Barabara za zege na Barabara za rami ipi ina ubora zaidi?

Bitoz

JF-Expert Member
Aug 27, 2015
30,823
126,549
Habari za week end waungwana
Siku hizi inaonekana barabara za zege zimeanza kushika kasi mfano mmojawapo ni barabara ya mabasi yaendayo kasi na kipande cha barabara inayoelekea Hospitali ya Hubert Kairuki kule Mikocheni jijini Dar es salaam nacho sasa hivi kimepigwa zege

Naomba kujuzwa kuhusu:
1/ Kati ya barabara ya lami na ya zege ipi ni gharama ?

2/Kati ya barabara ya lami na ya zege ipi ni imara?

3/Kati ya barabara ya lami na ya zege ipi ni rafikiI kwa watumiaji mfano magari na waenda kwa miguu ?
Natanguliza shukrani
 
Bara bara ya zege ni imara na ghali zaidi kuriko barabara ya lami..nakumbuka mlima kitonga kabla ya kuwekwa zege ile lami iliyokuepo ilikua inabonyea sana upande mmoja na kusababisha ajali..kwa Nchi zingine kila zaidi ya km 200 utakutana na zege la km 20 au zaidi kwa ajili ya kupoza tairi ambazo zimepata joto ulipokua unaendesha katika lami...
 
Boo cape ni mji upo cape town wengi wanaenda kushangaa hiyo town ipo mlimani bara bara zake za kufika katika makazi yaliyopo mlimani wameweka zege la kutosha na mawe madogo madogo yalio katika zege ili kufanya gari isiteleze au wapita kwa miguu pia wapite kwa urahisi kama ingekua ni lami ingekua shida..
 
Nimekuelewa vizuri sana mkuu...Big up
 
Pale kitonga lami ilichemsha pakapigwa zege pakawa safi. Barabara za zege ni cheap kuliko za lami
 
Wenzako wote wamesema zege ni expensive......ww unadai ni cheap hebu fafanua tukuelewe
 
Habari za week end waungwana
Siku hizi inaonekana barabara za zege zimeanza kushika kasi mfano mmojawapo ni barabara ya mabasi yaendayo kasi na kipande cha barabara inayoelekea Hospitali ya Hubert Kairuki kule Mikocheni jijini Dar es salaam nacho sasa hivi kimepigwa zege

Naomba kujuzwa kuhusu:
1/ Kati ya barabara ya lami na ya zege ipi ni gharama ?

2/Kati ya barabara ya lami na ya zege ipi ni imara?

3/Kati ya barabara ya lami na ya zege ipi ni rafikiI kwa watumiaji mfano magari na waenda kwa miguu ?
Natanguliza shukrani

Ukiona Barabara imejengewa na zege ujue hiyo sehemu inamajimaji, kwanza inawekewa zege halafu inamwagiwa cement baadaya ya miezi 3, 6 hata mwaka halafu inakuja kuwekewa lami. Sio kwamba ikiwekwa zege ndio imemalizika bado kaz itakuja kuendelea. Hizo zipo sana huku ughaibuni.
 
Kwa hiyo barabara ya mabasi yaendayo kasi ile sehemu kuna majimaji? Na baada ya muda itawekewa lami?.......Sidhani km ni sababu
 
Ile barabara ya kwenda kwa kasi ya kibongobongo wamechemsha kuweka zege na vikuta virefu vinavosumbua hata jinsi ya kuruka kwake hasa kwa akina mama.

Mwanzo nilijua kunataka kuwekwa matreni na njia za chuma, nimeshangaa baada ya kuona ni mabasi ya kawaida sana tena tofauti na ya wenzetu yenye gorofa na yanapita kwenye barabara za kawaida.
 
Boo cape ni mji upo cape town wengi wanaenda kushangaa hiyo town ipo mlimani bara bara zake za kufika katika makazi yaliyopo mlimani wameweka zege la kutosha na mawe madogo madogo yalio katika zege ili kufanya gari isiteleze au wapita kwa miguu pia wapite kwa urahisi kama ingekua ni lami ingekua shida..
Mkuu, hebu weka na picha kudhibitisha usemi wako.
 
Kwa hiyo barabara ya mabasi yaendayo kasi ile sehemu kuna majimaji? Na baada ya muda itawekewa lami?.......Sidhani km ni sababu

Mara nyingi huwa ni hivyo ukiona sehemu imetiwa zege ujue hiyo sehemu inakuwa na majimaji au ardhi yake ni ya majimaji. Sababu ya kuwekwa zege lenye cement ni kuyanyonya au kuyakausha maji hiyo sehemu. Kama ikiwekwa lami sehemu yenye majimaji bila ya kuweka zege likaushe hayo maji basi baada ya muda kuna kuwa na kibonde au panadidimia. Lina wekwa kwanza zege then baada ya muda wanatandika lami. Na itategemea na hilo zege litakavyokausha hayo maji kama ni miezi 3, 6 hata mwaka halafu panakuja kuwekwa lami.
 
Back
Top Bottom