Barabara mpya katikati ya makazi, Kibamba DSM

Barabara mpya katikati ya makazi, Kibamba DSM

Joined
Nov 17, 2011
Posts
40
Reaction score
7
Wadau, sina uhakika maana sijapata taarifa rasmi.

Kuna watu wamepita maeneo mbalimbali ya Kibamba Dar es Salaam (Majuma mawili yaliyopita) na kuweka alama zinazoonyesha hatari. Kuulizwa wamesema kuna barabara kubwa ya malori inategemea kupita eneo hilo kutokea Mbagala kuungana na Barabara ya Morogoro.

Maeneo waliyoweka hizo alama kwa kiasi kikubwa ni katikati ya makazi ya watu ambapo kama ni kweli ni nyumba nyingi sana zitaathirika.

Suala langu hapa ni kuweza kufahamu ukweli wa hili swala kutoka kwa anayefahamu hili.

Akhsanteee kwa msaada.
 
Unachotaka kufahamu ni kuhusu nini mkuu? Kuhusu kujengwa kwa barabara? Kuhusu kuwekwa hizo alama? kuhusu kubomolewa hizo nyumba nyingi? Au kuhusu kuathirika kwa hao watu na ni namna gani wanaweza kufidiwa? Anywa, mimi nitazungumzia kivingine, unajua kila mtu hata wewe analalamika kuwa jijini halikua na plan na pia barabra za kutokea na kuingia jijini ni chache. Mimi naona kama hili zoezi lipo itakuwa sawa na litapunguza foleni kwa kiasi fulani. Lakini pia ni lazima tukumbuke kila penye maendeleo kama hayo ni lazima kuna watu wataumia, kama hao ambao nyumba zao zitavyunjwa. Pamoja na haya yote ni lazima serikali ijipange kuhakikisha waathirika wanalipwa fidia na kupewa viwanja sehemu nyingine ili wakaendelee na maisha yao. Yangu ni hayo tu
 
Je, kiwanja chako kimepimwa na kupewa hati!? ...sio vile vipimo vya wajumbe wa ccm bali vile vya master plan ya mji.
Kama uliuziwa kashamba na kukajenga hata ghorofa basi ujue wakati wowote kanaweza kubomolewa kupisha vipimo sahihi vya miji. Hawawezi kubomoa bure ni lazima wakufidie lakini sio kama wale wa surveyed areas bali ni fidia za kuumizana.
 
Unachotaka kufahamu ni kuhusu nini mkuu? Kuhusu kujengwa kwa barabara? Kuhusu kuwekwa hizo alama? kuhusu kubomolewa hizo nyumba nyingi? Au kuhusu kuathirika kwa hao watu na ni namna gani wanaweza kufidiwa? Anywa, mimi nitazungumzia kivingine, unajua kila mtu hata wewe analalamika kuwa jini halikua na plan na pia barabra za kutokea na kuingia jijini ni chache. Mimi naona kama hili zoezi lipo itakuwa sawa na litapunguza foleni kwa kiasi fulani. Lakini pia ni lazima tukumbuke kila penye maendeleo kama hayo ni lazima kuna watu wataumia, kama hao ambao nyumba zao zitavyunjwa. Pamoja na haya yote ni lazima serikali ijipange kuhakikisha waathirika wanalipwa fidia na kupewa viwanja sehemu nyingine ili wakaendelee na maisha yao. Yangu ni hayo tu

Asante sana Manizzle kwa maelezo yako.
Kimsingi ninapenda kufahamu ukweli wa hilo nililolisikia ili nisijeingia mkenge kwa kununua eneo ambalo nimelikusudia pia iwe msaada kwa wengine.
Naunga mkono juhudi za kuongeza idadi ya barabara hasa jijini Dar, ila sina uhakika na taarifa kuwafikia wananchi/wadau kisawasawa. Kwa mfano katika hili nililosema, wananchi hakuna mwenye uhakika na kinachoendelea. Pia wanaotekeleza hawana maelezo sahihi zaidi ya kusema ni barabara ya malori.
Binafsi ningependa kufahamu ni barabara ambayo tayari ilisha amuliwa au ni mapendekezo tuuuu. Maeneo hayo kuna ujenzi unaendelea kila kukicha na hakuna mwenye taarifa rasmi. Linapokuja swala la fidia sijui nani atastahili maana hakuna taarifa rasmi ya kusitisha uendelezaji wa maeneo hayo........maswali ni mengi.
 
Mkuu nakushauri usinunue kiwanja ambacho hakijapimwa na mamlaka husika, inagawa asilimia kubwa ya makazi ya Dar mengi hayajapimwa. Lakini athari zake zinaweza zisitokee leo wala kesho, lakini tambu atu ipo siku kuna jambo linaweza tokea na likaharibu mfumo wako mzima wa maisha. Nakushauri, nenda manispaa wanakua na ramani za jijini zima, huko watakuonyesha hilo eneo unalotaka kununua kama limetwngwa kwa ajili ya matumizi gani? Kama ni makazi nunua then rasimisha kwa gharama zako mwenyewe, maana ukingoja serikali ikupimie utasubiri sana.
 
Unachotaka kufahamu ni kuhusu nini mkuu? Kuhusu kujengwa kwa barabara? Kuhusu kuwekwa hizo alama? kuhusu kubomolewa hizo nyumba nyingi? Au kuhusu kuathirika kwa hao watu na ni namna gani wanaweza kufidiwa? Anywa, mimi nitazungumzia kivingine, unajua kila mtu hata wewe analalamika kuwa jini halikua na plan na pia barabra za kutokea na kuingia jijini ni chache. Mimi naona kama hili zoezi lipo itakuwa sawa na litapunguza foleni kwa kiasi fulani. Lakini pia ni lazima tukumbuke kila penye maendeleo kama hayo ni lazima kuna watu wataumia, kama hao ambao nyumba zao zitavyunjwa. Pamoja na haya yote ni lazima serikali ijipange kuhakikisha waathirika wanalipwa fidia na kupewa viwanja sehemu nyingine ili wakaendelee na maisha yao. Yangu ni hayo tu
Jini = Jiji...
Maana wengine wasije fikiri kuna Jini mla watu huko ambaye hakuwa na plan za barabara!!
 
Back
Top Bottom