Baraka ft Ali kiba na video ya nisamehe

George Betram

JF-Expert Member
Oct 10, 2015
4,018
4,907
Leo katika pitapita zangu youtube nimekutana na video ya Baraka na Ali Kiba inayokwenda kwa jina NISAMEHE.

Kilichonishangaza ni kwamba ina wiki moja tangu iwekwe youtube lakini mpaka sasa ina viewers 120k tu..!

Hivi nini shida..?

Ali Kiba ni King wa Bongo Fleva na Baraka ni Crown Prince wa Bongo Fleva, hii ni kwa mujibu wa wasanii wenyewe.

Lakini mapokezi ya kazi yao hayatuthibishii hilo.

Je, shida iko wapi..?

Screenshot_20161009-092141.png


Baraka the PrincexAli Kiba: Nisamehe
Link:

https://m.youtube.com/watch?feature=youtu.be&v=el6Z2qziRFA
 
Hii nyimbo imebuma japo clouds wanajitaidi kuiboost wanaipiga kila kipindi
 
me naona timing ya kutoa huu wimbo ndo ilikua tatizo...bonge moja ya video ila haiwez furukuta huku kuna salome,kule kuna inde so itakua ngumu
Hapo kwenye timing nafikiri uko sahihi ndugu...
Sasa sijui management ya hawa jamaa ilifikiria nini..?
 
Nyimbo mbovu video kali" viewers pia huangalia nyimbo kwanza so kama audio ingekua kali nadhani ingeboost views kwenye YouTube ila watu hawana time nayo
 
Hapo kwenye timing nafikiri uko sahihi ndugu...
Sasa sijui management ya hawa jamaa ilifikiria nini..?
Mkuu akisubiri hiyo timing atasubiri sana maana WCB kila wakiamka wanatoa hit songs. Muhimu atoe ngoma Kali za kuwanyamazisha WCB.
 
Nyimbo anazoimba BEN POL, kama zingeimbwa na mmoja wa hao watoto wa Kigoma, DSM pasingetosha.
 
Nyimbo anazoimba BEN POL, kama zingeimbwa na mmoja wa hao watoto wa Kigoma, DSM pasingetosha.
Ben Pol na Barnaba Boy...
Huwa nasikitika sana nikisikiliza nyimbo za hawa jamaa...
Uwezo wao(kimuziki) na mafanikio yao havilingani..!
 
Au mashabiki wao hawana MB za kuwawezesha kuingia youtube..!?
Ila mimi nimewaongezea viewer leo kwasababu nimeichungulia kidogo video yao...
Pia naamini huu uzi unaweza kuwaongezea viewers wengine..!
aisee umesababisha nimeifungua tena ila sijasikiliza ni wimbo wa hovyo sana kwa upande wangu sijui na wenzangu pia kama wanaona hivyo
 
Tatizo kwa wimbo huu ni link official... kuna link tofauti za wimbo huu na zote zina viewers kati ya 50000 na 150000..... Inatakiwa Baraka ajipnge awe na account official ili pia imsaidie kuingiza pesa. Sina imani kuwa hata link uliyotumia kuutazama wimbo huo ni official
 
Back
Top Bottom