DOKEZO Barabara ya Inyala - Simambwe iliyojengwa kwa kiwango cha lami, mwaka wa pili tangu ikamilike tayari ina mashimo

DOKEZO Barabara ya Inyala - Simambwe iliyojengwa kwa kiwango cha lami, mwaka wa pili tangu ikamilike tayari ina mashimo

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Nipe Maji

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2025
Posts
335
Reaction score
190
Barabara ya Inyala - Simambwe yenye Kilomita 16.7 Mkoani Mbeya iliyojengwa kwa kiwango cha lami kwa shilingi bilioni 7.05 ikiwa mwaka wa pili sasa tangu kukamilika kwa ujenzi wake tayari imeanza kuwa na mashimo.

Kwenu TARURA. Je, ilistahili kujengwa kwa kiwango hiki cha kuwa na mashimo ndani ya miaka miwili tu au tumechezewa hapa?

Vipi baada ya miaka mitano barabara hii itakuwa na hali gani? Je, mnajenga barabara ili baadaye mje kuziba viraka?
1766987388539.png

1766987373942.png
1766987431860.png

1766986769516.png

1766986803673.png
 
Kwa sasa, barabara standard inajengwa 1KM kwa 1bn.

Naona hiyo barabara imejengwa 2KM kwa 1bn. Kivyovyote haiwezi kuwa imara.
 
Hili jambo lipo nchi nzima.kila MRADI upo chini ya kiwango hata RAIS tuliye Naye yupo chini ya kiwango
 
Haya mambo yanakera.
Ni kweli yanakera lakini shida hatuna uwezo wa kuwawajibisha na wala hakuna hatua zitakazo chukuliwa zaidi ya kuwahamisha wahusika kuwapeleka mahala pengine kwa minajili ndio uwajibishaji huo. Watawalia tutapiga makofi baada ya kuambiwa kunaundwa tume basi kwisha habari.
 
Back
Top Bottom