Barabara haijamalizika kujengwa wala haijakabidhiwa rasmi kwa wahusika mshaanza kuiponda, hebu kuweni na subra kidogo, akaa.
tatizo lililopo ni siasa za ujingaujinga tu, kila mtu alimkubali John Pombe Magufuli alivyofanya kazi kwenye sector ya barabara, lakini kwa kuogopa asiwe rais kwa sababu ajaandaliwa au hayupo kwenye ukoo huo wa kiraisi, JK akaamua kumtupatupa tu, ili asionekane umuhimu wake, ukweli ni kwamba hata kama ni msaada, uwezi kukubali msaada wa ujinga ujinga tu, hakuna kiongozi ambaye yuko commited kwenye mambo ya barabara kama alivyokuwa JP Magufuli, na alikataa kufungua miradi mingi tu ambayo ilikuwa substandard,
NCHI HII SASA HAINA MWENYEWE NA UTASHANGAA RAISI WA NCHI ANAENDA KUIFUNGUA HII BARABARA AKIWA PAMOJA NA WAZIRI WA MIUNDO MBINU NA WASHAURI WENGINE WA RAISI, NI AIBU
Barabara haijamalizika kujengwa wala haijakabidhiwa rasmi kwa wahusika mshaanza kuiponda, hebu kuweni na subra kidogo, akaa.
Hatupaswi kupuuzia mashaka walionayo watumiaji wa barabara kwa sababu tu eti sio wataalamu. Ni kweli wataalamu wanaweza kutupa tathmini nzuri zaidi, lakini hili halina maana tusio na utaalamu huo hatuwezi kujua kitu kizuri!
Waswahili wana msemo, ''Hadia japo ya kokwa la tende ni hadia'', sasa nyinyi mnapiga kelele kwa kibara-bara cha hadia? si mtowe pesa zenu za madafu halafu mjenge yenu, muisimamie mnavyopenda? Khaa, nawashangaa, mnasaidiwa halafu mnajitia wajanja, si mngejenga yenu? mnachonga kwa cha kuomba? mngekuwa mnataka class A road mngeijenga wenyewe. Tembeeni duniani muone, hata hapo Japan waliotusaidia haka ka barabara wana classes kwenye bara bara zao, tusitegemee barabara iliyo bora kwa kuomba-omba. Tumeomba, tunachopewa turidhike, kama hatukitaki tusiombe tena. Kuchonga tuwache.
......duuuhh.........sijui hata kama wee jamaa unaelewa unachoandika......hii hapo juu ni argument ya mwaka 2009...........naanza kukubali kauli ya Nyani...........NDIVYO TULIVYO!!!
Waswahili wana msemo, ''Hadia japo ya kokwa la tende ni hadia'', sasa nyinyi mnapiga kelele kwa kibara-bara cha hadia? si mtowe pesa zenu za madafu halafu mjenge yenu, muisimamie mnavyopenda? Khaa, nawashangaa, mnasaidiwa halafu mnajitia wajanja, si mngejenga yenu? mnachonga kwa cha kuomba? mngekuwa mnataka class A road mngeijenga wenyewe. Tembeeni duniani muone, hata hapo Japan waliotusaidia haka ka barabara wana classes kwenye bara bara zao, tusitegemee barabara iliyo bora kwa kuomba-omba. Tumeomba, tunachopewa turidhike, kama hatukitaki tusiombe tena. Kuchonga tuwache.
Na mimi naunga mkono hawa jamaa bado hawajakabidhi rasmi hii barabara, wanachofanya sasa ni kuwa wanaangalia mapungufu na kuyarekebisha kuweza kupata barabara iliyo bora lakini wananchi kwa vile wameruhusiwa kuitumia barabara ile wanafikiri tayari imemalizika. Kuweni na Subira.
Mkuu Elusive barabara ambayo tayari imetiwa lami na ina mabonde yanayokatisha tamaa, unangoja ukabidhiwe ndo ujue kuwa ni mbovu?
Huko ni kutoutendea ukweli haki , kitu kibovu kunaonekana mapema , barabara ya Kilwa bomu!
....Au ndio yale mambo yetu yaleee 10%%%%??!!This is a very good contribution,barabara yenye unene wa lami ya 50mm,wasimamizi wako wapi? Watanzania tusiliwe wakati tunaona wenyewe.Drainage hii mimi sijawahi kuona pengine kwa barabara za nje ya mji.
Kwa hiyo unataka kusema hii barabara ni sadaka na kama ni sadaka basi haipaswi kuwa bora? Mbona huwa tunasikia kuwa sadaka unatoa kilicho bora? Kama tutaendelea kusaidiwa kwa mabomu ili tusiseme kama kitu ni bora au la ni afadhali tusisaidiwe kabisa!
Mimi siyo kama nawatetea hawa KAJIMA, lakini nakumbuka miaka ya nyuma ilikuwa kampuni ya mwanzo ya KiJapan kutujengea barabara, kama mnakumbuka walijenga kipande cha barabara pamoja na daraja la Selander na kipande cha barabara iliyokuwa korofi enzi zile za MECCO cha Jangwani na walifanya kazi nzuri sasa sielewi kama KAJIMA ya sasa ndiyo ile ya zamani au vipi.
kuna siku alihojiwa akadai hajalipwa.Hii nchi inabidi tuwekeze kwenye uongozi hasa tukiwaleta wachina waje kusimamia utendaji serikalini, baada ya kufungwa upande mmoja baadhi ya sehemu ya barabara ya Kilwa na kusababisha usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa barabara hiyo ili kupisha marekebisho .
Hatimaye hizo sehemu zilikamilishwa na wajenzi lakini cha ajabu ndani ya wiki mbili tumeshuhudia contractor yule akiweka viraka katika sehemu zilezile alokamilisha ujenzi uliodumu karibu miezi 10, kaweka viraka kuanzia maeneo ya sabasaba hadi Mtoni Mtongani, mambo ya ajabu sana.
Sijui ni dharau au uwezo mdogo? hivi watu hawa si huko China tunasikia wanapigwa risasi?
Hii barabara itakua inakarabatiwa miaka yote?mbali na usumbufu tunaopata kwa ile style ya kufunga upande wa kutokea Mbagala na kuruhusu watokao Mjini.
Huyu Mkandalasi ni tatizo kubwa tunasubiri tuone reaction ya serikali kwa hili.
kuna siku alihojiwa akadai hajalipwa.