imetolewa Desemba 24, 2025, na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Pwani Ntele Benjamin, ambapo amesema uteuzi huo umefanyika kulingana ibara ya 6.3.5 ya katiba ya CHADEMA ya mwaka 2006 toleo la mwaka 2019.

‎Kulingana na taarifa hiyo, chama hicho tarehe 20 Desemba 2025 chini ya mwenyekiti wake wa Kanda, Boniface Jacob, kiliketi kikao cha kawaida cha Kamati tendaji ya kanda ambapo kilifanya ukaimishaji wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti na Mweka Hazina wa kanda hiyo.

Nandonde.png
 
Back
Top Bottom