Barabara ya Chanika inasubiri hisani ya Dkt. Philip Mpango?

Barabara ya Chanika inasubiri hisani ya Dkt. Philip Mpango?

Abdull Kazi

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2012
Posts
344
Reaction score
306
Sisi wakazi wa Chanika kwa sasa tunapata taabu Sana kwa barabara yetu Kutokea Kona ya Pugu kuelekea Chanika.

Barabara hii ilikuwa inaangaliwa mara kwa mara wakati Makamu wa Rais alipokuwa akipita mara kwa mara kwenda kuangalia familia yake.

Kwa sasa kiongozi huyo hapiti na hakuna matengenezo yoyote,kuna mashimo mengi Katikati ya Bara Bara,inaharibu magari wananchi wanapata kero ya usafiri na mamlaka zimefumba macho.

Swali langu kwa wahusika je huduma hii muhimu kwa Sisi watumiaji wa barabara hiyo,ilikuwa I apatikana kwa hisani ya Dk Mpango au kwa sababu ni huduma muhimu tunayostahili kupata kwa sababu utanzania wetu?
 
Back
Top Bottom