Barabara ya Rusahunga - Rusumo ifungeni tu ieleweke

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,879
35,888
Baada kupunguza safari zisizokuwa na ulazima kuitikia wito wa tuliowapa dhamana kwa yaliyojuu ya uwezo kuhusiana na uhai wetu, hatimaye nimejinafasi kutembelea pande za magharibi mwa Tanzania kujionea yanayojiri. Utalii si lazima kupokelewa na daktari bingwa KIA, JKIA au CIA.

Kwamba mkuu aliwahi kupiga simu kwa mbunge wa Ruangwa mkutanoni akaahidi barabara ya lami pande za huko?

Loooo! Mbona hiyo ni propaganda ya daraja la chini mno kama huku kwingine kupo katika hali hohehahe kama hii?

Kumbe huku kwa sababu ya ubovu wa barabara usiomithilika ajali ni kila leo?

Kumbe huku ambako hata madereva wetu kwenda DRC na Rwanda bado cha moto kuhusiana na Corona wangali wanakipata baada ya kuwa wameonjeshwa pepo vilivyo barabarani kwanza?

Ama kweli staajabu ya Mussa!

Hivi madereva wetu walipaswa kulalamikia madhila yatokanayo na Corona Rwanda, au kisisina mtoa roho za watu wanayekabiliana naye kila leo wakiwa njiani kwenda kujitafutia riziki zao na kusukuma gurudumu la uchumi wa nchi hii mbele?

Kwamba wanaopita njia hii na magari yao wamelipa kodi na tozo zote bila hata ya kujali kuwa pana mdororo wowote wa uchumi uliotokana na Corona na kuwa eti wanapita humuhumu na kimya kimya kuliko hata kondoo?

Kwamba maeneo haya yanatokea wabunge ambao ije October 2020 wanaomba tena ridhaa ya kurejea ofisini? Mbona aheri waache ijulikane wazi kuwa ubunge labda kama ni wa ni wa Chatto ndiyo dili lakini siyo huku?

Kwamba serikali ya awamu hii inajisifia kwa ujenzi wa barabara? Labda kama ni za Ruangwa, Chatto, na za Mfugale. Katu siyo huku! Akheri barabara hii wangeifunga tu ikaeleweka tu kuwa hakuna barabara huku.

Hapa ninaweka moja ya ajali za jana tu kuonyesha madhila wayapatayo ma transporta huku, kwa sababu tu ya ubovu wa barabara uliopitiliza:

IMG_20200705_171809_169.jpg



Kwamba pana mamlaka yenye kuhusika hali ya barabara kwa jina la TANROADS? Basi taasisi hiyo labda haitambui kuwa kipande hiki kama kipo hapa nchini na kipo kwenye himaya yao.

Juzi, katika ukanda huu huu gari la serikali lililokuwa kwenye msafara wa waziri wa madini limepata ajali na kujeruhi vibaya waliokuwamo. Sababu ya ajali ikiwa ubovu mkubwa huu wa barabara usiomithilika.

Kwa vile Corona si janga la taifa tena, yawezekana ni muda sasa kukawepo angalau na simu kama ya Ruangwa kuangazia barabara hii ambayo aghalabu ni muhimu sana kwa nchi hii ambayo sasa iko kwenye uchumi wa kati.

Hala hala kabla ya hatari, kama hamuwezi kuyarekebisha maeneo ya Rusahunga Nyamalagala, Ngazi Saba, na kipande cha Nyakahura Nyabugombe, basi ifungeni tu barabara hii. Vinginevyo haiko mbali siku ya kuhitaji uwajibishwaji wenu kwa mali na maisha yanayoendelea kutekeketea huku.

Picha zaidi ni taswira ya kipande hiki cha barabara takribani 90km tu, Isaka - Rusumo njia kuu kwenda Rwanda, Burundi na DRC:

IMG_20200705_164617_078.jpg
 
Poleni sana kwa hiyo changamoto. Ngoja tuone mzee ataamkaje! maana ndipo tulipokifia kwa sasa kama Taifa. Hakuna cha Tanroad au Tarura! Ni suala la mtu mmoja tu kutoa neno, na hiyo barabara inatengenezwa mara moja.
 
Poleni sana kwa hiyo changamoto. Ngoja tuone mzee ataamkaje! maana ndipo tulipokifia kwa sasa kama Taifa. Hakuna cha Tanroad au Tarura! Ni suala la mtu mmoja tu kutoa neno, na hiyo barabara inatengenezwa mara moja.

Kwa kweli mtu mmoja huyu ni shida.

Kama huku kuko hivi Ilikuwa nini mantiki kwa simu ile ya Ruangwa? Au siasa na kampeni tu hata katika masuala nyeti?
 
Kuna tetesi uwenda ni SRABAG GMBH wakapewa hiyo tender sio muda mrefu ndo maana mkandarasi alipomaliza kipande cha kwnz Ushirombo - Lusaunga bado hajatoa vifaa vyake ata asphalt plant hawajafungua so nafkir ipo kweny mchakato
 
Kumbe STRABAG wameishia Lusahunga,mi nilifikiri wanafika mpaka Rusumo. Wawape tuu maana wapo site huko kuliko kumpa mwengine aanze mambo ya logistic
 
Kumbe STRABAG wameishia Lusahunga,mi nilifikiri wanafika mpaka Rusumo. Wawape tuu maana wapo site huko kuliko kumpa mwengine aanze mambo ya logistic

Wawape au wasiwape haya mashimo barabarani kwa kiwango kikubwa hivi cha kusababisha ajali, uharibifu na mashaka makubwa kwa maisha ya watu yanasubiria Strabag kupewa kandarasi?

Tuwe wakweli kwetu sisi wenyewe kwa hali ya sasa bila kuona huwezi kuamini!

Hii wangeifunga tu, kwa kweli kwa sasa hakuna barabara hapo.

Ni aibu kuwa pana mamlaka yoyote yenye kuwajibika directly au indirectly na barabara hii. Ya kuwa eti mamlaka hiyo inapokea mshahara na marupurupu kwa shughuli hiyo.
 
Back
Top Bottom